Kuanzia leo nimeacha Rasmi kushabikia Mpira wa Tanzania

Kusema kweli sinaga hisia zozote na mpira wa bongo ,kiufupi naona kama mipira flani ya mchangani inayoendeshwa na wahuni ....
 
pale ushindi was Simba unapowanyima raha yanga wakati waliokuwa wakitamba wanataka kukutana na Simba
Walikua wanamtaka mshindi aliepita kwa uwezo wake sio wa kupigwa JEKI na msimamizi wa michezo.
Mimi naamini kwa dhati ya moyo yangu, Simba haihusiki kwa namna yoyote ile na uhuni ule wala refarii hakufanya kwa mahaba yake.
 
Nsikuchoshe na Usinchoshe,tusichoshane!.

SABABU NI HIZI.

1.Mpira wa Tanzania unaendeshwa Kisiasa,kwakuwa mimi sipendi siasa hivyo rasmi nimebwaga manyanga.

2.Upendeleo wa baadhi ya Timu hasa hizi kubwa (Yanga & Simba) huku timu ndogo zikidhurumiwa.

3.Maamuzi ya kionevu kwa timu zote kubwa na Ndogo.

4.Mpira wa Tanzania unanuka Rushwa,Kashfa za upangaji matokeo na uzwazwa,hivyo mimi kama kijana niliyeishia Form 6 nikiwa na Akili timamu nimeamua kabisa kutoshabika kabisa mpira wa Tanzania.

5.UPENDELEO

6.UPENDELEO

7.EPENDELEO

8.UPENDELEO

9.UJINGA WA VIONGOZI,,(Siwezi kuona naongozwa na viongozi wajinga)

10.SIASA ZA KIJINGA.(Mpira umekuwa kama mali ya chama fulani,na sisi tusio na vyama tunafanyaje?)

Njoo Taratibu ukiwa umemuaga mkeo,angalia nisije kupigwa ban kwa ajili ya ujinga wako.

Mercì Bandeko na Ngai
Hutaki ujumbe kinzani unataka mazuzu wa kukushangilia pekee
 
1.Mpira wa Tanzania unaendeshwa Kisiasa,kwakuwa mimi sipendi siasa hivyo rasmi nimebwaga manyanga.
Hata ulaya siasa inafika kwenye mpira. Mfano mwepesi chukulia sakata la kuuzwa kwa timu ya Chelsea baada ya kuanza kwa vita vya Ukraine. Siasa ndio iliamua pale.

2.Upendeleo wa baadhi ya Timu hasa hizi kubwa (Yanga & Simba) huku timu ndogo zikidhurumiwa.
As usual, kila sehemu ipo. Pale England kuna yule Howard Webb alikuwa akichezesha match za Man U ujue timu pinzani itagawiwa kadi kama njugu.

3.Maamuzi ya kionevu kwa timu zote kubwa na Ndogo.
Hata ulaya timu kubwa na ndogo zinalalamika kuonewa na waamuzi wa michezo na vyama vya mpira wa miguu. Mifano ipo ukitaka tutaleta.

4.Mpira wa Tanzania unanuka Rushwa,Kashfa za upangaji matokeo na uzwazwa,hivyo mimi kama kijana niliyeishia Form 6 nikiwa na Akili timamu nimeamua kabisa kutoshabika kabisa mpira wa Tanzania.

Mkuu, kuna sehem mpira hauna rushwa?
1. Zile tuhuma za Juve kupanga matokeo pale italia umesahau?

2. Vipi kuhusu skendo ya rushwa kwenye uenyeji wa kombe la dunia Qatar? Hata lile la Russia ilikuwa rushwa tupu.

3. Pale ufaransa umesau kuhusu timu ya Marsseile ilivyoshutumiwa kununua wachezaji wa timu pinzani na viongozi?

4. Bundesliga je, hujawahi kusikia kuhusu rushwa kwenye soka?

5. Pale FIFA na zile rushwa unasemaje, mfano tu wakati wa Blatter pale kulijaa rushwa kila eneo. Hata huu uchaguzi wa Infantinho ulituhumiwa kujaa rushwa.

6. Pale Uingereza tu penyewe rushwa inatembea sio mchezo.

Tuishie tu hapo.
 
Hata ulaya siasa inafika kwenye mpira. Mfano mwepesi chukulia sakata la kuuzwa kwa timu ya Chelsea baada ya kuanza kwa vita vya Ukraine. Siasa ndio iliamua pale.

As usual, kila sehemu ipo. Pale England kuna yule Howard Webb alikuwa akichezesha match za Man U ujue timu pinzani itagawiwa kadi kama njugu.

Hata ulaya timu kubwa na ndogo zinalalamika kuonewa na waamuzi wa michezo na vyama vya mpira wa miguu. Mifano ipo ukitaka tutaleta.

Mkuu, kuna sehem mpira hauna rushwa?
1. Zile tuhuma za Juve kupanga matokeo pale italia umesahau?

2. Vipi kuhusu skendo ya rushwa kwenye uenyeji wa kombe la dunia Qatar? Hata lile la Russia ilikuwa rushwa tupu.

3. Pale ufaransa umesau kuhusu timu ya Marsseile ilivyoshutumiwa kununua wachezaji wa timu pinzani na viongozi?

4. Bundesliga je, hujawahi kusikia kuhusu rushwa kwenye soka?

5. Pale FIFA na zile rushwa unasemaje, mfano tu wakati wa Blatter pale kulijaa rushwa kila eneo. Hata huu uchaguzi wa Infantinho ulituhumiwa kujaa rushwa.

6. Pale Uingereza tu penyewe rushwa inatembea sio mchezo.

Tuishie tu hapo.
Ulikuwa unatetea nini labda?

Napia nikujuze tu kwamba kujustify ujinga,dhuluma,ushenzi,upumbavv,rushwa,wizi n.k kwa kujaribu kumtaja mtu mwingine tena ambaye amefanya uovu kama wako na tena kwa kuleta mifano kabisa ni jambo la kipuuzi na la kijinga na kishenzi sana, na inakufanya wewe uonekane ni mshezi zaidi... weka hii akilini.
 
Back
Top Bottom