Kuandika business plan ni kupoteza muda

Kuandika business plan ni kupoteza muda

Atimachie

Member
Joined
Jan 17, 2019
Posts
15
Reaction score
12
Kumekuwa na mafundisho mengi yanayosema ni vizuri kuandika busines plan kabla ya kuanza biashara/mradi,Lakin ukifuatilia kwa undani hakuna business plan hata moja ambayo huwa inaonesha kipindi cha hasara,Na ukifuatilia biashara nyingi hufa ndani ya mwaka wa kwanza,Na wakati huo mtu ana business plan mkononi inayoonyesha angepata faida kubwa saaaana,Nakushauri anza biashara yako hata bila ya business plan,Biashara ni vitendo sio faida ya kwenye makaratasi.Uliza wafanyabiasbara waliofanikiwa Kama walianza kwa kuandika business plan.. ANZA LEO BIASHARA,USINGOJE KESHO.
 
Siku zote biashara ni upate au upoteze! Wakati pale unapoisaka faida mbele yako. Ndipo hasara nayo inapokunyemelea nyuma yako!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Business plan huwa haiendani na biashara mpya inayoanza. Biashara mpya zinahitaji kulelewa kwa muda ili zisimane. Inayondelea inaweza kuandikiwa plan na ikafuatwa.
 
Ni wazi hujui/ hujawahi hata kuandika business plan yeyote kwenye genge lako la vitumbua.

Unajua Vipengele vya Market Analysis na financial plan Projections vina kazi gani??

Nachojaribu kumuelewa huyu jamaa ni kwamba kuwa na business plan peke yake haiwezi kusababisha biashara ikafanikiwa. Kuna mambo mengi sana nje ya business plan ambayo wala huwezi kuyawaza lakini athari zake zikawa kubwa kwenye biashara. Ingekua business plan ni muarobaini, basi tusingesikia makampuni makubwa ya kimataifa yenye top class managers yakifilisika.
 
Mimi nilimuelewa na nilichogundua kwake ni kuwa hajui lolote kuhusu anachojaribu kukijengea hoja.

Wewe pia kujaribu kumuelewa kwa kuiunga mkono hoja yake..ni wazi nawe hufahamu/umekurupuka.
 
Nachojaribu kumuelewa huyu jamaa ni kwamba kuwa na business plan peke yake haiwezi kusababisha biashara ikafanikiwa. Kuna mambo mengi sana nje ya business plan ambayo wala huwezi kuyawaza lakini athari zake zikawa kubwa kwenye biashara. Ingekua business plan ni muarobaini, basi tusingesikia makampuni makubwa ya kimataifa yenye top class managers yakifilisika.
Wachache sana wanaoweza kuelewa hii kitu,Hapa panaitajika mtu mwenye afya akili #TheChoji
 
'Majasilimali' ndio kidude gani dogo?

Hivi wewe unafahamu au umefanya biashara gani? Wewe usiejua hata kuandika neno 'mjasiriamali' utajua umuhimu wa uandishi wa 'mpango wako wa 'biashara'.

Uliza usaidiwe sio kunyaa hapa maharage mabichi.
 
Bila shaka wewe ni mmoja unaowaibia watu kwa kuwauzia business plan😛😛😀..
Achana na vi BP.. Anza biashara, Utapeleka BP (business plan) yako inayoonyesha faidaa kubwaa bank/saccos ili upate mkopo,NAKUAMBIA UTAUZA KANYUMBA KAKO KAMATOPE .
 
Hapa nimejua sasa tatizo lako sio uandishi tu kumbe ufahamu/uelewa na Elimu yako ni ndogo sana.

Ushauri wa bure..bado nchi hii ina ardhi kubwa sana..nenda ukalime vitunguu swaumu.
 
Huenda hata jiwe ameliona hili ndio Maana akanunua midege Halafu business plan itafuta!
Matokeo yake lile dude kubwa halieleweki hata linafanya safari za wapi.....
Lilipeleka nyama ya mbuzi Uarabuni mara moja tu, likarudi linanuka lime-park hapo airport limajaa nzi!! Nikitaka kushangaa eti mataahira yaweze biashara?
 
