Kuanzia 2015 Tanzania itatawaliwa "kidikteta" Ukweli huu hapa

Kuanzia 2015 Tanzania itatawaliwa "kidikteta" Ukweli huu hapa

Duuuuuuuh aseeeeeeeh ulikuwaa sahihi mkuu.
Na kuna watu wengi walipinga na kuonesha ujuvi wao kule mwanzoni, jamaa kazungumzia mpaka wasiojulikana tukiwa 2012. Kama ni kweli anaangalia mbali kwa namna hiyo, ana jicho la mwewe. Tumshawishi aendelee kushusha maono yake hapa.
 
Huyu mtu aliyeandika hapa wakati huo, alikua kwenye system kuu ya chama. Alikua anajua kila kitu on the next.
 
Hayupo rena duniani huyu. Ashatangulia peponi.
 
Huyu mtu aliyeandika hapa wakati huo, alikua kwenye system kuu ya chama. Alikua anajua kila kitu on the next.
Lakini kuyapangilia yajayo kwa mtiririko huo, tena ukiyaongelea yatakayotokea miaka 3 mbele na kudumu kwa miaka 5, sio suala la kuwa kwenye system ya chama tu. Ni uwezo binafsi haswa. Hatuna sera za miaka 200 ijayo kusema itafuata bila kujali mtawala au itikadi. JK alipowageuka watarajiwa wake, hata system ya chama isingeweza kusema tulikuwa tukienda wapi. Sasa kwa mfumo huo wa "itategemea nitaamkaje", kutabiri la lisaa lijayo tu ngondo aisee.
 
Ila ni kweli ana IQ kubwa huyu mtu. Pongezi zake but naskia katangulia mbele za haki.
 
Mnyonge mnyongeni haki yake apewe ulitabiri vizuri sana kwa mpangilio ulionyooka respect sana
 
Kwa nini nimeamua kusema hivi? Kuna mambo matano (5) makuu yananilazimisha kusema kuwa:
"Tanzania itatawaliwa kidikteta"
Ni vigumu sana kwa mtu asiyeona mbali kunielewa kirahisi na pia ni rahisi sana kwa anayependa demokrasia kunibeza na kuniona kama naota.

1. Kwanza kuna uwezekano mkubwa Rais ajaye ataingia madarakani kwa utata nikimaanisha kutakuwa na mizengwe katika utoaji wa matokeo kwani hali halisi inajionesha wazi kuwa kuna mvutano mkubwa wa vyama viwili na hakuna kinachokubali kuwa kimeshindwa ki-haki.Endapo mgombea wa chama tawala akashinda basi chama kikuu cha upinzani kitatumia nguvu ya umma ili kupata sapoti wakati aliyejiona kashinda kwa haki atakimbilia ikulu na kushawishi dola kulinda ushindi wake kadri wawezavyo.Tukumbuke yaliyozikumba nchi za :LIBYA, IVORY COAST, LIBERIA, NIGERIA, ZIMBABWE, KENYA, VISIWA VYA COMORO, MISRI na TUNISIA.

2. Pili ni ahadi atakazozitoa hususani zile za kushughulikia "MAFISADI". Ili kupambana na aliyekuzidi kifedha lazima uchukue fedha zake kwa nguvu hivyo atataifisha mali za waliosemekana ni wahujumu uchumi au mafisadi. Akiwa yupo kwenye hali hiyo lazima watamwinda hivyo itamgharimu kuwa dikteta katika kupambana na mafisadi ikiwa ni pamoja na kunyonga baadhi yao ili kuweka fundisho. Pia atajikuta analipa kisasi cha mateso yote yaliyompata katika harakati za kuingia ikulu.

3.Suala zima la maendeleo haliendani na kuwapa watu uhuru wa kukaa mijini na kuendeleza masuala kama ya kupiga debe, kutembeza vitu mijini, kuuza na kula madawa ya kulevya, polisi wa barabarani kupokea rushwa, maafisa wa TRA kusamehe kodi na kutoa vibali kwa njia za panya, viongozi wa serikali kutumia ofisi zao kama kampuni zao! Yote haya yatasababisha rais ajaye awe dikteta na mkatili kwa wazembe wote wanaokwamisha matarajio yake, ikiwa ni pamoja na kuwafurutisha vijana wote mijini na kuwafukuza kazi wazembe wote.

4. Suala zima la ushawishi wa dini, endapo ataegemea dini moja basi atajikuta yupo kwenye wakati mgumu kwani atajikuta amegeuka gafla na kuwa adui wa dini nyingine hivyo kujikuta akichukua maamuzi ya kibabe ili kukabiliana na upinzani kutoka dini fulani. Suala kujiunga na dini ya mashetani au "FREEMASONS" litakuwa jambo la kawaida na watu wengi wenye kupinga serikali watatoweka na wasijulikane wapo wapi.

