Kuanzisha Biashara

Kuanzisha Biashara

Naomba akili yako ikae ikijua kuwa biashara ni risk.
Unaweza ukafanikiwa au la! Jiandae kwa yote mawili.
Kila la heri mkuu na nakuombea ufanikiwe.


Mkuu ili ufanikiwe maishani lazima urisk. Endelea na mipango yako lakini make sure uko na backup eg insurance. ili usije kuwa frustrated.
 
Wana JF
Katika pitapita zangu ndani ya jukwaa hili nimejionea mambo mengi sana ambayo yanaweza kutusaidia kama Watanzania kujikwamua kiuchumi.

Pamoja na hayo mimi pia nimefika mahali nimeona ni bora na mimi niombe ushauri wa jinsi ya kuanzisha biashara ili angalau niweze kukuza kipato changu kwani kwa kutegemea ajira sio rahisi mafanikio ya kiuchumi kupatikana. Mimi ni mhandisi na ningependa kumiliki kampuni ya Uzabuni (Contractor) itakayojihusisha zaidi na masuala ya umeme & Mitambo (electrical & mechanical) ila ugumu ninaouona ni suala zima la utaratibu na pia mahitaji muhimu kwa biashara hii sana sana vitu kama mtaji na rasilimali zingine.

Kwa wana JF wenzangu naamini kabisa wapo wenye upeo mkubwa juu ya hili, naombeni mnipe ushauri wa nini naweza kufanya ili kuitimiza adhma yangu ya kumiliki biashara yangu mwenyewe. Pia kama kuna ideas zingine nitashukuru kama mtanipatia

Nawasilisha...
Nipo kwenye the same professional lkn ni Civil Engineer.Unaitwa ukandarasi ni biashara sijui upande wa umeme na mechanical lkn Civil kulingana na daraja ulilonaro mtaji sio issue sana.Tatizo kubwa hapa ni upatikanaji wa kazi na hapo ndio panaitajika pesa ki ukweli,ukipata kazi ukiwa na mkataba waweza kupata malipo ya awali au kuazimwa pesa na mashirika ya fedha.
 
kwa ishu ya capital, nakushauri utafute mkopo toka bank, au financial institution yeyote. kama utakua na assets kama vile nyumba au plot, itakua rahisi zaidi kupata mkopo.
 
Naomba akili yako ikae ikijua kuwa biashara ni risk.
Unaweza ukafanikiwa au la! Jiandae kwa yote mawili.
Kila la heri mkuu na nakuombea ufanikiwe.
hili ni kweli na limeshanitokea ila najipanga upya sijakata tamaa
 
Kazi zipo nyingi tu,unatakiwa uandae fungu la kutafutia Tenda,hapo ndio kazi kubwa,kama contract ni ya millioni 100 unaandaa kifungua bahasha(tender box) kama milioni 7-10,na ukishakuwa awarded unawakilisha fungu lililo salia.
si utani its Just the Sad Facts of contracting in Bongoland
Ahsanteni wakuu mliochangia. Acha na mimi niongeze senti tano yangu. Kila wakati mtu anajibu save it. I will help in the future. Plenty of good materials, I have seen here. Here we go:

Kwanza nataka kuhakikisha nimekuelewa. kwa hiyo, usiponielewa naomba uni pm. kwa sababu huu mtiririko ukifumuka utapa support ya akili yako mpaka ukimbie.

1. Wewe ni muhandisi (muhandisi wa namna gani? kwa mfano wa nyumba za kuishi, au nyumba za maofisi na viwanda, au unapakaa chookaa na kufany marekebisho kwenye nyumba, je unatengeza barabara, je unatengeneza mifereji ya mashamba, yaani ingekua vizuri ukituambia ufundi wa aina gani unapenda kuendeshea maisha yako. Itasaidia kukagua soko lako kimakini zaidi.

2. Umesema lengo la biashara ni kukuza kipato (hengera and goodluck). Tuambie Unataka kuwa na uwezo wa kuingiza shilingi ngapi kwa mwaka? Usione aibu kutaja namba yoyote. Hii itasaidia kufikiria kulingana ujuzi, experiance, na network yako itakuaidia vipi kufikia malengo yako ya kuongeza kipato.

3. Kuhusu Problem ni Utaratibu. Hawa wana JF watakusaidi,. (Fikiria kwanza 1 & 2 kabla ya register your business).

4. Kuhusu Mtaji na Rasilimali Zingine. (a) Ujuzi ulionao ndio Rasilimali kubwa ulionayo sasa hivi. Kwa hiyo angalau una mfanya kazi mmoja. Kuna 13 simple rules za kufanikiwa katika business nadhani Invisible aliposti jana, hapa jamvini, ZISOME, ukiwa na swali tafadhali ni pm kuhusu hizo sheria za kujiendeleza kibiashara. (b) Rasilimali kama Jembe, koleo, nyundo, kalam ya mkaa, toroli, utapata. Hizo benki ziko mbele ya mlango unazania shida yao nini, Raha yao ya kwanza ni kukopesha. La muhimu hawataki wagidwe kama mabwege. Kuto kulipwa ndio kitu cha kwanza benki wanaogopa. Kama utaweza kuwahikishia biashara yako inahijika katika jamii, kuna about 50% chance watakukopesha hela za kuwekeza kwenye vifaa.

Fuatilia mtiririko wa plani za biashara tuliovugumiziwa hapa jamvini hivi karibuni nimesahau kichwa cha habari. Hiyo pia isome, au tafuta mtu msaidiane kuichakatua its components. it's nice
 
Mkuu Dmusa vipi mpango wako umefikia wapi so far
 
Back
Top Bottom