Kuanza kujulikana kwa watekaji na wauaji. Je, taifa limeanza kupumua na haya majanga?

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Utekwaji wa kukumbukwa zaidi ni wa Dr. Steven Ulimboka aliyeongoza mgomo wa madaktari enzi za Kikwete....
Alitekwa kisayansi kwa kujipeleka mwenyewe mdomoni mwa mwamba.

Wakamchukua wakampeleka huko kwao wakamtesa vilivyo kisha wakaenda kumtupa Mabwepande
Mapori ya Mwabwepande ndio yalikuwa yanaogopeka sana kipindi Hicho kwa watu kwenda lutupwa
Kabla ya hapo ilikuwa bonde la jangwani kuelekea Magomeni

Ya utekwaji wa Dr. Ulimboka ukafuatiwa na matukio ya watu kuvamiwa wanaporudi makwao hasa wanapoongia getini.

Matukio ya kukumbukwa zaidi ni waandishi Absalom Kibanda na Said Kubenea.. Huyu alivamiwa akiwa ofisini kwake akamwagiwa kimiminika kibaya usoni.. Kibanda alipokea kipondo heavy.

Matukio ya kuvamiwa ndani ya ua na kuuwawa ni yule mwanasheria simkumbuki jina.. Na Dr. Sengodo Mvungi wa NCCR ..huyu walimvamia ndani kwake na kumchanja mapanga ya kutosha mpaka wakamuua.

Baada ya hapo ndio kama kipenda kikawa kimepigwa.. Watu wakaanza kupotezwa kwa kasi sana hasa kipindi cha mwenda zake.. Fasheni mpya ikawa ni kutiwa kwenye sandarusi na kwenda lutupwa baharini.. Lakini kwa bahati mbaya bahari haikai na uchafu huutapika.

Matukio ya kuokotwa maiti kwenye fukwe za bahari yakawa mengi.. Na kwa asilimia 95 wahanga ni wapinzani na wakosoaji wa mamlaka

Mpaka kufikia hakuna mtekaji hata mmoja na pengine watesaji na wauaji ambao waliwahi kutajwa kwa uwazi na moja kwa moja kwa majina yao.. Ukiachilia tukio la kushabuliwa Lissu.

Kuna kipindi taifa lilipumua kidogo kukawa na amani ya mpito.. Taharuki ikapoa.. Lakini ghafla kuanzia mwaka jana mambo yakaanza kubadilika kwa haraka.. Utekaji utesaji kupotea kwa watu na mauaji vikatamalaki tena..
Kufika mwaka huu hali ikawa mbaya zaidi na kwenye kilele cha haya matukio kuna watu wakaanza kutwaja moja kwa moja kwa majina na vyeo vyao.. Kwa matukio ya nyuma na ya sasa!

Kuanzia hapo kuna kautilivu na kaukimya kametawala.. Lakini bado kiza ni kinene

Kushutumiwa na kutuhumiwa kwa makampuni za simu kutoa taarifa za faragha za wateja kwa mamlaka kumeleta taharuki mpya na faraja kwa kiasi chake

Je, watekaji watesaji na wauaji wataendelea kuaniakwa kwa uthubutu uleule? Je huu ndio mwisho wao?
Tuupe muda wakati.
 
Hapa JF wako 6, nakamilisha mchakato wa kuwaanika, hatuna sababu yoyote ya kuficha hawa wauaji
 
IMG-20240926-WA0033.jpg
 
Serikali yetu tukufu( kama inavyoitwa na wanufaike) katika hili imetushangaza na kutuacha vinywa wazi sisi ambao ndio walezi wake.......

Ukimya wa serikali, kejeli kutoka kwenye vinywa vya wenye mamlaka ya kutulinda, pamoja na ucheleweshwaji na ushughulikiwaji wa ripoti za matukio ya watu kutekwa, kuuwawa na kudhuliwa vinazidi kuzaa maswali na kuzijaza hofu nyoyo zetu dhidi ya serikali yetu tukufu.......

Mioyo yetu na fikra zetu vinajitahidi kupambana na mawazo na hisia za kuwa pengine serikali yetu tukufu inahusika na hila hii dhidi yetu lakini mtiririko wa matukio haya na aina ya watu wanaofikwa na masahibu haya na ushughulikiwaji wa hali yenyewe vinatufanya tuzidi kuamini hisia zetu.....

Wapo wahanga waliowataja watu ambao Inasemakana wanahusika moja kwa moja kwenye mambo haya machafu dhidi ya binadamu wenzetu na wengine wanatumikia majeshi yetu lakini hatujaona hatua zikichukuliwa dhidi ya watajwa.......

Tuhuma nzito zenye kuogofya kwenye jamii zinaonekana kama umbea na majungu ya mitaani mbele ya macho na masikio ya serikali yetu tukufu........

Hatari iliyopo ni kwamba kukithiri kwa matukio kama haya au yanayofanana na hayo kutashusha imani yetu kwa serikali yetu tukufu lakini pia itapelekea wananchi au wanyonge waanze kujitetea na kujichukulia sheria mkononi........

TUNAIOMBA SERIKALI YETU TUKUFU KUWA BADO MUDA UPO WA KUREKEBISHA........
 
Utapata jibu? Ah wapi🙌🏾

Hiyo miili ingefanyiwa DNA. Naamimi hawa hawakuwa Watanzania.

Haijalishi....

Mambo mengi yalitungwa tungwa tu
Wauaji ni wauaji tuu, ni kama wabaguzi na wakabila tuu, wakimaliza upande huu wanarudia hata familia zao, hauko salama kama unavyofikiria
 
Back
Top Bottom