Ahsanteni wakuu mliochangia. Acha na mimi niongeze senti tano yangu. Kila wakati mtu anajibu save it. I will help in the future. Plenty of good materials, I have seen here. Here we go:
Kwanza nataka kuhakikisha nimekuelewa. kwa hiyo, usiponielewa naomba uni pm. kwa sababu huu mtiririko ukifumuka utapa support ya akili yako mpaka ukimbie.
1. Wewe ni muhandisi (muhandisi wa namna gani? kwa mfano wa nyumba za kuishi, au nyumba za maofisi na viwanda, au unapakaa chookaa na kufany marekebisho kwenye nyumba, je unatengeza barabara, je unatengeneza mifereji ya mashamba, yaani ingekua vizuri ukituambia ufundi wa aina gani unapenda kuendeshea maisha yako. Itasaidia kukagua soko lako kimakini zaidi.
2. Umesema lengo la biashara ni kukuza kipato (hengera and goodluck). Tuambie Unataka kuwa na uwezo wa kuingiza shilingi ngapi kwa mwaka? Usione aibu kutaja namba yoyote. Hii itasaidia kufikiria kulingana ujuzi, experiance, na network yako itakuaidia vipi kufikia malengo yako ya kuongeza kipato.
3. Kuhusu Problem ni Utaratibu. Hawa wana JF watakusaidi,. (Fikiria kwanza 1 & 2 kabla ya register your business).
4. Kuhusu Mtaji na Rasilimali Zingine. (a) Ujuzi ulionao ndio Rasilimali kubwa ulionayo sasa hivi. Kwa hiyo angalau una mfanya kazi mmoja. Kuna 13 simple rules za kufanikiwa katika business nadhani Invisible aliposti jana, hapa jamvini, ZISOME, ukiwa na swali tafadhali ni pm kuhusu hizo sheria za kujiendeleza kibiashara. (b) Rasilimali kama Jembe, koleo, nyundo, kalam ya mkaa, toroli, utapata. Hizo benki ziko mbele ya mlango unazania shida yao nini, Raha yao ya kwanza ni kukopesha. La muhimu hawataki wagidwe kama mabwege. Kuto kulipwa ndio kitu cha kwanza benki wanaogopa. Kama utaweza kuwahikishia biashara yako inahijika katika jamii, kuna about 50% chance watakukopesha hela za kuwekeza kwenye vifaa.
Fuatilia mtiririko wa plani za biashara tuliovugumiziwa hapa jamvini hivi karibuni nimesahau kichwa cha habari. Hiyo pia isome, au tafuta mtu msaidiane kuichakatua its components. it's nice