Kuanzisha biashara

Kwani belo moja ni sh ngapi mkuu?
Sifahamu mi nimesajest hiyo biashara kutokana na kukutana na nguo za 2000 karume na wafanya wanaoleta huku mikoani huuza bei juu ya hiyo.

Ila navyofahamu bei zinatofautiana na gredi, mfano gredi A nguo moja unaweza kuta zaidi ya 10,000.
 
Kama upo Dar chukua hiyo laki moja nenda pale karume lenga mashati kwa bei ya 2000 kisha mida ya saa nne sogea mpaka kkoo tafuta sehemu iliyochangamka ongea na wenyeji watakukodisha eneo la kumwaga. Piga debe kwa bei ya 5000 utakua umeingiza sh 3000 kwa kila shati moja. Baada ya wiki tuletee mrejesho hapa. Kikubwa weka aibu pembeni wape wateja burudani ongeza na vituko kidogo... Usiwe mpole sana. Itakula kwako
 
1.biashara ya fruits catering
2. Kibanda cha Tangawizi na gahawa
3.soksi, mashati, culture,
4. Nunua dvd za kihindi au series zozote zinazo bamba kitaa uwe unaweza
5. Kama unaweza hanzisha u tube channel ila hapa ubidi uwe unatembele sehem zile interesting ambazo watu wangependa kwenda then una upload kwene channel yako ( very famous in kenya hiki kitu bongo sijaona[emoji1139])
6. Kama unaujuzi wakitu chochote kama .. Shoe shine, wakupaka rangi kucha za wadada tumia huo kama mtaji
7. Afu sahv nikipindi cha first year wanachuo wewe katafute mitumba mikali uje kuwapiga watoto wanao taka kuwa mabishoo
8.ingia na ubia na biashara yoyote mfano Tafuta muuza chips [emoji489] ambaye hauzi kuku , filigisi au sausages awe anaweka vitu ev kwene kabati lake na mna ongea utakuwa mnalipana vipi
9.kama vip tengenza hata icream zenye flavour za tofauti uza kwa watoto wa shule (inalipa sana kipindi vya shule)
10)……… ..
 
Thank you very much for your time and ideas
 
Hizi ideas zipo realistic sana mkuu! Nimezielewa halafu zinaonekana hazili mtaji mkubwa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…