Kuanza kujulikana kwa watekaji na wauaji. Je, taifa limeanza kupumua na haya majanga?

Kuanza kujulikana kwa watekaji na wauaji. Je, taifa limeanza kupumua na haya majanga?

Kule uchaggani mchawi akikaribia kufa huwa ana-ere. Kuere maana yake ni kutaja watu aliowaloga, kuwaua na kuwafanyia ubaya kwa kukanusha. Yani anasema mimi sikumuua Mrema, sio mimi nilimloga Shirima. Mkisikia watu wanasema mimi ndo nilimuua Kisanga waambieni sio mimi. Wabaya wananisingizia"

Ukimuona ndugu yako amefikia hatua hiyo ujue ana-ere. Unachotakiwa kufanya ni kumuita Mchungaji/Padri haraka, aje kumuongoza sala ya toba maana hiyo ndio nafasi ya mwisho amepewa ya kutubia dhambi zake. Anakaribia kukata roho huyo. Subhanallah.!
 
Hao inatakiwa uwataje kwa ushahidi. Ni vyema utengeneze ID nyingine na uwalipue kwani ukiitumia hii, mods watakupiga ban.
Nayajua yote hayo, Lakini Sheria ya JF ni lazima ifanyiwe marekebisho, inatubana, kwanini tuwalinde Wauaji?
 
Hakuna linaloshindikana kwenye kijiji chenye Wazee na Taifa bora lenye msingi wa kikatiba na utawala wa sheria huthamini Utawala Bora na usalama wa Raia....Tuzungumze pamoja na kutafuta suluhisho endelevu la pamoja. Ni tarehe 5 Oktoba pale Ubungo plaza....Tusipozungumza kama wenye hekima tutaangamia kama wapumbavu
20241002_091214.jpg
 
Hakuna linaloshindikana kwenye kijiji chenye Wazee na Taifa bora lenye msingi wa kikatiba na utawala wa sheria huthamini Utawala Bora na usalama wa Raia....Tuzungumze pamoja na kutafuta suluhisho endelevu la pamoja. Ni tarehe 5 Oktoba pale Ubungo plaza....Tusipozungumza kama wenye hekima tutaangamia kama wapumbavuView attachment 3112827
 
1.Unamteka mtoto wa kike kwa mtutu wa bunduki

2.Kundi la wanaume saba wakatili mnakubali kwenda kumteka, kumdalilisha, kumnyanyasa na kutweza utu wa mwanamke kwa ujira wa fedha?

3.Mnafunga kitambaa usoni mwanamke kisha mnamtoa nyumbani kwake Kibiti mnamsafirisha hadi mapori ya Kisarawe kwenda kumnyanyasa na kumfanyia ukatili

4.Mnajitambulisha kuwa ni maafisa wa chombo cha dola kisha mnatumia gari la kodi za wananchi, pingu na bunduki zilizonunuliwa kwa kodi zetu.

5.Mnachana nguo za mwanamke aliyefunzwa kujistiri kwa dini yake safi ya kiislamu tangu utotoni na kumuacha utupu.

6.Mwanamke mmoja anashirikiana na wanaume saba kumshambulia na kumdhalilisha mwanamke mwenzake kwa ujira wa pesa tu

7.Mmemaliza kumfanyia ukatili Mwanamke mnamtekeleza maporini mnaondoka na kujiona wajanja... mnajiona mmeyapatia maisha kweli.

8.Nawakumbusha yupo Mungu juu anayeona kila kitu muda wote na sehemu zote. Ipo siku kabla hamjazikwa na kufukiwa na udongo huu mnaotumia kumwaga damu, mtakumbushwa kila tukio moja mlilotenda.

9.Nawaonea huruma ninyi watekaji na wauaji, kwa kuwa najua hamjui watu makatili kama ninyi mwisho wenu unakuwaga vipi.

10.Lakini niwahakikishie akili za upinzani na harakati hazizimwi kwa mtutu wa bunduki na kufuli la Jela tulifikiri mmejifunza kwa Hayati Magufuli

Hamtoweza kuua watu wote,wapo watakaobaki nyuma yetu,wao watatulipia visasi vyetu.hilo mnatakiwa kulielewa siku zote.

Hakunaga Jambo linafanywa na watu zaidi ya wawili likabakia kuwa siri.
Boni yai Twitter
20241023_051623.jpg
 
Nimesoma mahali wanasema mayele yuko hoi india
 
Back
Top Bottom