CONTROLA
JF-Expert Member
- Sep 15, 2019
- 7,001
- 23,449
Kuna kitu kinachanganya sana watu wasio na ajira/waliomaliza vyuo wanaotamani siku moja kuwa wafanyabiashara wakubwa na wajiendeshe sio kuendeshwa, akili zao zinasikia mengi sana kitu kinachopelekea kubaki njiapanda sasa leo acha nifafanue kitu kimoja kwa faida ya nyie ambao hamuelewi tunaposema "Kuajiriwa ni mzigo" watu "wajiajiri" wenyewe.
Acha nianze na kuchambua hiyo title hapo juu inayosema
Kuajiriwa sio dhambi, angalia malengo yako: Ndio kuajiriwa sio dhambi tena sio dhambi kabisa japo kila mahali watu tunapinga watu wasiajiriwe,ila tukirudi kwenye uhalisia kama wewe ni mtu una malengo yako tu assume moyoni mwako unatamani siku 1 kuja miliki mgahawa kama wa shilole "shishi food", leo hii
Sio mbaya kabisa kama utaanza kukubali kuajiriwa kwenye migahawa/mama ntilie na sehemu zote zinazojihusisha na huduma ya chakula,sio mbaya kwa sababu unapoajiriwa unapata "uzoefu" na katika kitu muhimu kuliko vyote unahitajika kuwa nacho katika dunia ya kujiajiri ni uzoefu wako na kile
Unachotaka kwenda kukianzisha,kwa hiyo unapoajiriwa utapata uzoefu wa kazi inafanywaje,faida inapatikanaje,vyakula vinapikwaje, wateja wanapenda nini,hawapendi nini,nk nk. Utaweza jifunza vitu na siri ambazo leo hii ukimfata Shilole akueleze siri ya mafanikio yake (kamwe hatokaa akwambie).
Kwa maana hiyo,usidharau ajira Ifanye kwa bidii lakini kumbuka unapokuwa hapo kazini kwako elewa upo darasani, elewa kwamba mbali na kwamba unatafuta pesa ila tambua kua siku moja utakua na ofisi ya namna hiyo hivyo jiongeze, jifunze, uliza maswali, fanya kazi ambazo hata hukuambiwa ufanye
Fanya ili ukikosea uelekezwe jinsi ya kufanya,sio unaajiriwa kufanya kazi ya kuosha vyombo na usafi Basi na wewe ndio una deal na vyombo na usafi Huto toboa,hakikisha unaosha vyombo chap chap,usafi chap chap kisha unaingia jikoni unawauliza "jamani niwasaidie kupika nin/kuandaa nini?
Watakwambia kata karoti au Hoho, ukianza kukata tu Mpishi mmoja atakushautia "ndio unakataje karoti hivyo"? atakwambia Hii ni hotel karoti zinakatwa hivi,vitunguu vya kachumbari vinakatwa hivi (tayari usha pata somo hapo) ukirudi nyumbani wewe ni mfanya usafi/muosha vyombo ila tayari utakua
Unajua kumbe karoti za kitu flani zinakatwa hivi na hivi huo ndio "uzoefu wenyewe" utajua vingi,utafundishwa vingi kikubwa tu unapokua umeajiriwa usikae kama gogo penda kujiongeza "kiherehere",nakwambia hivyo kwasababu sio mara 1 wala mara mbili kipindi naajiriwa nilikua mzee wa kujiongeza sana na
Kila nikijiongeza boss akija ananibamba nafanya ile kazi niliyokuwa nimeenda tu kusaidia anakuta nimefanya kwa ubora basi unamsikia anashangaaa heeee CONTROLA na wewe unaweza kufanya hivi vizuri kumbe? Unamjibu ndio boss,basi unamsikia anasema kazi yako tutatafuta mtu mwingine wewe
Ungana na hawa fanyeni hii kazi. (najikuta nimepandishwa cheo ki utani utani tu) kumbuka cheo kikipanda na Posho inapanda upo hapo? Sasa jiulize Je ingekuaje ningekuwa nimekaa kule kule kwenye ile kazi yangu kisa tu nimeshaimaliza so sina kazi nyingine? Ningeonwa saa ngapi na Boss?
Kikubwa angalia malengo yako usibweteke popote pale utakapokuwa umeamua kwenda kufanya kazi hata kama ni kujitolea hakkisha unapata "uzoefu" maana hamna chuo kinafundisha "uzoefu" ukitaka uzoefu wa kitu chochote lazima uingie ukifanye kwanza wewe mwenyewe.
