Kuandika business plan ni kupoteza muda

Kuandika business plan ni kupoteza muda

Biznes plan starts with idea, idea yako na mikakati yakutaka kufanya biashara flani ndo biznec plan yenyewe

Nani ananifahamu?
 
Hata mbuyu ulianza kama mchicha,ila mchicha haujawai kuwa mbuyu,..Endelea KUHISI.. Alafu Dec tulete bank statement zetu hapa.. za wewe Muandika B.plan, Nasisi Tunaosema kuandika B.plan ni UZWAZWA
Sawa.
 
Hapana, hakuna ukweli kwenye hili.

Labda ungesema hivi "Business plan sio muharobaini wa matatizo yote yanayoikumba biashara...." hapo ningekuelewa vizuri mkuu.

Ni wazi kwamba, yapo mambo mengi sana nje ya business plan. Ambayo ni lazima mfanyabiashara ayafahamu, ili aweze kutetea pumzi ya biashara yake. Unless lazima biashara idecline in a short period of operations.
Kumekuwa na mafundisho mengi yanayosema ni vizuri kuandika busines plan kabla ya kuanza biashara/mradi,Lakin ukifuatilia kwa undani hakuna business plan hata moja ambayo huwa inaonesha kipindi cha hasara,Na ukifuatilia biashara nyingi hufa ndani ya mwaka wa kwanza,Na wakati huo mtu ana business plan mkononi inayoonyesha angepata faida kubwa saaaana,Nakushauri anza biashara yako hata bila ya business plan,Biashara ni vitendo sio faida ya kwenye makaratasi.Uliza wafanyabiasbara waliofanikiwa Kama walianza kwa kuandika business plan.. ANZA LEO BIASHARA,USINGOJE KESHO.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Business plan au kwa lugha ya kiswahili Mchanganuo wa biashara, kwa uelewa wangu una kazi zifuatazo.

1. Kumuongoza mtu na kumpa mchanganuo wa biashara anayotaka kuifanya.

Mfano unataka kuanzisha biashara ya kukamua mafuta ya alizeti huezi ukarupuka na kusema 10mil inatosha, lazima ukae ufanye tafiti kidogo, na hapa sio una assume prices, lazima uweke price zilizo realistic, mfano:
-je mashine za kukamua alizeti ni bei gani
-mashine inakula umeme kiasi gani
-chupa unazotumia kupack mafuta yako iwe 1ltr, 3ltr, 5ltr ni shingapi
- labels nazo bei gani
-je gunia la alizeti ni how much(kipindi cha on season bei iko chini/off season bei iko juu)
-mafuta utauza bei gani
-mashudu utauza bei gani
Hizi ni factors chache tu sio lazima kuichambua hii biashara in deep

2.kazi nyingine ya business plan inamsaidia mtu apewe mkopo(loan), kma wewe ni mfanya biashara na unataka uchukue loan kubwa ya ku grow au ku expand lazima business plan ihusike, hyo business plan itaandikwa kwa kutokana mtiririko wa financial records zako, toka uanze biashara, kma una previous loans umewahi ku clear vizuri au kudefault n.k, hii business plan ndo itakukingia wewe kifua uweze pata mkopo bank wa kutanua biashara yako. Washanya biashara wakubwa wengi wakifika stage ya ku expand their businesses lazima watumie business plans, kuna mashirika mengi wanaandika business plans na kuwasaidia watu wapate mkopo.

3. Business plan inamsaidia mfanya biashara aweze kupata wawekezaji(investors), bila business plan, huwezi kumshawishi mwekezaji aingize pesa kwenye biashara yako, lazima umpe business plan, una pitch(present) business plan mbele yake, au pannel akiwa convinced anawekeza pesa in ur venture

4. Business plan, inatumika kumsaidia mtu apate grants (ruzuku), kuna organization nyingi tu zinatoa grant funding, but lazima uwe na mchanganuo wa biashara.

Naongea with experience, kma entrepreneur, bcz nishapitia process ya kutafuta loan, nishajaribu kutafta investors, na pia nishawai kuandika kuomba grants na nikapata grant funding three times.