5.Ushawishi wa nchi za magharibi; hili nalo ni tatizo ambalo nitafanya nchi isitawalike endapo Rais ajae ataamua kufuata matwakwa ya raia wake kwenye masuala la uwekezaji, ajira, ugawaji wa ardhi, kodi, na utaifishaji wa mali za umma kama viwanda, mashamba makubwa, n.k.na endapo atawageuka wananchi na kusikiliza matakwa ya nchi za magharibi basi atajikuta amepitisha sera ya ndoa za jinsia moja, biashara haramu ya siaha, urutubishaji wa nyuklia. Hali hii itapelekea wanachi waanze kumchukia na atajikuta anatumia nguvu za dola kulazimisha wananchi wakubali sera zake.

Pia kuna mambo mengine kama kuibuka vyama vya siasa vyenye nguvu vinavyotaka kumtoa madarakani kwa nguvu na atajikuta akiwasweka rumande wapinzani wengi ambapo itachafua hali ya hewa ya nchi. Pia utata wa mgawanyiko wa wabunge maana kuna kila dalili vyama viwili vyenye ushindani kugawana sehemu kubwa ya idadi ya wabunge na hivyo kumlazimisha Rais kuwa na wakati mgumu wa kuvunja bunge zaidi ya mara moja kwenye kipindi cha miaka mitano.

Pia suala la ajira litaendelea kutesa nchi na ongezeko la wasomi itakuwa pia tatizo hivyo itamlazimu kutumia sheria kali na za kibabe ili kuendesha utawala wake.

Vyombo mbalimbali vitanyimwa uhuru wa kutoa mawazo yao hii itapelekea vyombo vya habari vya magharibi kumuulika nchi na hivyo hali kuwa mbaya zaidi.

Swali la kujiuliza, Rais ajaye atakuwa nani ?

Ni vigumu kupata jibu la moja kwa moja ingawa watu wengi wanatazamia kuona sura mojawapo kati ya hizi:
- Zito Kabwe,
- Dr. Willbrod Slaa,
- Dr. Asha Rose Migiro,
- Edward Lowassa.
- Samwel Sitta
- Prof. Ibrahim Lipumba.
- Bernad Membe, na
- John Pombe Magufuli
.

Kwanini Watanzania wengi wanategemea kati ya watu hawa mmoja wapo atakuwa Rais wa Tanzania mwaka 2015?
Jibu kubwa na la msingi ni suala zima la uwajibikaji na kujituma.

Kwanini nasema hivyo?
Ukiangalia sura zote ni watu wachapa kazi, wanajituma na wenye maamuzi magumu kwa masuala nyeti ya nchi. Ingawa kila mmoja ana mapungufu yake lakini ukweli bado unabaki pale pale wanauwezo mkubwa wa kulifikisha taifa pale Watanzania wanapotaka ikiwa watatekeleza majukumu yao ipasavyo.

Bado suala la wapinzani kuungana na kumsimamisha mgombea mmoja litakuwa ni ndoto. Kwanza utofauti wa sera na mawazo yao vinakinzana. Pia kuna suala zima la itikadi ya chama na mitazamo. Wapinzani wamejifunza mengi kutoka kwa jirani zao Kenya. Hivyo hawapo tayari kuungana na kuanza kung'ang'aniana madaraka ni bora kila mmoja ashiriki kwa nguvu zake na ashinde kwa nguvu zake.
Duhhhhh, thread ni 2012.

Ila, ni kama anazunguza ya leo.

Hongera kwa kuona mbali
 
Huyu jamaa kama sikosei ana blood group AB+ kama langu.Sisi niwatu tunaoona yambele au kuoteshwa yajayo.
R.I.P MAGAMBA MATATU.!

Nchi saivi imekuwa ya sisiemu yani ubabe ubabe.Hakuna aliyefungua mdomo kukemea huu uozo unaofanyika ktk hii nchi ya dunia ya 3.Walinda katiba wapo kimya,hata mamlaka za kimataifa pia zipo kimya au ndio mnaogopa ile tunaita 'foreigners interference' which we all have experienced that USA interferes & devastating any country which goes against.
Aisee Kilwa94 huyu jamaa amekufa lini ?Jamaa ana maono sana
 
Huyu jamaa kama sikosei ana blood group AB+ kama langu.Sisi niwatu tunaoona yambele au kuoteshwa yajayo.
R.I.P MAGAMBA MATATU.!

Nchi saivi imekuwa ya sisiemu yani ubabe ubabe.Hakuna aliyefungua mdomo kukemea huu uozo unaofanyika ktk hii nchi ya dunia ya 3.Walinda katiba wapo kimya,hata mamlaka za kimataifa pia zipo kimya au ndio mnaogopa ile tunaita 'foreigners interference' which we all have experienced that USA interferes & devastating any country which goes against.
Amefariki lini?
 
Back
Top Bottom