Kuanzia 2015 Tanzania itatawaliwa "kidikteta" Ukweli huu hapa

Kuanzia 2015 Tanzania itatawaliwa "kidikteta" Ukweli huu hapa

Kwa nini nimeamua kusema hivi? Kuna mambo matano (5) makuu yananilazimisha kusema kuwa:
"Tanzania itatawaliwa kidikteta"
Ni vigumu sana kwa mtu asiyeona mbali kunielewa kirahisi na pia ni rahisi sana kwa anayependa demokrasia kunibeza na kuniona kama naota.

1. Kwanza kuna uwezekano mkubwa Rais ajaye ataingia madarakani kwa utata nikimaanisha kutakuwa na mizengwe katika utoaji wa matokeo kwani hali halisi inajionesha wazi kuwa kuna mvutano mkubwa wa vyama viwili na hakuna kinachokubali kuwa kimeshindwa ki-haki.Endapo mgombea wa chama tawala akashinda basi chama kikuu cha upinzani kitatumia nguvu ya umma ili kupata sapoti wakati aliyejiona kashinda kwa haki atakimbilia ikulu na kushawishi dola kulinda ushindi wake kadri wawezavyo.Tukumbuke yaliyozikumba nchi za :LIBYA, IVORY COAST, LIBERIA, NIGERIA, ZIMBABWE, KENYA, VISIWA VYA COMORO, MISRI na TUNISIA.

2. Pili ni ahadi atakazozitoa hususani zile za kushughulikia "MAFISADI". Ili kupambana na aliyekuzidi kifedha lazima uchukue fedha zake kwa nguvu hivyo atataifisha mali za waliosemekana ni wahujumu uchumi au mafisadi. Akiwa yupo kwenye hali hiyo lazima watamwinda hivyo itamgharimu kuwa dikteta katika kupambana na mafisadi ikiwa ni pamoja na kunyonga baadhi yao ili kuweka fundisho. Pia atajikuta analipa kisasi cha mateso yote yaliyompata katika harakati za kuingia ikulu.

3.Suala zima la maendeleo haliendani na kuwapa watu uhuru wa kukaa mijini na kuendeleza masuala kama ya kupiga debe, kutembeza vitu mijini, kuuza na kula madawa ya kulevya, polisi wa barabarani kupokea rushwa, maafisa wa TRA kusamehe kodi na kutoa vibali kwa njia za panya, viongozi wa serikali kutumia ofisi zao kama kampuni zao! Yote haya yatasababisha rais ajaye awe dikteta na mkatili kwa wazembe wote wanaokwamisha matarajio yake, ikiwa ni pamoja na kuwafurutisha vijana wote mijini na kuwafukuza kazi wazembe wote.

4. Suala zima la ushawishi wa dini, endapo ataegemea dini moja basi atajikuta yupo kwenye wakati mgumu kwani atajikuta amegeuka gafla na kuwa adui wa dini nyingine hivyo kujikuta akichukua maamuzi ya kibabe ili kukabiliana na upinzani kutoka dini fulani. Suala kujiunga na dini ya mashetani au "FREEMASONS" litakuwa jambo la kawaida na watu wengi wenye kupinga serikali watatoweka na wasijulikane wapo wapi.

5.Ushawishi wa nchi za magharibi; hili nalo ni tatizo ambalo nitafanya nchi isitawalike endapo Rais ajae ataamua kufuata matwakwa ya raia wake kwenye masuala la uwekezaji, ajira, ugawaji wa ardhi, kodi, na utaifishaji wa mali za umma kama viwanda, mashamba makubwa, n.k.na endapo atawageuka wananchi na kusikiliza matakwa ya nchi za magharibi basi atajikuta amepitisha sera ya ndoa za jinsia moja, biashara haramu ya siaha, urutubishaji wa nyuklia. Hali hii itapelekea wanachi waanze kumchukia na atajikuta anatumia nguvu za dola kulazimisha wananchi wakubali sera zake.

