DELETED ACCOUNT
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 9,805
- 15,476
Ni jambo la kusikitisha sana "unapewa ndege" kama wanavyoiweka, una nafasi karibia 200 za kupeleka mashabiki wenye vibe la kutosha ila unawakosa watu wa kubeba unaishia kuokotezaokoteza maafisa, waandishi wa habari na wazee. Hivi Ndugai anaenda kutoa sapoti gani kwa Simba huko Morocco?
Nikiangalia wote walioenda katika safari hii, ambao kweli wanaweza kutoa mchango wa hamasa hawazidi watu 30 na haya yanaweza kuwa makadirio ya juu. King Faida kachukuliwa na wenzake wasiozidi 5 wakati kundi lake tu walitakiwa wawe si chini ya 30. Hii ni aibu!
Kuna faida nyingi za kuwa na kundi rasmi la ushangiliaji. Kwanza washangiliaji wanakuwa wanatambulika rasmi na wana pasi za kusafiria muda wowote safari, wanakuwa wamepewa mafunzo ya kukabiliana na mazingira korofi, wanakuwa wanajua wajibu wao muda wote wa mchezo, wanakuwa na mbinu mbalimbali za ushangiliaji zenye tija kwa timu, nk. Sasa hivi vikitokea hivi visafari tunasita kuchukua watu tukiogopa wanaweza kuzamia ikawa kashfa nyingine.
Kwenye ushangiliaji kuna mambo mengi. Kuna kuimba, kupiga makofi kwa pamoja, kurukaruka kwa pamoja, kusimama kwa mstari uwanja mzima, kubeba mabango, kupeperusha bendera, kushika vitambaa vikubwa, kuvaa nguo zinazofanana, nk. Haya hayawezi kufanyika bila kuwa na usimamizi maalumu au kundi kubwa maalumu la mashabiki la kuongoza wengine.
Kuna mtu humu JF aliwahi kutoa wazo la kusajili kampuni au kikundi cha hamasa ambacho hakifungamani na timu yoyote, yaani timu yoyote inaweza kuwatumia. Hili wazo nililisapoti sana na hii safari ya Simba inaonyesha mahitaji ni makubwa sana katika eneo hili na nakumbuka kumwambia nitampa sapoti akiwa tayari.