Kuanzia 2015 Tanzania itatawaliwa "kidikteta" Ukweli huu hapa

Ni zamu ya Wazanzibar na waislamu pia, hakuna wa kuligeuza hili 2025.
Unajidanganya. Huna ujualo bwana mdogo.

Hata huyo Mwinyi wako ni PAZIA tu — Yaani ni KANYABOYA kwa lugha nyingine.

Walio nyuma ya Mwinyi ndio wenye mamlaka ya kweli.

You are simply a controlled mindless zombie who is there to clap the hands to the advantage of the cabals.
 
Wewe ni mpiga ramli?? Duuh! Yote uliyotabiri yametimia!!
 
Uzi wako haukumlenga jpm, ulimlenga lowasa, kwanza ukiangalia kipindi hicho lowasa alikuwa na nguvu na ushawishi mkubwa, pia ukiangalia kutoelewana kwake na jk, ulijua hata akienda upinzani atakubalika, ni wazi ulitumia takwimu za uchaguzi wa 2010 pia ccm ilishachokwa na wananchi kutokana na utawala wa kipindi hicho kuwa na mapungufu mengi, kikwete alipata shida sana kunadi sera zake kwa wananchi kutokana na ufisadi na uongozi usioridhisha na ndio sababu uchaguzi wa 2015 jpm alijinadi yeye mwenyewe chagua magufuli, ni wazi ccm isingemteua magufuli ilikuwa ndio mwisho wake 2015, magufuli ndio mtu pekee aliyekubalika na wengi pia alikuwa na historia safi ya uwajibikaji tofauti na wagombea wengine, pia kwenye utawala wake jpm kwa kiasi kikubwa ni tofauti na ulivyotabiri maana aliwasikiliza wananchi alijua ni nini wanataka na walimkubali.
 
Duh unaona wivu au

Sent from my Infinix X658E using JamiiForums mobile app
 
Uzi wa mwaka 2012 💯💯...alafu kuna mtu anajiita paschal mayala anadai eti yeye ndio alitabiri Magufuli atakua Rais kwenye thread aliyoiandika 2014😂😂
Mkuu masare, nitake radhi!. Maudhui ya uzi huu sio nani atakuwa rais wa Tanzania 2015, bali tutatawaliwa kidikiteta 2015 bila kumtaja specifically rais wetu atakuwa nani.

Mimi bandiko langu hili Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli sio la utabiri, sio la ubashiri, sio guess work, ni info pack!, nimeambiwa na mtu from deep inside!.

Katika bandiko hili langu, nime copy kitu gani kutoka bandiko hili la Mkuu MAGAMBA MATATU?.
P
 
Jiwe hakushinda 2015 kihalali kama ambavyo hakushinda 2020.
CCM ilichokwa kitambo na imechokwa sasa na hakukuwa na wa kuiokoa na hakuna wa kuiokoa kihalali.
 

Magufuli aliwasikiliza wananchi, na wananchi walimkubali, cha ajabu ilibidi apore uchaguzi ili aendelee kukaa madarakani! Sasa kama unakubalika unanajisi uchaguzi ili iweje.
 
Jiwe hakushinda 2015 kihalali kama ambavyo hakushinda 2020.
CCM ilichokwa kitambo na imechokwa sasa na hakukuwa na wa kuiokoa na hakuna wa kuiokoa kihalali.

Kula tano, na ushahidi kuwa CCM imeendelea kuchokwa hata baada ya Magufuli kuingia madarakani, chaguzi nyingi wakati wa utawala wake zilijaa wizi mkubwa wa kura, ukiukwaji mkubwa wa sheria za chaguzi, na ndio utawala uliofanya box la kura kudharaulika rasmi.
 
Wanakuandama sana mkuu.
 
Nakufuatilia sana uko vizuri
 
We jamaa ni nabii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…