Kuanzia 2015 Tanzania itatawaliwa "kidikteta" Ukweli huu hapa

Kuanzia 2015 Tanzania itatawaliwa "kidikteta" Ukweli huu hapa

Sasa hapa ndio unataka kuharibu, mimi mwenzio ni investigative journalist, hivyo uliponitajia tuu Katto, nineishafanya homework yangu vizuri, usizungumzie kabisa mambo ya jina Katto na adoption, ni top secret, maadam ni mimi na wewe tuu tunayemjua Katto, tuwe tunataja tuu Katto, not a word more, not word less.
P
Basi tunaishia hapa kuhusu Katto
 
No Hutaki Unaacha ni mtu wa jikoni, kule kule kunako, Pasco wa JF ni lumpenproletariat mmoja mganga njaa fulani, anayegangia njaa kwenye ukanjanja wa habari.
P
Kweli mkuu kuna siku tulikutana kwenye uzinduzi wa kiwanda cha Total pale Temeke Vetenari ndiyo ulikuwa organizer ya ile kazi ila ulikuwa busy nikashindwa kukushtua.
 
Kweli mkuu kuna siku tulikutana kwenye uzinduzi wa kiwanda cha Total pale Temeke Vetenari ndiyo ulikuwa organizer ya ile kazi ila ulikuwa busy nikashindwa kukushtua.
Next time ukiniona, nisalimie tuu.
P
 
Mkuu Dudu Washa, sijashtuka, bali nimeshangaa tuu na kumuuliza Mkuu Britannica, jina la mleta mada hiyo ni Magamba Matatu, jina la Mzee Joseph Mauzi amelipata wapi na amelileta la nini?.
P
Hakika amekiuka sheria za jf, hiyo haikubaliki hata kidogo ,alichokifanya ni ramli chonganishi
 
Daa, JF unajifunza mengi, Nimeunganisha nyuzi na kupata habari kamili, kiukweli kukiwa na ubishani wa jambo mambo yanakuwa wazi. Aksante Britanica kuanzisha na Pascal kukoleza, hence False + False = Tautology
 
Mkuu Britannica, jina la mleta mada hiyo ni Magamba Matatu, jina la Mzee Joseph Mauzi

Umelipata wapi?.
Vipi umesahau mambo ya name calling.
P

Sauti kubwa ikasikika kutoka kundi la watu waliosimama kustaajabu juu ya unabii ule, ikasema, "Na utuambie tena basi, huyu mtabiriwa atakaa nasi hata lini? Na ajaye baada yake ni nani?"

Ukimya ukatanda na kutawala, kisha akasema, atazamaye na aone!
 
Daa, JF unajifunza mengi, Nimeunganisha nyuzi na kupata habari kamili, kiukweli kukiwa na ubishani wa jambo mambo yanakuwa wazi. Aksante Britanica kuanzisha na Pascal kukoleza, hence False + False = Tautology
Huyu britanicca nyuzi na post zake usomage kwa umakini sana lazima utatoka na moja la ziada.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vichwa kama hivi ni vichache sana ulimwenguni.

Mi nadhan Mkuu Magalla ,naww ndo hawa hawa walotumika kutufikisha hapa.
 
Kwa nini nimeamua kusema hivi? Kuna mambo matano (5) makuu yananilazimisha kusema kuwa:
"Tanzania itatawaliwa kidikteta"
Ni vigumu sana kwa mtu asiyeona mbali kunielewa kirahisi na pia ni rahisi sana kwa anayependa demokrasia kunibeza na kuniona kama naota.

1. Kwanza kuna uwezekano mkubwa Rais ajaye ataingia madarakani kwa utata nikimaanisha kutakuwa na mizengwe katika utoaji wa matokeo kwani hali halisi inajionesha wazi kuwa kuna mvutano mkubwa wa vyama viwili na hakuna kinachokubali kuwa kimeshindwa ki-haki.Endapo mgombea wa chama tawala akashinda basi chama kikuu cha upinzani kitatumia nguvu ya umma ili kupata sapoti wakati aliyejiona kashinda kwa haki atakimbilia ikulu na kushawishi dola kulinda ushindi wake kadri wawezavyo.Tukumbuke yaliyozikumba nchi za :LIBYA, IVORY COAST, LIBERIA, NIGERIA, ZIMBABWE, KENYA, VISIWA VYA COMORO, MISRI na TUNISIA.

2. Pili ni ahadi atakazozitoa hususani zile za kushughulikia "MAFISADI". Ili kupambana na aliyekuzidi kifedha lazima uchukue fedha zake kwa nguvu hivyo atataifisha mali za waliosemekana ni wahujumu uchumi au mafisadi. Akiwa yupo kwenye hali hiyo lazima watamwinda hivyo itamgharimu kuwa dikteta katika kupambana na mafisadi ikiwa ni pamoja na kunyonga baadhi yao ili kuweka fundisho. Pia atajikuta analipa kisasi cha mateso yote yaliyompata katika harakati za kuingia ikulu.

