Kwakuwa ni mwanafunzi, itapendeza zaidi ukifanya biashara ambayo wateja wako watakuwa hao hao wanafunzi. Mi natoa idea zifuatazo kulingana na mtaji wako watakao kuja watatoa mawazo bora zaidi:
1. Watoto wa kike wa chuo wanapenda kuwa na cover za simu zaidi ya moja ili kumatch na nguo au kubadili style tu, unaweza kununua cover na earphone ukawa unawatangazia wenzio. Wakijua kuwa room kwako una cover nzuri watakuwa wanakuja kwako
2. Nunua handbags nzuri Kariakoo kama tano hivi, kila hand bag ikikupa faida ya elfu kumi (minimum) utakuwa na faida ya elfu hamsini hivyo mtaji utaendelea kukua. The more you sell, the more you will make profit. Baadae unaweza kuchanganya hand bags na viatu
3. Kipindi chuo kikiwa kinafungua unaenda Karume kununua mashuka ya mtumba unauzia wanafunzi wenzio (Hii inakuwa biashara ya msimu, inakuwa ina support biashara nyingine utakayokuwa unaifanya)
4. Mtaji wako ukija kukua huko baadae hamia kwenye biashara ya simu huku wateja wako walengwa wakiwa wale wale wanafunzi. Mpaka unamaliza degree utakuwa na mtaji mkubwa kidogo kufanya biashara kubwa zaidi
NB: Tangaza pia kwenye socia media, zinasaidia sana
- Ikifika mwakani tuombe uzima, mi maskini mwenzio lakini nitakutafuta nikuchangie laki nyingine ya mtaji endapo nikiona kweli ulianza biashara.
Kila la kheri dogo lasi