Viongozi mliopo serikalini mkae mkijua,kuwa linaloanza kutoa mvuke karibu litashika kasi,kinachohitajika ni tume huru ya Uchaguzi ,na hili halina mswalie Mtume,Hii kero imeshapevuka na sasa kama ni jipu linakaribia kupasuka.
Na Mliopo madarakani msiingizwe mkenge na CCM,nikimaanisha CCM kama Chama na sio Serikali iliyopo madarakani.Serikali ni ya wananchi wote kama alivyo Raisi mara tu baada ya kuapishwa yeye na serikali yake hutakiwa kuwahudumia wananchi wote bila ya kujali itikadi za vyama vya wananchi hao.
Wananchi wote sasa wanasema umefika wakati wa kuwa na Tume huru ya Uchaguzi inayojiamini kama ilivyomihimili mingine. Hii Tume iundwe na kuanzia january 2022,kila mkoa utajiimarisha katika kudai Tume huru ya Uchaguzi.
Na hili litasaidia vyama vyote ikiwemo CCM ,maana kumekuwa na uenguaji wa wapendwa wetu kutoka CCM huenguliwa na kusababisha mtafaruku ndani ya Chama na kama haitoshi hata kukigawa Chama,mifano hai ipo tele.
Dawa ni Tume huru,yale mambo ya kuenguliwa kihuni wakati hakuna kisichorekebishika yawepo,sijui unaenguliwa kwa tu umekosea herufi na upumbavu mwingi usio na maelezo.
Ukiingia kwenye kuhesabu kura nako polisi wamejaa utasema ni majeshi ya kukodiwa kiasi ya kusababisha maafa yasio na sababu za msingi.
Tume huru ni wito na jambo linalotaka kupewa kipau mbele,anaeshinda awe ameshinda bila ya mizengwe,malalamiko yasiwepo kwa asilimia 99 kama chaguzi zilizopita.
Mdharau mwiba mguu huota tende na siku hizi mdharau kipele hutibu kensa.