Lakini kama unafanya a normal business sio lazima uingie deep kuandika professional business plan, fanya tafiti, zijue gharama zote (costs) jua mauzo yako (sales), then chukua sales minus costs upate faida (profit) haina haja kuandika professional business plan, dont complicate.

Mwisho wa siku uwe na business plan au usiwe nayo haina maana kwamba, huwezi pata loss.

Japo kuna kipingele kwenye business plan inaitwa SWOT analysis (Strengths, Weakness, Opportunities, Threats) kwenye Weakness and Threats hapo ndo unaelezea possible conditions zinazoweza kukuletea hasara.

kuna unforseen events nyingi zinaweza kukuletea hasara, theft, kutapeliwa,mashine breakdowns, gari kupata ajali wakati una safirisha na products kuharibika n.k

Note: Huo ndo uelewa wangu, siongei kama consultant kwamba nimejaribu kujitangazia indirectly nipate watu niwaandikie business plans, hua nikiandika B.P hua i do it for my own use.




Sent using Jamii Forums mobile app
Upo correct mkuu.

Big up

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Samahani mkuu, unajua wewe ni mjinga?
Hahaaaaaaa ndio maana kuna watu wamekuwa wakali sana humu ndani,Ni hii ndio maana maskini wameendelea kuwa maskini wakutupwa,Kwa sababu wanafundishwa kufanya vitu ambavyo haviwezi kukuza biashara zao hata kidogo.. Wenye Akili Tunaelewana haraka sana,Ila walio kalili hawawezi kuelewa kabisaaa.
Samahani mkuu, unajua kuwa wewe ni ndezi?
 
Nimekuwa na deal na hizi issues za BP kwa zaidi ya miaka 12
Ilitokea wakati fulani kwenye laptop yangu hukosi BP 200 au 300

1. Kwa kawaida bp inatakiwa iandikwe na mfanyabiashara mwenyewe kwa lugha nyepesi anayoijua yeye. Atoe yote ya moyoni kuhusu jinsi atavyoendesha hiyo biashara. Hata kama ataandikiwa lazima asailiwe kwa undani ili kujua dhamiri na mikakati yake kibiashara. Lakini mambo yapo kinyume mtu anaenda kwa mtaalamu anamwambia nataka kufanya biashara fulani niandalie bp, mtaalamu anafanya copy and paste anampa mfanyabiashara kwa ajili ya utekelezaji
BP au wazo la biashara limefikiriwa na mtu mwingine na aliyeliandika ni mwingine hapo ndipo tatizo linapoanza

2. Kuanda BP na kuifuatisha kiutekelezaji kama ilivyoandikwa ni vitu viwili tofauti
Wengi huandaa BP kama hitajio toka mamlaka flani lakini sio kwa ajili ya matumizi kama dira ya biashara hivyo kwenye utekelezaji wa majukumu ya kibiashara watendaji wanaweza wakakaa hata miezi 6 hawajaipitia BP kujua mwenendo wa biashara unalingana na malengo

3. BP inategemea na ukubwa wa biashara
Mtu mwenye Genge mchanganuo wa kutasa 1 au 2 unatosha
Mtu mwenye duka kariakoo la medium size BP ya kurasa 10 -20 zinatosha
Mtu mwenye kiwanda pugu road kina wafanyakazi let's say 300 hii inahitaji very professional approach

"Failure to plan, is a plan to fail"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nashangaa watu wanaobeza Bplan.
Hakika hii ni shida kwa watanzania. Anyway ni uelewa wake tu..na uvivu wa kudadavua mambo..au hajui bplan inavyoandikwa ...nijuavyo bplan haiachi aspect yoyote for the sake of the business development.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nashangaa watu wanaobeza Bplan.
Hakika hii ni shida kwa watanzania. Anyway ni uelewa wake tu..na uvivu wa kudadavua mambo..au hajui bplan inavyoandikwa ...nijuavyo bplan haiachi aspect yoyote for the sake of the business development.

Sent using Jamii Forums mobile app
For the sake of business development not for the sake of starting a business na si kwamba business plan inaandaliwa pale tu unapoanza business but ni continuously as business development is
 
Back
Top Bottom