Kuanzia 2015 Tanzania itatawaliwa "kidikteta" Ukweli huu hapa

Kuanzia 2015 Tanzania itatawaliwa "kidikteta" Ukweli huu hapa

Dah wa mwisho kawa wa kwanza...!!
Mkuu fanya mpango utufunulie tena yajayo tuone kama yatakuwa yanafurahisha ama laa..
 
"Mnaniona mimi nacheka cheka, basi atakae kuja atakuwa BULLDOZER".. Haya maneno aliyasema Raisi Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete..

"katika utawala wangu matajiri wataishi kama Mashetani"..
"Kila mtu atakijua kijiji chake, mtarudi kijijini kwenda kulima"

haya maneno aliwahi kuyasema Raisi wa Tanzania John Pombe Magufuli..

Magufuli hakuupata Uraisi wa Tanzania kwa bahati mbaya, Mipango ilianza kupangwa miaka 3 nyuma ya Magufuli Kuwa Raisi wa Tanzania, kigezo kikubwa alichokuwa nacho Magufuli ni mchapa kazi, anajiamini, anathubutu..

Nani HASA hawa MAGAMBA MATATU!!?? Hawa ni wale waliokaa kikao na kukubaliana nani awe Raisi, na vipi Tanzania itawaliwe kuanzia 2015..

MAGAMBA MATATU si wengine bali ni MAGUFULI, MKAPA na KIKWETE..
 
Watabiri wapo sasa sijui connection na yanayotokea.Mwaka 2015 Nabii Bushiri alitabiri kuhusu tz,kwamba mshindi atakuwa huyo chaguo la lubuva ikawa,Tz itapigwa tetemeko likatokea BK watu wakatukanwa wao ndo wameleta tetemeko,akasema anga la Tz limejaa damu kila MTU ni shahidi damu zisizohatia zimepotea kuanzia Mkiru,Kigoma,Ben,Azori,nk kupitia utekaji wasiojulikana,pia akatabiri uchumi wa Tz utashuka kila mwaka kila mwaka hali inazidi kuwa ngumu jibu mnalo kila MTU ni shahidi ukitoa wateule kina bashit,slow,mulaga,le nk hakuna kundi lisilolimia meno yaani kuisoma namba haswaa!!! matajiri wamefanyiziwa utadhani sio raia hadi wengine wamelala mbele kuhamishia nje mitaji yao wanyonge waliochekelea matajiri kushushwa ni sawa na kuni mbichi kuichekelea kuni inayooungua wamenyongwa hatari yaani wako hoi majalala wamejikuta kumbe bila mafisadi kusaza wameshindwa kwenda chooni.Tumuombe mtabiri mwingine atutabirie yajayo hii namba ni lini mwisho wake kuisoma na haya yote yataisha lini?
Muanzishie uzi wake bushiri huyo ili wana wamchambue. Wewe unabishana na mwana aliyeyasema haya 2012 ambapo hata moshi mweupe wa uchaguzi 2015 haujaonekana,

Huwezi linganisha na aliyesema chochote 2015
 
Wana JF, MAGAMBA MATATU si mwengine bali ni mmoja katika waliomdhamini MAGUFULI aingie Madarakani,hii ni mipango madhubuti iliyokuwa imepengwa, kwa atakae kuja kututawala kwa Upande wa CCM

Haya yaliyoandikwa katika huu uzi sio kama yamendikwa kwa bahati mbaya au ramli,yameandikwa kwa Makusudi, kwa lengo la kupima msimamo na maoni ya wanachapa wa JF..

Huu uzi umekuwa disigned kuangalia upepo na msimamo wa Watanzania kwa muda wote wa awamu ya 5,

Mission accomplIshed, MAGAMBA MATATU, ameingia mitini, amebadilisha ID yuko pembeni anawachora wana JF,..

Siasa ni mchezo mchafu, wana JF mnatakiwa kutoa maoni yenu, kwa hayo yaliyoandikwa na huyu jamaa anayejiita MAGAMBA MATATU, sio kusifu utabiri wake..
Umefail hujaeleweka rudi tena
 
Kwa hio wasiojulikana kumwaga damu za watu,kusomesha namba mlishapanga.Jua ni nature lzm litoke
Yes, haya yalipagwa miaka mitatu kabla ya uchaguzi,.. Magufuli hakuchukua nchi kibahati mbaya, alitayarishwa, alipangiwa nini afanye, na analindwa..

