Kuanzia 2015 Tanzania itatawaliwa "kidikteta" Ukweli huu hapa

Kuanzia 2015 Tanzania itatawaliwa "kidikteta" Ukweli huu hapa

Mmmh bado una mawazo haya mkuu?
Haya ni mawazo yako , naweza kukuambia kuwa haya unayoyasema baadhi tao yapo sasa hivi , ubabe , kuvunjwa kwa baraza la mawaziri na mengine , free mason kuongelewa na wapuuzi bila sababu za msingi , so hakuna jipya
 
Mwandishi wa hii taarifa ya Mwaka 2012 anahitajika kupewa medali ya DHAHABU kwa huu utabiri though watu wengi walimpinga but uhalisia wa maisha ndo huu tunauona.

PONGEZI SANA MKUU KWA UTABIRI.
 
Mwandishi wa hii taarifa ya Mwaka 2012 anahitajika kupewa medali ya DHAHABU kwa huu utabiri though watu wengi walimpinga but uhalisia wa maisha ndo huu tunauona.

PONGEZI SANA MKUU KWA UTABIRI.
Tunamtafutia tuzo. Atapewa siku ya uhuru wa vyombo vya habari.
 
Hii dunia ina siri nyingi sana, Magufuli hapo alipo huenda akawa ni kama nembo tu ila kuna watu wapo nyuma yake wana mcotrol, ndiyo maana kuna siku alisha wai kusema urais ni mzingo yaani ni kama vile anajilaumu kukubali kuwa hapo alipo...
Ni kweli kuna watu nyuma yake lakini yote kwa yote wanalenga maslahi yao.
Kumbuka kuna kikundi cha watu waliojiingiza kwenye harakati za kupigania Uhuru wakiwa wameandaliwa na wakoloni na wakaaminiwa na waafrika wenzao waliokua na elimu Duni. Baada ya kupewa nafasi za juu wakatumia mifumo na katiba ile ile ya mkoloni kuanzaia kuchukua Mali za watu, ardhi na rasilimali zilizopo na kuziiita za serikali bila kutuambia hasa serikali ni nani zaidi ya wao wenye madaraka. Huku wakigoma kuweka mfumo wa haki wa kuipata hiyo serikali ili isimamia rasilimali zetu kwa haki.
Tunaona kwa sasa CCM ikiwa ndiyo yenye watu wa Daraja la juu na vyama vingine wakiwa ni kama wageni wasio na haki katika nchi hii.
Umetengenezwa ukoloni ndani ya watu wa Aina moja na taifa moja.

Kila kitu kina faida na hasara yake.
Hasara ya wachache inaweza ikawa faida ya wengi na faida ya wachache inaweza ikawa hasara ya wengi.

Tangu wanadamu walipokataa kutawaliwa na Mungu kama mfumo na kuamua kutafuta mfumo wao dunia imekua ikitawaliwa kwa faida ya wachache mana hakuna anayejua thamani ya mwingine zaidi ya faida na thamani yake mwenyewe na familia yake.

Ndio maana watawala na Wakuu wanajilinda kwa kila aina ya ulinzi kuanzia ushirikina mpaka kijeshi. Yote ni kuwa hawana imani na mtu yeyote. Kila MTU ni adui mbele yao Isipokua wachache wanaofanana nao . Hii inasababisha akitokea mtu akasema fulani ni adui wa maslahi na nafasi zetu basi panakua na uhasama mkubwa.

Ni pale tu tutakapopata watawala waliopo tayari kupoteza heshima zao na madaraka yao kwa faida ya wengi ndipo tutakapokuwa tunaujenga ufalme wa Mungu.
Leo hii watawala wanashindwa kwenye kura zilizopigwa tena wao wakiwa wamepata muda na fedha nyingi na kila fursa ya kupiga kampeni na kutumia kila aina ya ujasusi lakini wanapoona kura za wananchi hazitoshi wanakua tayari kutumia nguvu kubwa sana ya kuwapa ushindi hata pale wanapojua watapoteza maisha na uhai na kudhuru watu wengine;kwao hawajali


Tutafakari tu kwa Mfano Kule S.Afrika ambapo wakati wa kuelekea Uchaguzi ,serikali ya Chama cha ANC ambacho ndicho chenye dhamana ya kusimamia usalama wa watu wote kilikaa kimya na serikali yake wakati wageni wakiwa wanauawa na kufanyiwa vitendo vya kinyama na Mali zao kuporwa huku wakijua wazi kabisa kuwa wao ndio wanaobeba lawama ya kushindwa kutoa ajira ya watu wake baada ya Uhuru wa miaka zaidi ya 30 wa kujitawala.
Vyombo vya ulinzi na usalama navyo vilikaa kimya na hatujui ni kwa nini na kwa faida ya nani!!
sababu wao ndio wanaobeba lawama ya kushindwa kutoa ajira ya watu wake baada ya Uhuru wa miaka zaidi ya 30 wa kujitawala.