Epuka malipo ya mwisho wa mwezi: Bwana mimi katka kuajiriwa kwangu nilishalipwa malipo yote nilianza ya mwezi nikaja malipo ya wiki kisha ya siku ila katika njia zote hizo 3 za malipo hakuna njia nzuri niliipenda kama "malipo ya siku" unapolipwa malipo ya siku japo umeajiriwa ila amini nakwambia Boss hawezi kukwambia fyeee wala fyuuuu.
Ila malipo ya wiki na mwezi haya malipo ukiyakubali kubali tu kua boss kwako atakua MUNGU mtu yani utajikuta unamsalimia asubuhi mchana jioni ili tu asije akakasirika akakufukuza kazi kabla hujakamilisha "wiki yako" au kabla hujakamilisha "mwezi wako".
Maboss wanaolipa wafanyakazi zao malipo kwa wiki/mwezi hawa ni maboss vichefu chefu nawaitaga maana hawa wanaangalia faida wiki hii au mwezi huu kapata kiasi gani akichungulia akiona labda alijiwekea kila mwezi akaunti iwe ina mil 3 (faida) then akachungulia akaona faida ipo 2mil asee nakwambia nyie mshahara wenu wa mwezi 3 mtapewa ikifika mwezi wa 4 tarehe 13. WHY?
Kwa sababu BOSS wenu ni mfanyabiashara,hawezi kubali eti awafurahishe nyi wakati yeye kampuni yake haijaingiza faida ya kueleweka na kwakua umeshachagua kufunga ndoa na boss wako kwa "malipo ya mwezi" huna la kufanya,utalalamikaaa ila kazini utabaki,na jinsi maboss wa kulipa kwa mwezi walivyo na sifa wanamtindo wa kusainisha watu mikataba ka kipengele flani eti "ukitaka kusitisha mkataba utoe taarifa kwa muajiri 1 month or two before"
Sasa balaa ni kwamba umeshatoa taarifa 1 month or two before halafu mshahara wako anao boss,Bwana weee utaipenda nakwambia kwenye malipo yake. kwa hiyo eneo hili la malipo kama umeamua kujitosa kwenye kuajiriwa jaribu kuchagua/tafuta kazi za malipo per day (ni nyingi sana tu)
Fanya kazi yako kwa bidiii jioni ukiwa unaondoka unapewa chako huyooo unasepa,kesho unarudi tena kazini.Pesa yako ya siku iwekee malengo kama unataka kutafuta mtaji wewe mwenyewe unajua unahtaji mtaji wa kiasi gani so kusanya hela yako ukifika muda hela imetimia una uhuru wa kuacha kazi bila hata kuomba ruhusa mtu,Japo sikushauri uache kazi kienyeji (usitukane mamba).
ila usikubali haya makazi/vibarua vya mwezi,juzi kati nilisoma thread moja ya jamaa ameamua kuileta fursa humu kuwa "vijana kwa mwenye uhitaji wa kuvuna chai" nikawa nasoma comment watu wakawa wanauliza malipo yapoje? Jamaa akawajibu kilo 1 sh.ngapi sjui ila hela yako unakusanyiwa unakuja kupewa mwisho wa mwezi kulingana na kilo ulizochuma.
Nilisikitika sana nikasema ebu nitoke kwenye huu uzi nisije andika kitu cha ajabu,maana kuna uwzekano 50/50 watakao chuma hizo chai kutokulipwa kwa wakati mambo yakawa kama ya wauzaji korosho mtwara,wanadai hela wengine hadi na kesho kutwa hawajui hela watapewa lini za korosho zao,ndio nasemaga mimi kama mtu umeamua kutoka jasho iwe kibarua cha kulima/usafi/kupika/kubeba zege/utingo,nk nk
Hakikisha unapewa chako pale pale ukimaliza kabla jasho lako halijakauka,maswala ya njoo kesho,ntakutumia tigo pesa,ntakuwekea kwenye akaunt,nk,nk Weka mkasi. Mtu hawezi kukulipa kwa siku Pita vile katafute kazi pengine.
Sipangiii mtu maisha jamani ila nataka tu kuku kumbusha matapeli wapo aina nyingi,na Muogope tapeli wa Muda wako huyo ni tapeli mmoja ambae ukibahatika kumit nae leo,Sepa na shingo yake.