Elections 2010 KUANGUSHWA: Jinsi Samwel Sitta alivyotoswa kwenye Uspika


Waache watakula joto ya jiwe
 
Mimi nashangaa sana watu wanaowafungamanisha mafisadi na dini !!!!!!, hivi mafisadi wana dini
Kama Chenge utasema Mkristo kweli yule naawambia hana dini
Kam Rostam , hawezi kuwa na dini kwa maana uislam haurusu wizi kama anaofanya yeye
Kam Lowasa , ana DINI gani , kwanza kuna tetesi naye anatoka sana nje ya ndoa kuna tetesi anagonga yule muuimbaji wa gospal C shushu
kama Makamba , chakaza ile mbaya wa wanawake , huyu hana dini

Mimi nawauliza wale wanaozungumzia Dini katika masuala ya siasa
Ni katiba ya chama gani inanukuu vitabu vya dini ?

HII ITAKUWA KIKWETE TIMU INAYONDELEZA PROPAGANDA ZA UNDINI

MLAAAAAAAAAAANIWE WOTE WENYE TABIA HIYO
 

Kwa orodha hiyo, kila mtanzania hatashangaa kwa nini six amedondoka.
 

Uchambuzi wako nimeupenda na naunga mkono kwa asilimia 200. Ubarikiwe sana mpendwa wa Mungu.
 
Anavuna alichopanda. Ukipanda mchicha huwezi vuna bangi. Ukipanda Nyanya huwezi vuna pilipili.
Tulimshauri sana hakusikia. Wacha apate.

Mara nyingi mtu ukiwa ndumila kuwili basi mwisho wako unakuwa kama yalivyompata Sitta!!Alitaka kuwafurahisha mafisadi kwa kuinyonga hoja ya Richmond; alikwisha waumiza na papo hapo akawa anawahurumia na sasa wao wamepata nafasi hawamuhurumii bali wanamsulubu moja kwa moja bila huruma!! Huwezi kuuwawa kwa kisu kama umeua kwa upanga!!
 

ahahah ahahah ahahaha.... sendeka nae ni jasiri? hakuna kitu kama hicho ndani ya hicho chama. wewe subiri wote hao akina sendeka,mwakyembe,manyanya,kilango na wote wanaojiita wapambanaji wa ufisadi watakutana na panga la chama chao.ushauri pekee kwao,kama wao kweli ni wapinga ufisadi,ondokeni ccm! ama sivyo hivi karibuni yatawakuta yaliyomkuta malecela,shelukindo,selelii na sasa sam6.
 
Miongoni wa masuala ya kisiasa yaliyotokea hapa nchini na kusononesha wananchi wengi na hata viongozi wa mataifa mbalimbali yanayofuatilia siasa za Tanzania, ni kuondolewa kwa Mzee Sitta kwenye kinyang'anyilo cha kiti cha uspika. Kila mtanzania mzalendo anatambua fika kuwa Mzee Sitta alikuwa anawindwa na mafisadi tangu kuanza kwa Bunge lililopita. Wengi wanazungumzia suala la Richmond kama limechangia kwa kiasi kikubwa kuondolewa kwa Mzee Sitta lakini kwa watu makini wanatambua kuwa hata Richmond isingekuwepo, Mzee Sitta angeondolewa tu kutokana na uhuru mpana aliokuwa ameutoa kwa wabunge kuchangia mawazo yao bungeni bila woga. Hilo lilikuwa ni badiliko kubwa sana kwa takriban miaka 20 iliyopita tangu uongozi wa Mzee Mwinyi na Mzee Mkapa. Mzee Sitta amejizolea sifa kubwa ya kutukuka kwa uongozi wake mahiri bungeni. Hata kama wakati fulani nae alikuwa akisukumwa na maslahi ya chama, lakini kwa ujumla, watanzania tumeshuhudia kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu, waziri mkuu na mawaziri wengine wakiadabishwa kwa kulazimishwa kujiuzulu kutokana na makosa ya kiutendaji.

Kutokana na utendaji huo uliotukuka, ninamshauri Mzee Sitta akatae katakata uteuzi wa kinafiki wa aina yoyote serikalini au kwenye chama chake cha ccm. Kwa kufanya hivyo, atakuwa amelinda heshima yake mbele ya wananchi. Nina hakika kabisa kuwa wabaya wake wamemuandalia 'vyeo uchwara' ambavyo kupitia hivyo, Mzee Sitta atajikaanga kwa mafuta yake na kufuta rekodi yake mioyoni mwa watanzania.
 
Baeleze ba elewe bob sam!
 


Angelikuwa ndiyo mimi ningehama chama.
 
Hii ni baada ya kamati kumuelewesha akae pembeni na asubili kiti kingine atakachateuliwa
 
Kama aliponea tundu la sindano kutimuliwa CCM na uspika ndio wamemchinjia baharini, unadhani atapewa chochote?. Hapewi chochote, completelly nill ila atabaki kuwa mtumishi wa wananchi wake wa Urambo.
 
Hapana, kuhamaChama sio suluhisho ila atulie alinde heshima yakekwaumma kwakutojiingiza kwenye uteuzi wowote maana siwameona haifai iko siku umma utasema anafaa.
 
Angelikuwa ndiyo mimi ningehama chama.

Laiti Sita angeyajua haya tangu awali angeshahama chama ila alikuwa na matumaini kuwa angerudishwa kwenye nafasi yake ya uspika.
Na sasa baada ya kutoswa ana matumaini ya kuukwaa angalau unaaibu waziri.
Endapo atatoshwa na nafasi hiyo, hapo ndipo wazo la kuhama chama ndipo litakapokuja kwani 2015 hata nafasi ya kugombea ubunge atatoswa.
 
Tena kabisa Mh Sitta usikubali cheo chochote iyo itakuwa danganya toto,kaa hapo bungeni tena back bench halafu uwe unaiwashia moto serikali kwa sana tu (jana nilikuwa nimekaa sehemu nikasikia kuwa mh. sitta tokea juzi anapigiwa simu na jk hapokei, kama ni kweli safiiii!! tena i-delete no yake kabisa!!!)
 
Hivi wewe Malaria Sugu unafurahia Sita kutoswa au?
Hebu nipe maoni yako juu ya jambo hili.
 

...MKUU, UMENENA! As said, you cannot eat your cake and have it!
 
[Anavuna alichopanda. Ukipanda mchicha huwezi vuna bangi. Ukipanda Nyanya huwezi vuna pilipili.
Tulimshauri sana hakusikia. Wacha apate.)

Hakika hukumu hii hakuonewa kamwe ogopeni vigeugeu
ukiamua kuwa moto kuwa moto na baridi kuwa baridi vuguvugu always ni wanafiki tu wachumia tumbo:A S-baby:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…