Ndugu jamaa na marafiki, poleni na majukumu ya kila siku!!
Nimekuja kupata ushauri kwa yeyote mwenye idea kuhusu kuanzisha rasmi kituo cha soka la watoto (academy). Nimejiwa na wazo ili baada ya kuona kwamba michezo ni ajira pia ni biashara. Tuna vijana tunawahudumia hapa mtaani kwetu kwa kuwawezesha nikimaanisha ku-organise,kugharamia vifaa kama jezi, mipira, nyavu za magoli na kuwatibia in case wanapoumia.
Pia tuna wahudumia chakula na usafiri pale inapobidi kufanya hivyo. Tumekuwa na mwamko huo kwa zaidi ya miaka mitatu sasa, na kwa bahati hawa watoto kila tunapowapelelka basi baada ya muda utakuta wanachukuliwa na kusajiriwa na vilabu vya ligi kuu, huku kituo hakiambuliii hata sh moja.
Hivi sasa ninavyoandika vijana watano tayari wako mbioni kujiunga na vilabu mbalimbali vya premier league. Naomba muongozo ni kwa jinsi gani tunaweza kugeuza hili jambo kuwa ni biashara kwa kituo badala ya kubaki na sifa tuuu kuwa tuna vijana wapo ligi kuu kutoka kwetu?
Napenda kuwakilisha.