Lilipeleka nyama ya mbuzi Uarabuni mara moja tu, likarudi linanuka lime-park hapo airport limajaa nzi!! Nikitaka kushangaa eti mataahira yaweze biashara?
Walisema ndo hilo litakua linaleta watalii!
Hivi kuna mtalii anapanga kuja kula bata halafu upande dude ambalo linapaki nyama ya mbuzi [emoji23] [emoji23]
 
Inavyoonekana hauna uelewa wowote kuhusu business plan zaidi sana umelisikia hili neno kwa wazee wa fursa.
Jaribu kujua key points zinazozingatiwa kwenye uandishi wa business plan. Wewe unadhani business plan ni kutaka kujua tu faida ya biashara
 
Kumekuwa na mafundisho mengi yanayosema ni vizuri kuandika busines plan kabla ya kuanza biashara/mradi,Lakin ukifuatilia kwa undani hakuna business plan hata moja ambayo huwa inaonesha kipindi cha hasara,Na ukifuatilia biashara nyingi hufa ndani ya mwaka wa kwanza,Na wakati huo mtu ana business plan mkononi inayoonyesha angepata faida kubwa saaaana,Nakushauri anza biashara yako hata bila ya business plan,Biashara ni vitendo sio faida ya kwenye makaratasi.Uliza wafanyabiasbara waliofanikiwa Kama walianza kwa kuandika business plan.. ANZA LEO BIASHARA,USINGOJE KESHO.
Business plan au kwa lugha ya kiswahili Mchanganuo wa biashara, kwa uelewa wangu una kazi zifuatazo.

1. Kumuongoza mtu na kumpa mchanganuo wa biashara anayotaka kuifanya.

Mfano unataka kuanzisha biashara ya kukamua mafuta ya alizeti huezi ukarupuka na kusema 10mil inatosha, lazima ukae ufanye tafiti kidogo, na hapa sio una assume prices, lazima uweke price zilizo realistic, mfano:
-je mashine za kukamua alizeti ni bei gani
-mashine inakula umeme kiasi gani
-chupa unazotumia kupack mafuta yako iwe 1ltr, 3ltr, 5ltr ni shingapi
- labels nazo bei gani
-je gunia la alizeti ni how much(kipindi cha on season bei iko chini/off season bei iko juu)
-mafuta utauza bei gani
-mashudu utauza bei gani
Hizi ni factors chache tu sio lazima kuichambua hii biashara in deep

2.kazi nyingine ya business plan inamsaidia mtu apewe mkopo(loan), kma wewe ni mfanya biashara na unataka uchukue loan kubwa ya ku grow au ku expand lazima business plan ihusike, hyo business plan itaandikwa kwa kutokana mtiririko wa financial records zako, toka uanze biashara, kma una previous loans umewahi ku clear vizuri au kudefault n.k, hii business plan ndo itakukingia wewe kifua uweze pata mkopo bank wa kutanua biashara yako. Washanya biashara wakubwa wengi wakifika stage ya ku expand their businesses lazima watumie business plans, kuna mashirika mengi wanaandika business plans na kuwasaidia watu wapate mkopo.

3. Business plan inamsaidia mfanya biashara aweze kupata wawekezaji(investors), bila business plan, huwezi kumshawishi mwekezaji aingize pesa kwenye biashara yako, lazima umpe business plan, una pitch(present) business plan mbele yake, au pannel akiwa convinced anawekeza pesa in ur venture

4. Business plan, inatumika kumsaidia mtu apate grants (ruzuku), kuna organization nyingi tu zinatoa grant funding, but lazima uwe na mchanganuo wa biashara.

Naongea with experience, kma entrepreneur, bcz nishapitia process ya kutafuta loan, nishajaribu kutafta investors, na pia nishawai kuandika kuomba grants na nikapata grant funding three times.

