Miaka ya mwanzoni mwa 2010 ilikuwa zama za dhahabu kwa mashabiki wa filamu za
Marvel Cinematic Universe (MCU). Kila filamu iliyotoka ilikuwa tukio la kusisimua. Kuanzia
Iron Man (2008),
The Avengers (2012), hadi
Avengers: Endgame (2019).
Marvel ilijenga himaya ya hadithi zilizochanganya ubunifu, nguvu, na hisia za kibinadamu. Lakini kadiri muda ulivyopita, ule moto uliowasha mioyo ya mashabiki duniani ukaanza kufifia โ na sasa, wengi wanasema โufalme wa Marvel umeanguka.โ
Tatizo si tu uchovu wa watazamaji, bali ni mabadiliko ya mwelekeo katika uandishi wa hadithi. Filamu zilizokuwa zikitufanya tusubiri miaka kadhaa kwa muendelezo wake, sasa zinatoka kila baada ya miezi michache zikiwa na hadithi zisizo na msisimko wala uzito wa kihisia. Wengine wanasema
MCU imegeuka jukwaa la majaribio ya Propaganda badala ya kubaki kuwa injini ya ubunifu.
Uhalisia huu unaonekana zaidi pale tunapowatazama wahusika waliokuwa mashujaa wa kweli sasa wakionekana dhaifu, waliopoteza mvuto. Mfano, Bruce Banner wa
The Incredible Hulk (2008) โ aliyechezwa na
Edward Norton โ alikuwa ishara ya nguvu na hasira isiyozuilika kirahisi.
Lakini
Bruce Banner wa sasa, hasa katika
She-Hulk, anaonekana kama kivuli chake mwenyewe, akigeuzwa mcheshi asiye na heshima ya kale. Ni kana kwamba
MCU imesahau kwamba nguvu ya mhusika haipo tu kwenye misuli mikubwa, bali kwenye historia na hisia zake.
Edward Norton angekuwa kwenye
Endgame sijui kama
Thanos angepata nafasi ya kupumua.
Hali imezidi kuwa mbaya kwa filamu kama
The Marvels,
Madame Web, na
Ironheart, ambazo zimekosolewa kwa kujaribu kulazimisha ajenda ya โwanawake wenye nguvu kuliko woteโ bila msingi wa kimaudhui.
Watazamaji wanataka wahusika wenye mizizi, si propaganda. Ni kweli, sinema inapaswa kuonyesha usawa wa kijinsia, lakini si kwa kumdhalilisha mhusika wa kiume au kubadili kabisa kanuni zilizojenga uhalisia wa dunia ya
Marvel Cinematic Universe.
Leo hii,
Tony Stark na Steve Rogers watabakia kuwa watu wa muhimu ndani ya
MCU. Mtoto mdogo kama
Riri Williams hawezi kufikia ubunifu wa
Stark hata ยผ yake, kama ambavyo
Kara Danvers hawezi kugusa kiwango cha kina cha hisia alichokileta
Henry Cavill akiwa
Superman. Hata kizazi kipya kinaanza kujiuliza: โJe, Marvel bado ni hadithi ya mashujaa, au ni jukwaa la kuuza Propaganda mpya kwa nguvu?โ
Ukweli ni kwamba, Marvel inahitaji kurudi kwenye mizizi yake โ hadithi nzuri, visa halisi, na mashujaa wanaotupa matumaini, si maelezo mepesi ya kisiasa. Waachane na Propaganda za majukwaa ya ABC na kuonesha kuwa nyota za zamani walikuwa wanapoteza muda.
Sasa hivi wanataka kutengeneza
Nick Fury mwenye jinsia ya kike ambaye pia atakuwa
Lebanese, huyo ndio atakuwa Mkurugenzi mpya wa
S.H.I.E.L.D, kitu ambacho watu wa ABC wamekifurahia sana na kuona ni hatua kubwa ya kumpa nguvu mwanamke. Sasa
Nick Fury mwanamke? Wapo serious kabsa?!