3.Suala zima la maendeleo haliendani na kuwapa watu uhuru wa kukaa mijini na kuendeleza masuala kama ya kupiga debe, kutembeza vitu mijini, kuuza na kula madawa ya kulevya, polisi wa barabarani kupokea rushwa, maafisa wa TRA kusamehe kodi na kutoa vibali kwa njia za panya, viongozi wa serikali kutumia ofisi zao kama kampuni zao! Yote haya yatasababisha rais ajaye awe dikteta na mkatili kwa wazembe wote wanaokwamisha matarajio yake, ikiwa ni pamoja na kuwafurutisha vijana wote mijini na kuwafukuza kazi wazembe wote.

4. Suala zima la ushawishi wa dini, endapo ataegemea dini moja basi atajikuta yupo kwenye wakati mgumu kwani atajikuta amegeuka gafla na kuwa adui wa dini nyingine hivyo kujikuta akichukua maamuzi ya kibabe ili kukabiliana na upinzani kutoka dini fulani. Suala kujiunga na dini ya mashetani au "FREEMASONS" litakuwa jambo la kawaida na watu wengi wenye kupinga serikali watatoweka na wasijulikane wapo wapi.

5.Ushawishi wa nchi za magharibi; hili nalo ni tatizo ambalo nitafanya nchi isitawalike endapo Rais ajae ataamua kufuata matwakwa ya raia wake kwenye masuala la uwekezaji, ajira, ugawaji wa ardhi, kodi, na utaifishaji wa mali za umma kama viwanda, mashamba makubwa, n.k.na endapo atawageuka wananchi na kusikiliza matakwa ya nchi za magharibi basi atajikuta amepitisha sera ya ndoa za jinsia moja, biashara haramu ya siaha, urutubishaji wa nyuklia. Hali hii itapelekea wanachi waanze kumchukia na atajikuta anatumia nguvu za dola kulazimisha wananchi wakubali sera zake.

Pia kuna mambo mengine kama kuibuka vyama vya siasa vyenye nguvu vinavyotaka kumtoa madarakani kwa nguvu na atajikuta akiwasweka rumande wapinzani wengi ambapo itachafua hali ya hewa ya nchi. Pia utata wa mgawanyiko wa wabunge maana kuna kila dalili vyama viwili vyenye ushindani kugawana sehemu kubwa ya idadi ya wabunge na hivyo kumlazimisha Rais kuwa na wakati mgumu wa kuvunja bunge zaidi ya mara moja kwenye kipindi cha miaka mitano.

Pia suala la ajira litaendelea kutesa nchi na ongezeko la wasomi itakuwa pia tatizo hivyo itamlazimu kutumia sheria kali na za kibabe ili kuendesha utawala wake.

Vyombo mbalimbali vitanyimwa uhuru wa kutoa mawazo yao hii itapelekea vyombo vya habari vya magharibi kumuulika nchi na hivyo hali kuwa mbaya zaidi.

Swali la kujiuliza, Rais ajaye atakuwa nani ?

Ni vigumu kupata jibu la moja kwa moja ingawa watu wengi wanatazamia kuona sura mojawapo kati ya hizi:
- Zito Kabwe,
- Dr. Willbrod Slaa,
- Dr. Asha Rose Migiro,
- Edward Lowassa.
- Samwel Sitta
- Prof. Ibrahim Lipumba.
- Bernad Membe, na
- John Pombe Magufuli
.

Kwanini Watanzania wengi wanategemea kati ya watu hawa mmoja wapo atakuwa Rais wa Tanzania mwaka 2015?
Jibu kubwa na la msingi ni suala zima la uwajibikaji na kujituma.

Kwanini nasema hivyo?
Ukiangalia sura zote ni watu wachapa kazi, wanajituma na wenye maamuzi magumu kwa masuala nyeti ya nchi. Ingawa kila mmoja ana mapungufu yake lakini ukweli bado unabaki pale pale wanauwezo mkubwa wa kulifikisha taifa pale Watanzania wanapotaka ikiwa watatekeleza majukumu yao ipasavyo.

Bado suala la wapinzani kuungana na kumsimamisha mgombea mmoja litakuwa ni ndoto. Kwanza utofauti wa sera na mawazo yao vinakinzana. Pia kuna suala zima la itikadi ya chama na mitazamo. Wapinzani wamejifunza mengi kutoka kwa jirani zao Kenya. Hivyo hawapo tayari kuungana na kuanza kung'ang'aniana madaraka ni bora kila mmoja ashiriki kwa nguvu zake na ashinde kwa nguvu zake.
Wewe mtabiri mzuri, mengi uliyoyatabiri ndio tunayoyaona katika utawala huu wa sasa hivi
 
Sasa hapa ndio unataka kuharibu, mimi mwenzio ni investigative journalist, hivyo uliponitajia tuu Katto, nineishafanya homework yangu vizuri, usizungumzie kabisa mambo ya jina Katto na adoption, ni top secret, maadam ni mimi na wewe tuu tunayemjua Katto, tuwe tunataja tuu Katto, not a word more, not word less.
P

There is no such a thing as top secrecy. Mambo yanatokea ili mambo yaweze kwenda.
 
Back
Top Bottom