Walichofanya ANC na serikali yake ni kukaa kimya wageni waporwe na kuuawa mana walijua wangewadhibiti wale vijana wahalifu bila shaka wangepoteza kura nyingi kwa vijana ambao walionekana kuunga mkono wapinzani. Baada ya uchaguzi ndio wamejifanya sasa wanaomba radhi na kushughulikia ushenzi ule.

Hata hapa tunaona matamko ya kuruhusu boda boda kuendeshwa hovyo bila kufuata sheria jambo ambalo ni dhahiri litaleta karaha na hata ajali.
Kilicholengwa ni uchaguzi. Wanaogopa kusimamia ukweli hata pale wanapoona watapoteza.
Ni lazima tuwe na watu walioko tayari kusimamia haki na ukweli hata kama watapoteza madaraka na maslahi yao vinginevyo tutakua tunatawaliwa kwa uamuzi wa kakundi kadogo kwa malengo yao wanayaita ya taifa wakati hawafuati katiba wala sheria Bali maamuzi yao.

Waafrika sijui nani amewaloga.
 
Kama kamanda aliandaliwa tangia mda mrefu na tabia zake walikuwa wanazijua iweje tena walio mweka kwenye kiti waanze tena kumpiga vijembe kwenye mitandao? Kichwa kinaniuma
Hakuandaliwa bali woga wao na kuweka maslahi yao na Chama chao mbele ndio kilichofanya wakahofia Upinzani kuchukua nchi.

Kelele za ufisadi zilizokua zinapigwa na wapinzani nchi nzima usiku na mchana kila kona bila mipaka zilisababisha JK aonekane ni mtu asiyefaa.
Kumbe alijitolea kupoteza heshima yake kwa faida ya wengi . Alijenga Diplomasia kubwa ya nchi yetu na wakati mwingine alikutana na wapinzani na kuongea nao.
Hii ilisababisha nchi kupata Misaada mingi toka nchi za Magaharibi, Mashariki ya Kati, Kaskazini ,kusini na mashariki ya mbali. Huku wawekezaji na watalii walizidi kumiminika Nchini.

Wapinzani wakashindwa kuwa na ustarabu wakazidisha hujuma za kutumiwa na makundi ndani ya CCM kumchafua JK kwa kila eneo.
Bahata Mbaya zaidi pakawa na Spika ambaye alikua ameweza kuibana serikali kisawasawa.

Suala la kujenga Demokrasia ndilo lilolokuwa linapigwa vita ndani ya Chama chake na sio suala la uchumi wa nchi.
Makada wa CCM kwao Chama kwanza Tanzania baadae .
Kikwete alijaribu kulijenga kwanza Taifa lenye watu wamoja wanaoweza kukaa pamoja wakafanya shughuli za uchumi bila kujali itikadi zao,dini zao ,makabila yao na rangi zao jambo ambalo kwa sasa linatokomea.

Kundi lenye ubinafsi lilikuwepo ndani ya CCM na ndilo lililopora Mali za umma zikiwemo nyumba na kujimilikisha. Hilo halikuwahi kutaka nchi hii iongozwe na Chama kingine wala mtu mwenye huruma na maslahi ya wengi.
 
Jamaa alijua kila kitu,

kwenye kupanga haya majina, akaanza na yenye nafasi ndogo zaidi, afu akashuka lenye nafasi kubwa, na kumalizia lenyewe kabisa,

mwaka 2012, possibility ya Zitto kuwa raisi ilikuwa hafifu kuliko Slaa, Possibility ya Slaa ilikuwa hafifu kuliko mgombea wa CCM, Mgombea wa CCM,

Ukiangalia hapo pote, hao wote, unagundua walikuwa wapo kwenye mbio za uraisi na wanajulikana,na walikuwa tayari wanatajwa tajwa isipokuwa Magu, lakini yeye bado alimuweka na ndo akamweka kama mfunga Dimba. ambapo kwa mpangilio wake unagundua ndo alimpa chance kubwa

Bado sijajua jamaa alijuaje haya, ila ni somo kwa raia wanaokuwaga wa kwanza kucoment, kwa mihemko, kuwa si kila uzi unakurupuka kucoment kwa mihemuko.
 
Ila huu uzi, umenifanya niwe na amani

Nchi yetu ipo salama, Watu walio nyuma ya pazia ni watu makini sana wanajua kucheza karata zao vizuri
 
Back
Top Bottom