Kuanzia Septemba 2022 TANESCO itaanza kuwaunganishia umeme wateja wapya kwa kutumia Mita Janja

Kuanzia Septemba 2022 TANESCO itaanza kuwaunganishia umeme wateja wapya kwa kutumia Mita Janja

Donnie Charlie

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2009
Posts
16,908
Reaction score
19,123
Mita janja kuanza kuunganishiwa wateja Septemba

SERIKALI imesema kuanzia mwezi Septemba itaanza kuwaunganishia umeme wateja wapya kwa kutumia Mita Janja ili mkusaidia kununua umeme akiwa safarini bila kulazimika kuingiza kwenye mita yake.

Waziri wa Nishati, Januari Makamba.

Waziri wa Nishati, Januari Makamba, ameyasema hayo jana wakati akijibu swali kwa mmoja wa wananchi wa mkoa huo aliyetaka kujua ni lini Shirika la Umeme nchini (TANESCO) litaanza kuwafungia wateja wake mita za aina hiyo kwa kuwa baadhi yao wanazisubiri kwa hamu kubwa.

Waziri Makamba, alizungumza na wakazi wa mkoa huo na kutoa ufafanuzi mambo mbalimbali ya wizara yake kupitia kituo kimoja cha redio cha mkoani humo wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja mkoani Rukwa.

Alisema Wizara ya Nishati kupitia TANESCO, ilitangaza kuanzia mwezi Julai, mwaka huu ingeanza kuwaunganishia umeme wateja wapya kwa kutumia Mita Janja (Smart Meter), lakini kutokana na taratibu za ununuzi kutokamilika kwa wakati ilishindikana kuanza mwezi huo.

Makamba alisema tayari TANESCO imempata mzabuni na imekubaliana naye ataingiza mita hizo mpya zipatazo 300,000 ambazo zitatumika kuwaunganishia umeme wateja wapya kuanzia mwezi Septemba na wateja wa zamani wataendelea kubadilishiwa mita zao taratibu.

Waziri Makamba pia aliwataka wananchi wanaoishi kwenye vitongoji nchini kuwa wavumilivu kwa kuwa kuanzia mwezi Januari 2023, serikali itaanza kuunganisha umeme kwa wananchi walioko kwenye vitongoji vyote vilivyoko nchini, mpango wa mwanzo ilikuwa kuunganisha umeme kwenye vijiji vyote nchini.

Awali, akiwa katika kisiwa cha Mandakelenge, Ziwa Tanganyika, wilayani Nkasi, Mbunge wa Jimbo la Nkasi Kaskazini, Aidan Khenani, alimwomba waziri kuhakikisha wananchi walioko katika visiwa vya ziwa hilo wanapata nishati ya umeme pamoja na gesi.

Alisema wakazi wa visiwa hivyo wanahangaika kupata nishati ya kupikia kwa kuwa wamekata miti kwa ajili ya kuni na kuchoma mkaa na hawana nishati mbadala na kusababisha maeneo yao kuanza kugeuka jangwa na kuwalazimu kusafiri kwa mitumbwi umbali mrefu ili kutafuta kuni, hali inayohatarisha maisha yao.

Khenani alisema, wajasiriamali walioko katika visiwa vya Mandakelenge, Manda Ulwile, Mvuna pamoja na Kalungu wengi wao ni wanawake wanaofanya biashara za kuuza samaki wa kukaanga na wateja wao wanatoka mataifa ya Rwanda, Burundi na Zambia, kama wakipata nishati ya umeme na gesi itawasaidia kufanya shughuli zao katika mazingira salama.

Nipashe.
 
Zabuni ten pasenti new projects life goes on tanesco oyeee wateja karibuni ulimwengu wa kidigitali.
 
nimependa Quote yako Every government is run by liars, and nothing they say should be believed.
 
nimependa Quote yako Every government is run by liars, and nothing they say should be believed.
umeona aisee, january 2022 makamba alisema zitaanza kufungwa julai hivyo na hili linaweza likasogezwa tena mbele.
 
Back
Top Bottom