Yanayotokea Tanzania chini ya Magufuli ni mipango iliyopangwa kwa muda mrefu..
 
ng'wanamangilingili ndio wewe MAGAMBA MATATU??.. Tujuze Mkuu
 
Kumbe MAGAMBA MATATU bado yuko active JF, kumbe hajaingia mitini... August 21 alikuwa hewani
IMG_20191023_205620.jpg
 
Yes, haya yalipagwa miaka mitatu kabla ya uchaguzi,.. Magufuli hakuchukua nchi kibahati mbaya, alitayarishwa, alipangiwa nini afanye, na analindwa..

Yanayotokea Tanzania chini ya Magufuli ni mipango iliyopangwa kwa muda mrefu..
Anga kujaa damu na kusomeshwa namba hayo nayo yalishapangwa?
 
Muanzishie uzi wake bushiri huyo ili wana wamchambue. Wewe unabishana na mwana aliyeyasema haya 2012 ambapo hata moshi mweupe wa uchaguzi 2015 haujaonekana,

Huwezi linganisha na aliyesema chochote 2015
Yalitabiriwa kabla ya uchaguzi 2015 ingia YouTube inatofauti gani na ya 2012,Then yote yaje kufanyika baada ya uchaguzi
 
Watu kuuawa lipo awamu zote. Matajiri ''kusomeshwa namba'' lazima ingetokea kwa sababu kampeni iliahidi kupigana na ufisadi. (Actually mimi sikubali watu wanaposema ''matajiri wamesomeshwa namba'' kwani hakuna mtu aliyedhulumiwa kwa sababu tu ni tajiri. Matajiri waliokumbana na mkono wa sheria walikuwa na makosa yaliyowafanya wakumbane na mkono wa dola.
Manji,MO,walifanya makosa gani tujuze.Bilicanas ilikuwa na kosa gani.Ufisadi upi hali vinara wa ufisadi wamepokelewa,wengine ni mabalozi kina dau,makengeza wako nje.Sema ni vita ya waliokinyume nao.Hizo biashara zilizohamishiwa nje je
 
Kwa nini nimeamua kusema hivi? Kuna mambo matano (5) makuu yananilazimisha kusema kuwa:
"Tanzania itatawaliwa kidikteta"
Ni vigumu sana kwa mtu asiyeona mbali kunielewa kirahisi na pia ni rahisi sana kwa anayependa demokrasia kunibeza na kuniona kama naota.

1. Kwanza kuna uwezekano mkubwa Rais ajaye ataingia madarakani kwa utata nikimaanisha kutakuwa na mizengwe katika utoaji wa matokeo kwani hali halisi inajionesha wazi kuwa kuna mvutano mkubwa wa vyama viwili na hakuna kinachokubali kuwa kimeshindwa ki-haki.Endapo mgombea wa chama tawala akashinda basi chama kikuu cha upinzani kitatumia nguvu ya umma ili kupata sapoti wakati aliyejiona kashinda kwa haki atakimbilia ikulu na kushawishi dola kulinda ushindi wake kadri wawezavyo.Tukumbuke yaliyozikumba nchi za :LIBYA, IVORY COAST, LIBERIA, NIGERIA, ZIMBABWE, KENYA, VISIWA VYA COMORO, MISRI na TUNISIA.

2. Pili ni ahadi atakazozitoa hususani zile za kushughulikia "MAFISADI". Ili kupambana na aliyekuzidi kifedha lazima uchukue fedha zake kwa nguvu hivyo atataifisha mali za waliosemekana ni wahujumu uchumi au mafisadi. Akiwa yupo kwenye hali hiyo lazima watamwinda hivyo itamgharimu kuwa dikteta katika kupambana na mafisadi ikiwa ni pamoja na kunyonga baadhi yao ili kuweka fundisho. Pia atajikuta analipa kisasi cha mateso yote yaliyompata katika harakati za kuingia ikulu.

3.Suala zima la maendeleo haliendani na kuwapa watu uhuru wa kukaa mijini na kuendeleza masuala kama ya kupiga debe, kutembeza vitu mijini, kuuza na kula madawa ya kulevya, polisi wa barabarani kupokea rushwa, maafisa wa TRA kusamehe kodi na kutoa vibali kwa njia za panya, viongozi wa serikali kutumia ofisi zao kama kampuni zao! Yote haya yatasababisha rais ajaye awe dikteta na mkatili kwa wazembe wote wanaokwamisha matarajio yake, ikiwa ni pamoja na kuwafurutisha vijana wote mijini na kuwafukuza kazi wazembe wote.