Pia kuna mambo mengine kama kuibuka vyama vya siasa vyenye nguvu vinavyotaka kumtoa madarakani kwa nguvu na atajikuta akiwasweka rumande wapinzani wengi ambapo itachafua hali ya hewa ya nchi. Pia utata wa mgawanyiko wa wabunge maana kuna kila dalili vyama viwili vyenye ushindani kugawana sehemu kubwa ya idadi ya wabunge na hivyo kumlazimisha Rais kuwa na wakati mgumu wa kuvunja bunge zaidi ya mara moja kwenye kipindi cha miaka mitano.

Pia suala la ajira litaendelea kutesa nchi na ongezeko la wasomi itakuwa pia tatizo hivyo itamlazimu kutumia sheria kali na za kibabe ili kuendesha utawala wake.

Vyombo mbalimbali vitanyimwa uhuru wa kutoa mawazo yao hii itapelekea vyombo vya habari vya magharibi kumuulika nchi na hivyo hali kuwa mbaya zaidi.

Swali la kujiuliza, Rais ajaye atakuwa nani ?

Ni vigumu kupata jibu la moja kwa moja ingawa watu wengi wanatazamia kuona sura mojawapo kati ya hizi:
- Zito Kabwe,
- Dr. Willbrod Slaa,
- Dr. Asha Rose Migiro,
- Edward Lowassa.
- Samwel Sitta
- Prof. Ibrahim Lipumba.
- Bernad Membe, na
- John Pombe Magufuli
.

Kwanini Watanzania wengi wanategemea kati ya watu hawa mmoja wapo atakuwa Rais wa Tanzania mwaka 2015?
Jibu kubwa na la msingi ni suala zima la uwajibikaji na kujituma.

Kwanini nasema hivyo?
Ukiangalia sura zote ni watu wachapa kazi, wanajituma na wenye maamuzi magumu kwa masuala nyeti ya nchi. Ingawa kila mmoja ana mapungufu yake lakini ukweli bado unabaki pale pale wanauwezo mkubwa wa kulifikisha taifa pale Watanzania wanapotaka ikiwa watatekeleza majukumu yao ipasavyo.

Bado suala la wapinzani kuungana na kumsimamisha mgombea mmoja litakuwa ni ndoto. Kwanza utofauti wa sera na mawazo yao vinakinzana. Pia kuna suala zima la itikadi ya chama na mitazamo. Wapinzani wamejifunza mengi kutoka kwa jirani zao Kenya. Hivyo hawapo tayari kuungana na kuanza kung'ang'aniana madaraka ni bora kila mmoja ashiriki kwa nguvu zake na ashinde kwa nguvu zake.
Dah! Mkuu MAGAMBA MATATU umetisha vibaya. Yote yametimia isipokuwa tu hilo la kuvunja bunge!
 
Kamwenee
Mkuu MAGAMBA MATATU,

Nashukuru kwa maoni yako, lakini naomba nikukumbushe kuwa, haya unayoyaandika kama maono yako, yalikuwa yatokee 2010. Katika uchaguzi wa 2010, ccm walitumia kila hila kushinda ule uchaguzi, ccm waiba kura kwa mbinu mbalimbali, kuanzia urais mpaka udiwani. Kwa karama za Mungu, viongozi wa CDM walivumilia huo uchafu wote, ili damu ya mtanzania isimwagike, hata Mh. Dr. Slaa alilizungumzia hili.

Kwa hiyo, hayo maono yako sidhani kama yanaweza kutokea 2015 kwa sababu, hadi kufika huko ccm itakuwa imeshapoteza mvuto au itakuwa imeshajifia kabisa. Ila swala la CDM kuingia ikulu kwa umwagaji damu, hilo swala halipo...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo Brita anatabia ya kike kujua kila kitu na kila mtu. Utazani kaambiwa amtaje kwa jina halisi sio la kwenye mada.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu Massa, tabia ya kutaka kujua kila kitu sio tabia ya kike, hii inaitwa inquisitive, ni element muhimu kwa researchers, investigators, good lawyers na waandishi wa habari wa habari wa investigative journalism.

