Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu,
Peleka maombi yako kwa msajili wa magazeti. Katika maombi yako eleza unakusudia gazeti liwe linahusu nini.
Utatakiwa kulipa ada ya Tshs. Laki Tano (hii huenda ishaongezeka).
Kama uko Dar, wacheki Wizara ya Habari, Vijana na Utamaduni.
Mambo yakikunyokea utapata usajili wa kisheria wa gazeti lako.
Sasa hapo mkuu uwe na hela za uchapishaji, usambazaji na kuwalipa waandishi. Tafadhali usitumie makanjanja.
Kila la heri.
nenda pale maelezo, karibu na askari monument/Q-print utapata maelezo zaidi, kwakuwa walisema watachange baadhi ya vitu, ila kama jamaa alivyosema unaandika kwanza barua ikielezea malengo etc na pia uwe tayari na majina angalau matatu ya hilo gazeti then wenyewe watapick moja,watakupa form yenye mambo mbalimbali, ila we nenda maelezo upate kila kitu
Jamani si mumujibu!
...Wakuu, mwenye Ufahamu na haya mambo aje atiririke hapa kumsaidia mwenzetu. Nami pia ningependa mno kufahamu kuhusu hili..!
Nenda pale habari maelezo na barua ya kuomba usajili ikiwa na machaguzi ya majina ya gazeti lako,jina litakalopita utapewa fomu ya kujaza vitu vinavyohitajika ni mhariri,waandishi wa habari wasiopungua wanne ( kutoka vyuo vya serikali), dammy,hati ya printa kukubali kukuprintia hicho kitabu na benki statement ya kuweza kuprint magazeti mara kumi na laki tano kama bond.
Baada ya hapo utapewa cheti utakipeleka maktaba ndio wanaotoa isbn ( International Serial Business Number)
Asante sana mkuu kwa ushauri murua. Nitafuata maelekezo yako