Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Watafute leseni
Hoja yako ina mashiko sana. Natamani wahusika walifanyie kazi suala hila. Ukiwa na gari zako mbili au tatu na una pata wageni wachache ni vigumu kuweza kulipa TALA $5,000 kwa mwaka. Ila kwa big fish kama Leopard Tours mwenye gari zaidi ya 200 na bookings nyingi kulipa amount hiyo ni rahisi. Serikali isikie kilio hiki.Mikoa ya kanda ya kaskazini hutegemea madini na utalii ktk kuwaingizia kipato, ila kwa miaka ya karibuni serikali imeonekana kuwapa kipato mbele zaidi wawekezaji wageni kulikoni wazawa na kusababisha wachimbaji wengi kuhamia kwenye sekta ya utalii ambapo tena serikali imeingilia kwa kuwabana kwa kisingizio cha kodi.
Tukiachana na misururu ya kodi anayolimbikiziwa mfanyabiasha, sioni uhalisia wa kodi ya leseni ya utalii (TALA) kwenye wamiliki wa magari yakutoa huduma hiyo ilihali kuna mamlaka ya usafiri (SUMATRA) ambayo huwapatia kibali cha kufanya shughuli hilyo, hifadhi zimezuia magari hayo kuingia huko, sasa hiyo pesa iliyolipwa kwa Sumatra kwaajili ya utalii siyo hasara kwa mjasiriamali mzawa?
Ukiwa na stika ya Sumatra imeandikwa for tours only, hiyo tours ukaifanyie wapi?
Kama ni swala la kuingiza mapato, kwanini TALA isilipwe kwa kila gari angalau $100 ~ Tsh 218,000/-, kwa mwenye gari 200 tutapata $20,000/- na Tsh 50,000,000/- ya Sumatra, ambapo kwa sasa kwa mwekezaji mkubwa tunapoteza $18,000/- mbali na magari moja moja ya wawekezaji wadogo,,
Hebu aliyeko karibu na mamlaka awasaidie wajasiriamali wa Arusha kwani gari la safari ni gharama sana kulinunua na kuliendesha na ukisema wasiwepo ni vigumu hayo makampuni kumudu mahitaji ya soko.
Hebu tusaidiane kwa hilo.