Kuanguka kwa Ufalme wa Marvel: Uandishi Uliopoteza Mwelekeo

Kuanguka kwa Ufalme wa Marvel: Uandishi Uliopoteza Mwelekeo

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,236
Reaction score
10,774
Miaka ya mwanzoni mwa 2010 ilikuwa zama za dhahabu kwa mashabiki wa filamu za Marvel Cinematic Universe (MCU). Kila filamu iliyotoka ilikuwa tukio la kusisimua. Kuanzia Iron Man (2008), The Avengers (2012), hadi Avengers: Endgame (2019).
MCDAVEN_EC039.jpg

Marvel ilijenga himaya ya hadithi zilizochanganya ubunifu, nguvu, na hisia za kibinadamu. Lakini kadiri muda ulivyopita, ule moto uliowasha mioyo ya mashabiki duniani ukaanza kufifia — na sasa, wengi wanasema “ufalme wa Marvel umeanguka.”
images (65).jpeg

Tatizo si tu uchovu wa watazamaji, bali ni mabadiliko ya mwelekeo katika uandishi wa hadithi. Filamu zilizokuwa zikitufanya tusubiri miaka kadhaa kwa muendelezo wake, sasa zinatoka kila baada ya miezi michache zikiwa na hadithi zisizo na msisimko wala uzito wa kihisia. Wengine wanasema MCU imegeuka jukwaa la majaribio ya Propaganda badala ya kubaki kuwa injini ya ubunifu.
dc9049-civilwar_master.jpg

Uhalisia huu unaonekana zaidi pale tunapowatazama wahusika waliokuwa mashujaa wa kweli sasa wakionekana dhaifu, waliopoteza mvuto. Mfano, Bruce Banner wa The Incredible Hulk (2008) — aliyechezwa na Edward Norton — alikuwa ishara ya nguvu na hasira isiyozuilika kirahisi.
Avengers_Endgame_International.jpg

Lakini Bruce Banner wa sasa, hasa katika She-Hulk, anaonekana kama kivuli chake mwenyewe, akigeuzwa mcheshi asiye na heshima ya kale. Ni kana kwamba MCU imesahau kwamba nguvu ya mhusika haipo tu kwenye misuli mikubwa, bali kwenye historia na hisia zake. Edward Norton angekuwa kwenye Endgame sijui kama Thanos angepata nafasi ya kupumua.
sz5d2s3mz8i11.jpg

Hali imezidi kuwa mbaya kwa filamu kama The Marvels, Madame Web, na Ironheart, ambazo zimekosolewa kwa kujaribu kulazimisha ajenda ya “wanawake wenye nguvu kuliko wote” bila msingi wa kimaudhui.
edward-norton-marvel-incredible-hulk.jpg

Watazamaji wanataka wahusika wenye mizizi, si propaganda. Ni kweli, sinema inapaswa kuonyesha usawa wa kijinsia, lakini si kwa kumdhalilisha mhusika wa kiume au kubadili kabisa kanuni zilizojenga uhalisia wa dunia ya Marvel Cinematic Universe.
Black-panther-wakanda-forever-riri-williams-iron-man-tony-stark.jpg

Leo hii, Tony Stark na Steve Rogers watabakia kuwa watu wa muhimu ndani ya MCU. Mtoto mdogo kama Riri Williams hawezi kufikia ubunifu wa Stark hata ¼ yake, kama ambavyo Kara Danvers hawezi kugusa kiwango cha kina cha hisia alichokileta Henry Cavill akiwa Superman. Hata kizazi kipya kinaanza kujiuliza: “Je, Marvel bado ni hadithi ya mashujaa, au ni jukwaa la kuuza Propaganda mpya kwa nguvu?”
brie-larson-teases-future-captain-marvel-appearances-but-v0-imW0GJR9AwIGl86ke83AQr38ekL0pZsbhc...jpg

Ukweli ni kwamba, Marvel inahitaji kurudi kwenye mizizi yake — hadithi nzuri, visa halisi, na mashujaa wanaotupa matumaini, si maelezo mepesi ya kisiasa. Waachane na Propaganda za majukwaa ya ABC na kuonesha kuwa nyota za zamani walikuwa wanapoteza muda.
MCDAVEN_EC039.jpg

Sasa hivi wanataka kutengeneza Nick Fury mwenye jinsia ya kike ambaye pia atakuwa Lebanese, huyo ndio atakuwa Mkurugenzi mpya wa S.H.I.E.L.D, kitu ambacho watu wa ABC wamekifurahia sana na kuona ni hatua kubwa ya kumpa nguvu mwanamke. Sasa Nick Fury mwanamke? Wapo serious kabsa?!
 

Attachments

  • images (66).jpeg
    images (66).jpeg
    33.8 KB · Views: 44
Naulizia mazishi yanafanyika wapi?, wazee wa kamati ya michango tusije kukosa kuhuzuria...
 
Hayo mabadiliko bado hayajazoeleka ila taratibu taratibu mtazoea na kuona kitu cha kawaida, pia hao superheroes wapya hawapo kwa ajili ya kizazi chenu bali kizazi kipya a.k.a Generation Alpha (akili nyingi, nguvu kidogo na ucheshi),
Kuweni wapole, utawala wa Mwanamke huu
 
Nje ya mada ndugu Damaso hizi nyuzi zako unaandika mwenyew kiongozi

Kama unaandika mwenyew big up kiongozi we fundi 👏👏👏
 
Hayo mabadiliko bado hayajazoeleka ila taratibu taratibu mtazoea na kuona kitu cha kawaida, pia hao superheroes wapya hawapo kwa ajili ya kizazi chenu bali kizazi kipya a.k.a Generation Alpha (akili nyingi, nguvu kidogo na ucheshi),
Kuweni wapole, utawala wa Mwanamke huu
Sawa Mkuu! Ndio maana Bruce Banner wa Gen Z anafall inlove kabsa 😃 😀 😄
 
Kwani hujui kuwa kila superhero ana sexual identity yake dead pool ni bisexual kwa eternals phastos ndo gay ,superman ni bisexual,x men members mule kuna gays na lesbians
Tatizo mkuu watu wanashabilia Marvel films pekee wakasome vizuri Comic books wanaelewa
 
Back
Top Bottom