Tabia za kike ni kufuatilia maisha ya watu ili kutafuta umbea kwa ajili ya kuusambaza.

Kitendo cha kufananisha jina lolote la jf na mtu yoyote halisi ni kosa kubwa la kustahili ban, kwa sababu huku ni kumu expose mtu, which is not good at all kwa sababu kiukweli kabisa miongoni mwa wana jf, tuna jamaa kibao wa sehemu humu, mfano itokee umelijua jina halisi la Hutaki Unaacha, halafu ukamtaja, jee unajua ni nini kitakachompata?.

P
CC. britanicca
 
Hii sio name calling? Nadhani,kwa sheria na taratibu za JF, Mkuu britanicca unastahili ban mara moja. Umefanya jambo lisilo la kiungwana kabisa kwa kimbelembele chako.

Cc Invisible , Active
We ndo unapanga adhabu?

Kwanza kuthibitisha kwamba nastahili Ban kwa kosa gani?

Mi nimemtungia jina tu huyo kama wewe ambaye naweza kukuita Jina lolote haimaanishi ndo jina lako
 
Sikubaliani na wewe, baada ya 2015 kutakuwa na katiba mpaya ambayo haitampa raisi madaraka makubwa na kutakuwa na utawala wa sheria, pia kuwawajibisha wavivu siyo udikteta, swala la mashoga raisi hawezi kuwa na maamuzi nalo kwani litakuwa chini ya mahakama ya katiba kuamua, kumbuka wakati huo mahakama zitakuwa huru, tofauti na sasa.

Kuhusu kupola mali za mafisadi huenda hasifanye hivyo, badala yake akawasamehe, akaunda tume ya uwazi na ukweli ambayo itawahoji watakaohisiwa walikuwa mafisadi ili wasaidie kuzuia ufisadi usitokee kirahisi.

Rais ajae atakuwa na kazi ngumu sana, kwani kila idara ya nchi imeoza na hawezi kuwa na nguvu sana kisheria kama alivyo raisi wa sasa.
Upo mkuu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Massa, tabia ya kutaka kujua kila kitu sio tabia ya kike, hii inaitwa inquisitive, ni element muhimu kwa researchers, investigators, good lawyers na waandishi wa habari wa habari wa investigative journalism.

Tabia za kike ni kufuatilia maisha ya watu ili kutafuta umbea kwa ajili ya kuusambaza.

Kitendo cha kufananisha jina lolote la jf na mtu yoyote halisi ni kosa kubwa la kustahili ban, kwa sababu huku ni kumu expose mtu, which is not good at all kwa sababu kiukweli kabisa miongoni mwa wana jf, tuna jamaa kibao wa sehemu humu, mfano itokee umelijua jina halisi la Hutaki Unaacha, halafu ukamtaja, jee unajua ni nini kitakachompata?.

P
CC. https://www.jamiiforums.com/members/britanicca.290488/

Nimekwelewa pasco. Samahani nyingi kwa britannica. Ila ajitahidi kuwa na code kwenye mada zake.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Coded? Encrypted? Decrypted?

Hivyo kwa mujibu wa Magamba matatu ni hakuna umuhimu wa kupiga kura.
 
Nimekwelewa pasco. Samahani nyingi kwa britannica. Ila ajitahidi kuwa na code kwenye mada zake.

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante Sana Mkuu Massa, huu ni uungwana wa hali ya juu sana kusema sorry, Mkuu britanicca
nae afanye uungwana, japo huku kutaja taja majina kwake, kumetusaidia sana kumjua jamaa mmoja wa kihaya anaitwa Katto.

Lakini name calling is uncalling for kwa mtu wa caliber ya britanicca
P
 
Back
Top Bottom