Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
BINAMU HIMSELF: TUKIO LA MAUAJI SALENDER BRIDGE JANA
Tukio la mauaji Salender Bridge jana
Kumekuwa na hisia na hukumu nyingi kuhusiana na tukio la jana lililopoteza maisha ya watu watano. Ugaidi, kisasi, chuki vimetajwa kama sababu na baadhi ya wengi, Ilimradi kila mmoja amesema anavyodhani ni sawa.
Kiujumla ni tukio baya, linaloleta picha mbaya ndani na nje ya nchi. Ni tukio ambalo tukiruhusu kila mmoja atoe hukumu yake, aongee apendavyo balaa lake liko mbeleni maana watu wataikataa ripoti ya kipelelezi ambayo Mh Rais ameagiza itolewe haraka.
Wakati palishakuwa na hali ya utulivu Dar es Salaam baada ya mabadiliko yaliyofanywa ktk jeshi la Polisi jambo hili lisipofuatiliwa kwa umakini litaleta doa. Je ni kweli polisi walitaka kumdhulumu dhahabu zake? Je ni suala la ugaidi? Je ni tatizo la kiakili? Yote tuyasubirie yatolewe na wahusika.
Kuanza kuhusisha siasa (kumtengenezea Muuaji kadi ya Chadema ama kuonyesha UCCM wake ni ushamba). Maana hakuna chama kinachoweza kuhimiza mauaji ya watu wake. Kama mtu ni MUOVU ashughulikiwe kama YEYE BINAFSI na sio taasisi, dini ama kabila lake.
Ni imani ya kila mmoja kwamba wenye jukumu la kuitoa ripoti ya tukio hilo WATAISIMAMIA KWELI kwa faida ya nchi. Kama ni ugaidi hatua stahiki za kuufuatilia mtandao huo zichukiwe na kama kuna huo uchafu wa dhuluma nao usemwe maana kuna wasio waaminifu.
Nirudie kulipongeza Jeshi la Polisi kwa namna walivyokabiliana na tukio hilo, lakini niupongeze ushujaa binafsi wa askari walioonekana katika video clips namna walivyokabiliana na Bwana Hamza.
Tuombe pia wakati huu wa uchunguzi ukiendelea familia ya kina Hamza isielemezewe uovu wakati wa kutafuta kiini cha jambo hili. Wabaki kuwa wasaidizi muhimu kwa dola na sio watuhumiwa muhimu.
BinamuHimself!