Lakini kama unafanya a normal business sio lazima uingie deep kuandika professional business plan, fanya tafiti, zijue gharama zote (costs) jua mauzo yako (sales), then chukua sales minus costs upate faida (profit) haina haja kuandika professional business plan, dont complicate.

Mwisho wa siku uwe na business plan au usiwe nayo haina maana kwamba, huwezi pata loss.

Japo kuna kipingele kwenye business plan inaitwa SWOT analysis (Strengths, Weakness, Opportunities, Threats) kwenye Weakness and Threats hapo ndo unaelezea possible conditions zinazoweza kukuletea hasara.

kuna unforseen events nyingi zinaweza kukuletea hasara, theft, kutapeliwa,mashine breakdowns, gari kupata ajali wakati una safirisha na products kuharibika n.k

Note: Huo ndo uelewa wangu, siongei kama consultant kwamba nimejaribu kujitangazia indirectly nipate watu niwaandikie business plans, hua nikiandika B.P hua i do it for my own use.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wapinga mpango wa biashara wengi kimsingi wanachopinga siyo mpango wa biashara bali wao wana bifu na kitendo cha kuandika mpango katika makaratasi, kwanini nasema hivyo? Duniani kote hakuna biashara yeyote ile iwe kubwa au ndogo, iwe ni biashara itakayokufa baada ya miezi sita au iwe ni biashara itakayodumu kwa karne moja isiyokuwa na mpango. Mpango maana yake ni nini? mpango wa biashara ni jumla ya mambo yote mjasiriamali anayofikiria kuhusiana na biashara yake anayotarajia kuifanya au hata ambayo tayari ameshaanza kuifanya.

Ninachotaka kieleweke hapa ni kwamba mpango wa biashara siyo lazima uandikwe kwenye karatasi ndipo uitwe mpango wa biashara hapana, Unapokaa na kuanza kufikiria jinsi utakavyofanya biashara yako tayari unafanya kitendo cha kupanga penda usipende. Biashara huanzia akilini mwa mtu pale anapowaza atapata vipi mtaji, atafanyia biashara eneo gani, ni nani atasimamia biashara, atanunua wapi malighafi, atajitangaza vipi, atapata faida au hasara nk. Sasa unapotudanganya kuwa mpango wa biashara ni kupeteza muda hebu tuambie wewe biashara yako unafanya vipi? unakurupuka tu kama unakwenda kuzima moto au unafanyaje?

Unapoona mtu aliyefanikiwa katika biashara na hakuwahi hata siku moja kuandika mpango wa biashara, haimaanishi kuwa hakutengeneza mpango wa biashara yake, alipanga lakini kila alichopanga alikihifadhi kichwani kwake badala ya kuandika katika karatasi kama unavyopinga. Vilevile mpango wa biashara wowote ule uwe ni wa kwenye karatasi au wa kichwani kama unaopendekeza wewe hauwezi kukupa gerentii ya mafanikio kwa asilimia 100% ndio maana hata mabenki yenyewe huwa hata siku moja hayatumii kigezo cha Mpango wa biashara kumkopesha mtu pesa huangalia zaidi vigezo vingine hasa dhamana nk. Kwa ujumla mpango wa biashara ni nyenzo ya kumsaidia mjasiriamali kuweza kuifanya biashara yake kwa ufanisi zaidi na hivyo kuzidisha uwezekano wa kufanikiwa.

Kwahiyo maoni yangu ni kuwa Kusema mpango wa biashara ni kupoteza muda tunadanganyana mchana kweupe, labda uniambie kwamba kuandika mpango wa biashara katika makaratasi kitaalamu ni jambo gumu linalogharimu muda mwingi tofauti na kupanga kichwani kama watu wengi tulivyozoea.
 
Jamani poleni sana naombeni msimlaumu mtoa mada Maana Nina uhakika asilimia 100
Hajui biashara ni nini wala haelewi biashara huwa inakuwaje
sasa kama hajui Biashara ni nini unadhani ataweza kujua nini maana ya na umuhimu wa andiko la biashara?
Msipoteze mda naona ana matatizo yake aiseee
 
Back
Top Bottom