Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Leo nimepitia sheria ya Ukimwi/HIV iliyopitishwa mwaka 2008 baada ya kusikia mwamba wa Mara huko kafungwa miaka 7 kwa kusambaza Ukimwi makusudi.
Kifungu cha 47 cha sheria hiyo kinasema mtu yeyote kwa makusudi akasambaza virusi vya ukimwi kwa mtu mwingine atakuwa ametenda kosa na akithibitika ametenda hilo kosa anatakiwa kufungwa kifungo kisichopungua miaka mitano na kisichozidi miaka 10.
Kifungu cha 46 kinamhukumu mhudumu wa afya atakayevunja usiri wa taarifa za afya za mgonjwa pia zinamuhukumu mtu yeyote atakayetoa taarifa kuhusu hali ya kiafya ya mtu endapo ameambukizwa au hana HIV/AIDS faini isiyopungua laki tano na isiyozidi milioni moja au kifungo cha miezi 6-12 au vyote kwa pamoja.
Zaidi, nimeambatanisha sheria husika. Kipengele cha hukumu kipo mwishoni...