Kuanguka kwa Blackberry: Somo kwa Wajasiriamali

Kuanguka kwa Blackberry: Somo kwa Wajasiriamali

bless on

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2026
Posts
1,213
Reaction score
2,938
Blackberry zilikuwa simu pendwa sana miaka ya 2000. Kila mtu aliyekuwa akimiliki simu hizo alionekana kuwa wa kishua au mtu mwenye hela.

Zilikuwa simu nzuri sana kiasi kwamba Nokia naye akaamua kuleta Nokia Asha ilimradi tu zifanane kimuonekano. Blackberry ltd ilianzishwa na marafiki wawili Mike Lazaridis na Douglas Fregin walikuwa na malengo mazuri sana lakini utoto uliwaponza.

Wakati mwingine kwenye ofisi yako ni lazima uajiri watu wenye moyo wa UANAMUME na si UVULANA hapo tunafeli wengi tu, ndiyo, Kuna watu Wana uwezo mkubwa Lakini bado Wana UVULANA mwingi sana. Sasa wamiliki wa Blackberry ikabidi waingie mkataba na jamaa mwingine aliyeitwa Jim.

Huyu jamaa alikuwa yupo vizuri sana kwenye masoko na alipoanza kazi aligundua Kuna Mambo hayako sawa kwenye kampuni.

Kampuni yoyote Ile haitakiwi kuendeshwa kirafiki, ni lazima bosi uwe mkali kwenye kila kitu. Kumbuka umewekeza pesa zako ukileta urafiki muda wote, kampuni au biashara itakushinda kwa asilia mia moja.
Sasa baadaye Jim akakutana na jamaa anayeitwa Charles huyu alipoingia kwenye kampuni ndiyo aliwaambia ili tufanikiwe, mnahitaji kuwa WANAUME hamtakiwi kuwa WAVULANA. Aliona jinsi kampuni ilivyokuwa ikiendeshwa yaani kulikuwa na ufala mwingi sana.

Ebu fikiria, Kuna Mambo makubwa yanatakiwa kufanyiwa kazi, Kuna vitu vinahitaji kuwekwa sawa, system ilikuwa Ina uwezo wa kubeba simu laki Tano tu ilibidi ibadilishwe na iwe na uwezo wa kubeba simu milioni mbili unamwambia mtu alifanyie kazi anakuambia Leo ni siku ya kuangalia muvi, hivyo sitoweza kufanya kazi hiyo ilimkera sana Charles akaona humu hamna watu, hawa watu bado hawajakua, hawajajua ni namna gani kampuni inatakiwa kuendeshwa. So wakajisahau kwenye kila kitu, Mwisho kabisa Apple wakaanza kulaunch simu Yao ya IPhone.

Hilo likawa pigo kubwa sana kwao. kwanini? Huyu Apple alikuwa anakuja na simu isiyokuwa na batani, yaani simu ya tachi, kwa mara ya kwanza Apple wanaamua kuja na simu ya tachi iliyoitwa IPhone, hakukuwa na simu ya tachi Duniani. Mike na wenzake walivyoona hivyo kwanza wakabisha wakasema huo ugunduzi ni wa kijinga kuwahi kutokea Duniani. Simu ya tachi? Yaani mtu asijisikie wakati anabonyeza batani, akaupinga sana ugunduzi huo so watu wanaoweka pesa wakamuita na kuhitaji kuona kama Kuna Kitu amekiona kutokana na ugunduzi wa Apple, Cha ajabu Mike akawaambia atakuja na simu iitwayo Blackberry bold. Yaani kila mtu alimshangaa. Unaletaje simu hiyo wakati Apple ameleta simu ya maajabu sana? Yeye akasema atashindana naye, wasiwe na hofu.

Walipoingia sokoni, IPhone ikauza sana, tena sana na sana mwisho wa siku Blackberry wakashindwa kwenda na Dunia, wakajikuta wakiangukia pua na kufeli kabisa. Blackberry waliangushwa na utoto. Waliangushwa kwakuwa hawakuwa na wabunifu. Kwenye kampuni yoyote Ile ni lazima kuwe na ubunifu. Hili limeshindikana kukurudisha juu. Unaleta Kitu gani ili urudi? Sasa hapo unatakiwa kuwa mbunifu. Blackberry hawakuwa na watu hawa. Apple waliona kabisa Blackberry Wapo juu, hatuwezi kuwatoa hapo walipo tufanyeje? Wakaamua kuleta simu isiyo na batani, yaani unapangusa tu, wakapiga pesa nyingi nayo makampuni mengine yakaiga, Samsung naye akaanza kutengeneza simu za tachi, hata Blackberry baadaye naye aliiga sana japokuwa Mike ilimuuma sana.

Kwa Leo ni hayo tu, nimezungumzia Mambo mawili acha utoto unapoanzisha kampuni pia tafuta watu wanaoweza kubuni vitu kuifanya kampuni kuwa juu zaidi.

research-in-motion-1980s.jpg
 
Back
Top Bottom