Kuahirishwa kwa Mechi ya Simba na Yanga, Bodi ya Ligi Kuu ijitafakari

Kuahirishwa kwa Mechi ya Simba na Yanga, Bodi ya Ligi Kuu ijitafakari

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2014
Posts
631
Reaction score
1,577
Uamuzi wa kamati ya uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) kuahirisha mchezo namba 184 kati ya Young Africans (Yanga SC) na Simba SC uliokuwa uchezwe tarehe 08 Machi 2025, haukuzingatia hasara mbalimbali zilizotokana na kuahirishwa kwa mchezo huo, ikiwemo nafasi ya mashabiki, wafanyabiashara, warusha matangazo, wapenzi wa soka, na maendeleo ya soka nchini kwa ujumla.

Kwa mujibu wa Katiba ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), ibara ya 55 (2) inatoa jukumu kwa Bodi ya Ligi kusimamia ligi kuu na kuhakikisha timu zinaheshimu sheria, kanuni na maamuzi ya TFF. Kanuni namba 15 (3) inasisitiza kuwa ratiba ya ligi itatangazwa na Bodi ya Ligi na itabadilishwa tu kwa dharura au sababu za msingi. Hata hivyo, Bodi ya Ligi imekuwa ikibadili ratiba mara kwa mara bila dharura wala sababu za msingi, jambo linalosababisha hasara kubwa kwa wadau.

Kuahirishwa kwa mchezo kulitokana na madai ya timu ya Simba SC iliyozuiwa kufanya mazoezi ya mwisho katika uwanja kama kanuni na taratibu za mchezo wa Soka zinavyoeleza, aidha upande wa Yanga SC katika taarifa yake rasmi kwa umma ilieleza inatambua mechi ipo palepale na kwamba haitakuwa tayari kucheza mechi hiyo siku nyingine.

Soma Pia: Bodi ya Ligi kuu yaahirisha Mechi ya Derby kati ya Yanga dhidi ya Simba
WhatsApp Image 2025-03-09 at 17.09.20_b140f388.jpg
ACT Wazalendo inaona mwenendo huu wa Bodi ya Ligi umejaa malalamiko kutoka kwa wadau wengi, kwa kuwa imekuwa ikiongozwa na utashi wa timu hizo za Kariakoo, jambo linaloharibu taswira ya ligi yetu, heshima ya Tanzania kisoka, na kuleta hasara kwa wadhamini, mashabiki na wafanyabiashara.
ACT Wazalendo inaitaka Bodi ya Ligi iliyopo madarakani kujitafakari kama inafaa kuendelea kusimamia ligi kuu ya Tanzania au inapaswa kujiengua.

Pili, ACT WazalendoTunaitaka Bodi ya Lingi kuendesha ligi kwa kuzingatia na kusimamia sheria na kanuni bila uonevu wala upendeleo kwa timu yoyote.

Tatu, Bodi ya Ligi ichukue hatua za haraka na za haki kwa mujibu wa kanuni ya 31 (1.1 hadi 1.8), ikiwa ni pamoja na adhabu kama vile kupoteza ushindi, kushushwa madaraja mawili, kutozwa faini ya Milioni 3, na kutopata gawio la mchezo husika.

Nne, TFF ifanye tathmini ya madhara yote yaliyotokana na kuhairishwa kwa mechi hii na waathirika wote walipwe fidia.

Mwisho, ACT Wazalendo inataka kuona Mpira wa Tanzania unaendelea kukua, kupata heshima na kusaidia kukuza uchumi wa mtu mmojammoja, vilabu na Taifa kwa ujumla, hatutafumbia macho matukio yote yatakayohatarisha shabaha hiyo.

Imetolewa na
Ndg. Monalisa Joseph Ndala
Naibu Waziri Kivuli wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
09 Machi 2025.
 
Kuna madudu mengi ya hii nchi KUANZIA kwenye ziara ya mama mpaka ndani ya serikali yake. Mpira ni jambo jingine .. yanayotokea yamepangwa yatokee yafunike madudu yote hayo.. Mpira umegeuzwa kuwa Imani na maisha ya watu, hatuna Cha kuwaza Zaid ya mpira?Mimi nisiye na Banda la kuonesha mpira , mpira unanisaidia Nini?
 
TFF na bodi ya ligi wote ni wana Simba na imefika hatua maamuzi ya timu yamekuwa na nguvu kuliko kanuni tutegemee migomo mingi Sana kimfano yanga nae asipo enda uwanjani ni nini kitafuata?
 
Naona Simba na Yanga wote ni wakubwa kuliko bodi ya ligi ndio maana wanafanya maamuzi yoyote yale
 
Nimewahi kushuhudia mengi Duniani ila kwa maamuzi yanayofanyika na baadhi ya viongozi sijui huwa wanawaza nini?

Viongozi mjitafakari kama hizo nafasi mnazozikalia na kuzitumia mnahitaji kuendelea kukaa kwenye hizo nafasi....

TFF inatoa taarifa na Bodi inatoa taarifa na zinakinzana.... Nashindwa kuelewa nani amsikilize mwenzie?
 
Mimi nimechoka kabisa na aibu hii kama nchi,eti ligi yetu ni ya nne afrika kwelii?????? Kwa ujinga huuu?????? shame of you
 
Kila sehemu Nchi Inachezewa na Wajinga wajinga.
Mpira Wa miguu Umeingiliwa na wajinga wajinga.
Serikalini kuna watu wamepewa Mamlaka Lakini Wanajiona Wanaweza Kila kitu na Kutoa Maamuzi kwa Kuangalia Mapenzi yao kwa Club Fulani.
Ligi Inaendeshwa Kihuni kuanzia Marefa Mpaka wasimamizi wa Vilabu Husika.
Siasa Na mpira wapi na wapi !
 
Mimi nimechoka kabisa na aibu hii kama nchi,eti ligi yetu ni ya nne afrika kwelii?????? Kwa ujinga huuu?????? shame of you
sio ya nne ilikuwa ya tano mwaka jana mwaka huu imeshuka imekuwa ya sita na wakiendelea hivi itashuka mno!
 
Back
Top Bottom