4. Suala zima la ushawishi wa dini, endapo ataegemea dini moja basi atajikuta yupo kwenye wakati mgumu kwani atajikuta amegeuka gafla na kuwa adui wa dini nyingine hivyo kujikuta akichukua maamuzi ya kibabe ili kukabiliana na upinzani kutoka dini fulani. Suala kujiunga na dini ya mashetani au "FREEMASONS" litakuwa jambo la kawaida na watu wengi wenye kupinga serikali watatoweka na wasijulikane wapo wapi.

5.Ushawishi wa nchi za magharibi; hili nalo ni tatizo ambalo nitafanya nchi isitawalike endapo Rais ajae ataamua kufuata matwakwa ya raia wake kwenye masuala la uwekezaji, ajira, ugawaji wa ardhi, kodi, na utaifishaji wa mali za umma kama viwanda, mashamba makubwa, n.k.na endapo atawageuka wananchi na kusikiliza matakwa ya nchi za magharibi basi atajikuta amepitisha sera ya ndoa za jinsia moja, biashara haramu ya siaha, urutubishaji wa nyuklia. Hali hii itapelekea wanachi waanze kumchukia na atajikuta anatumia nguvu za dola kulazimisha wananchi wakubali sera zake.

Pia kuna mambo mengine kama kuibuka vyama vya siasa vyenye nguvu vinavyotaka kumtoa madarakani kwa nguvu na atajikuta akiwasweka rumande wapinzani wengi ambapo itachafua hali ya hewa ya nchi. Pia utata wa mgawanyiko wa wabunge maana kuna kila dalili vyama viwili vyenye ushindani kugawana sehemu kubwa ya idadi ya wabunge na hivyo kumlazimisha Rais kuwa na wakati mgumu wa kuvunja bunge zaidi ya mara moja kwenye kipindi cha miaka mitano.

Pia suala la ajira litaendelea kutesa nchi na ongezeko la wasomi itakuwa pia tatizo hivyo itamlazimu kutumia sheria kali na za kibabe ili kuendesha utawala wake.

Vyombo mbalimbali vitanyimwa uhuru wa kutoa mawazo yao hii itapelekea vyombo vya habari vya magharibi kumuulika nchi na hivyo hali kuwa mbaya zaidi.

Swali la kujiuliza, Rais ajaye atakuwa nani ?

Ni vigumu kupata jibu la moja kwa moja ingawa watu wengi wanatazamia kuona sura mojawapo kati ya hizi:
- Zito Kabwe,
- Dr. Willbrod Slaa,
- Dr. Asha Rose Migiro,
- Edward Lowassa.
- Samwel Sitta
- Prof. Ibrahim Lipumba.
- Bernad Membe, na
- John Pombe Magufuli
.

Kwanini Watanzania wengi wanategemea kati ya watu hawa mmoja wapo atakuwa Rais wa Tanzania mwaka 2015?
Jibu kubwa na la msingi ni suala zima la uwajibikaji na kujituma.

Kwanini nasema hivyo?
Ukiangalia sura zote ni watu wachapa kazi, wanajituma na wenye maamuzi magumu kwa masuala nyeti ya nchi. Ingawa kila mmoja ana mapungufu yake lakini ukweli bado unabaki pale pale wanauwezo mkubwa wa kulifikisha taifa pale Watanzania wanapotaka ikiwa watatekeleza majukumu yao ipasavyo.

Bado suala la wapinzani kuungana na kumsimamisha mgombea mmoja litakuwa ni ndoto. Kwanza utofauti wa sera na mawazo yao vinakinzana. Pia kuna suala zima la itikadi ya chama na mitazamo. Wapinzani wamejifunza mengi kutoka kwa jirani zao Kenya. Hivyo hawapo tayari kuungana na kuanza kung'ang'aniana madaraka ni bora kila mmoja ashiriki kwa nguvu zake na ashinde kwa nguvu zake.
Naogopa kusema kwamba "Yanatimia..."
 
Kumuwajibisha kiongozi mzembe na mvivu sio udikteta ndugu zangu. Mbona wakati wa uongozi wa Mwl. Nyerere na Sokoine viongozi wote waliokuwa chini yao walijituma na kufanya kazi kwa bidii kwa kuogopa kujibishwa? Tatizo lililopo sasa hivi ni kupeana madaraka kwa kujuana au kulipa fadhila.
Mimi sioni kama kumuwajibisha waziri au Mbunge ni udikteta!!
Na uchumi ulipaa sana wakati huo maana viongozi walichapa sana kazi!!!
Nguvu kazi... kodi ya kichwa... uhujumu uchumi... bidhaa adimu... "TUKUTANE SARIDARAMU..."
 
Back
Top Bottom