Ngaliwe
Senior Member
- Dec 30, 2015
- 164
- 374
Inasikitisha lakini haishangazi, kwamba wapo baadhi ya watu, wakiwemo Watanzania wenzetu wameanza tena kurejea tabia iliyokuwa imeanza kukoma, ya udokozi wa mali ya umma, wizi. Kwamba baadhi ya wafanyabiashara waliokuwa na mwenendo mzuri wa kulipa kodi wameanza ujanja na kulegea katika msimamo huo, na baadhi ya wawekezaji walioko kwenye majadiliano na serikali kuhusu namna nzuri ya kugawana rasilimali zetu wameanza kurudi nyuma.
Mwanamwema wa Tanzania na Afrika, Hayati John Magufuli, alipokuwa akisisitiza kwamba tuko katika vita ya kiuchumi, na kwamba ni lazima tushikamane na kuombeana na zaidi sana kumuombea yeye anayeongoza vita hivyo, si watu wengi walikuwa wakielewa maana yake hasa.
Onyo lililotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan, wakati analihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuhusu wizi ulioanza kurejea, kutaka kukengeuka kwa wafanyabiashara ambao walisharejea kwenye njia nzuri ya ulipaji kodi na dalili za kutaka kurudi nyuma na / au kuleta masharti mengine mezani kwa wawekezaji ambao wako katika meza ya mazungmzo na serikali kuhusu namna nzuri na mgawanyo wa rasilimali zetu ni tafsiri halisi ya vita hiyo ya kiuchumi.
Kwamba muda wote ni kama tunaviziana, wako baadhi ya watu, makampuni makubwa ya kimataifa na watumishi wa umma wenye tamaa ya fisi, muda wote wako mawindoni kuona ni namna gani wanaweza kupenyeza agenda zao ovu ili waweze kupata mwanya wa kujilimbikizia mali kadiri wanavyoweza kwa gharama ya watanzania.
Kwao hawa suala la kufanya biashara kwa ubia wa usawa (win - win situation), kulipa kodi bila shurti, kufanya kazi halali kwa kipato halali si sehemu ya utaratibu wa maisha yao ya kawaida, malengo yao wakati wote ni kukomba kila kitu. Ni wazi kwamba hawakufurahishwa sana na msimamo wa serikali ya wamu ya tano kuhusu usimamizi wa rasilimali za umma, kusimamia nidhamu ya utumishi serikalini na kubinya mianya ya ukwepaji kodi. Na watu hawa si wadogo hata kidogo, ni watu wazito wana nguvu za kiuchumi na ushawishi mkubwa sana kwa viongozi wengi wa Afrika na dunia.
Ndiyo maana, haikuwa bahati mbaya kwamba, mara tu baada ya kuanza kupata umaarufu duniani kuhusu namna ya utendaji kazi wake, na kuzaliwa misamiati kama Magufulification, hashtag za whatwouldmagufulido, na sifa zingine, wakubwa hawa waliona hatari ya ushawishi wa mtu anayeitwa John Pombe Magufuli, kwa maslahi yao na hatma yake. Wakaanzisha vita dhidi yake.
Mashambulizi kuanzia ndani ya nchi, kupitia wapinzani, baadhi ya wana CCM, mashirika ya yanayojiita ya haki za binadamu yote yakikosoa utawala wake, hayakuzuka tu kutoka hewani, ulikuwa ni sehemu ya mkakati wa wakubwa hawa kuona kwamba wanafunika mazuri yote anayoyawafanya kwa ajili ya Tanzania, ambayo yalianza kutoa dira na mwelekeo wa namna gani kizazi cha viongozi wa wa sasa wa Afrika kinatakiwa kuazisha na kusimamia vita vya ukombozi wa pili, ukombozi wa kiuchumi.
Kukubalika kwa staili ya uongozi wa Magufuli na ujasiri wake katika kulinda maliasili za Taifa kwa manufaa ya wananchi wake, kulimweka katika kundi ‘lisilotakiwa’ la viongozi wa Afrika. Kumchafua yeye ilikuwa ni mbinu ya wakubwa hawa kuhakikisha kwamba atakapomaliza muda wake, kusiwe na mtu ana hamu na aina yake ya utawala, ili hata viongozi wengine wanaokuja badala yake siyo tu wasione fahari kujinasabisha naye, isipokuwa waepuke kila kitu chake.
Ni katika muktadha huo, haikushangaza sana, mara tu baada ya Rais Samia kuapa kushika madaraka kama Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania, wale wote waliokuwa wapinzani wakubwa wa Magufuli, ghafla wakawa wafuasi lia lia wa rais mpya. Huu ni sehemu ya mkakati mzito sana wa wakubwa ambao wengi wa wanaodemka na mirindimo ya ngoma zake ni wahanga tu wa harakati hizo, hawajui nini asili na msingi wa kubadilika huko kwa upepo, wanaitikia tu kibwagizo cha wimbo wasiojua maudhui yake, kama bendera fuata upepo.
Mabadiliko haya ya ghafla, ni kama yalitaka kutuma ujumbe kwa Rais Samia kwamba, akitaka kuwa ‘Rais mzuri’ asiende katika njia ya mtangulizi wake. Ni katika sehemu ya mkakati huo haraka sana, katika hali isiyokuwa ya kawaida, hata kabla Taifa halijaanua matanga ya maombolezo ya Hayati Rais Magufuli, ukaanzishwa mjadala kuanza kulinganisha na kushindanisha nani bora kati ya Magufuli na Samia.
Wakati sisi tunashinda na kukesha mitandaoni kuonyeshana umwamba na ujuvi wa hoja kuhusu ama tunamuunga mkono Hayati Rais Magufuli au Rais Samia, wenye agenda yao wakaingia kazini, wanataka kurudi nyuma au labda kubadili mwelekeo wa majadiliano na serikali kuhusu mgawanyo wa rasimali zetu, wameanza dalili za kurejea kwenye kukwepa kodi, na wameanza wizi, hayo yote ni kutikisa kiberiti, kimejaa au la.
Hawafanyi hivi kwa bahati mbaya, kampeni yao dhidi ya Hayati Rais Magufuli, ililenga kuyafanya mambo yote aliyofanya kwamba ni yake binafsi,hayahusiani na Tanzania wala watanzania na kwa kuwa walikuwa wanamchafua sana ili kuwatisha watakaokuja baada yaje waone kujinasabisha naye ni kujichafua, ndiyo maana wameanza wizi huo. Wanampima Mama, waone kama kiberiti kimejaa au la.
Inatia moyo kwamba Mama, Rais Samia, ametambua hila zao, na kwamba Hayati Magufuli amekwenda peke yake, maono yake kuhusu Tanzania mpya na usimamizi wa rasilimali za umma, yamebaki na yataendelea kutekeelezwa kwa ari na ngvu ile ile.
Na kwa kuwa ni kweli kwamba, Rais Samia na Hayati Rais Magufuli ni kitu kimoja, wametekeleza wote ilani ya CCM 2015 – 2020 na walianza pamoja safari ya utekelezaji wa ilani ya mwaka 2020 – 2025, ni matumani yetu kwamba Mama ataanza na hao walioanza wizi na kumjaribu, asicheke nao.
Kwa sababu huu ni ubeberu katika ubora wake, unajua kunyinyambulisha na kujibadili kwa namna nyingi sana ili kuitika mahitaji ya wakati katika kulinda na kutetea maslahi yake, ukiachiwa uendelee hivi, hatma yetu kama Taifa itakuwa shakani.
ASANTE SAMIA