Kuandika business plan ni kupoteza muda

Biznes plan starts with idea, idea yako na mikakati yakutaka kufanya biashara flani ndo biznec plan yenyewe

Nani ananifahamu?
 
Hata mbuyu ulianza kama mchicha,ila mchicha haujawai kuwa mbuyu,..Endelea KUHISI.. Alafu Dec tulete bank statement zetu hapa.. za wewe Muandika B.plan, Nasisi Tunaosema kuandika B.plan ni UZWAZWA
Sawa.
 
Hapana, hakuna ukweli kwenye hili.

Labda ungesema hivi "Business plan sio muharobaini wa matatizo yote yanayoikumba biashara...." hapo ningekuelewa vizuri mkuu.

Ni wazi kwamba, yapo mambo mengi sana nje ya business plan. Ambayo ni lazima mfanyabiashara ayafahamu, ili aweze kutetea pumzi ya biashara yake. Unless lazima biashara idecline in a short period of operations.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Upo correct mkuu.

Big up

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Samahani mkuu, unajua wewe ni mjinga? Samahani mkuu, unajua kuwa wewe ni ndezi?
 
Nimekuwa na deal na hizi issues za BP kwa zaidi ya miaka 12
Ilitokea wakati fulani kwenye laptop yangu hukosi BP 200 au 300

1. Kwa kawaida bp inatakiwa iandikwe na mfanyabiashara mwenyewe kwa lugha nyepesi anayoijua yeye. Atoe yote ya moyoni kuhusu jinsi atavyoendesha hiyo biashara. Hata kama ataandikiwa lazima asailiwe kwa undani ili kujua dhamiri na mikakati yake kibiashara. Lakini mambo yapo kinyume mtu anaenda kwa mtaalamu anamwambia nataka kufanya biashara fulani niandalie bp, mtaalamu anafanya copy and paste anampa mfanyabiashara kwa ajili ya utekelezaji
BP au wazo la biashara limefikiriwa na mtu mwingine na aliyeliandika ni mwingine hapo ndipo tatizo linapoanza

2. Kuanda BP na kuifuatisha kiutekelezaji kama ilivyoandikwa ni vitu viwili tofauti
Wengi huandaa BP kama hitajio toka mamlaka flani lakini sio kwa ajili ya matumizi kama dira ya biashara hivyo kwenye utekelezaji wa majukumu ya kibiashara watendaji wanaweza wakakaa hata miezi 6 hawajaipitia BP kujua mwenendo wa biashara unalingana na malengo

3. BP inategemea na ukubwa wa biashara
Mtu mwenye Genge mchanganuo wa kutasa 1 au 2 unatosha
Mtu mwenye duka kariakoo la medium size BP ya kurasa 10 -20 zinatosha
Mtu mwenye kiwanda pugu road kina wafanyakazi let's say 300 hii inahitaji very professional approach

"Failure to plan, is a plan to fail"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nashangaa watu wanaobeza Bplan.
Hakika hii ni shida kwa watanzania. Anyway ni uelewa wake tu..na uvivu wa kudadavua mambo..au hajui bplan inavyoandikwa ...nijuavyo bplan haiachi aspect yoyote for the sake of the business development.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
For the sake of business development not for the sake of starting a business na si kwamba business plan inaandaliwa pale tu unapoanza business but ni continuously as business development is
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…