SoC04 Kuanzishwa kwa kisimbuzi kimoja kitakacho kusanya channel za ndani na nje ya nchi

SoC04 Kuanzishwa kwa kisimbuzi kimoja kitakacho kusanya channel za ndani na nje ya nchi

Tanzania Tuitakayo competition threads
Joined
Jul 19, 2022
Posts
64
Reaction score
89
Miaka ya 1960 mpaka miaka ya 2000 nchini Tanzania runinga nyingi zilitumia mfumo wa analojia ambapo mfumo huo uliwezesha runinga hizo kupata matangazo ya moja bila kuwa na kisimbuzi ambapo mtumiaji alipaswa kuunganisha runinga yake na antena ili kupata matangazo ayo.
FB_IMG_17167034348636518.jpg

kielelezo picha namba 1.mfano wa TV zilzotumia mfumowa analojia.

Maendeleo yakazidi kupiga hatua ambapo mfumo wa urushaji wa matangazo ukahamia kwenye visimbuzi ,pia kukaja runinga janja "smart TV " ambazo zimeboreshwa na zina uwezo wa kupokea matangazo kwa njia mbalimbali na kwa namna nyingi "multi function ".
FB_IMG_17164366690276383.jpg


Kielelezo picha namba 2.runinga janja (smart TV).

Kutokana na maendeleo aya kampuni mbalimbali zimejiingiza kwenye uzalishaji na uuzaji wa visimbuzi .Kwa Tanzania kampuni ambazo zimeuza na kusambaza sana visimbuzi ni pamoja na star times, Azam Tv pamoja na DSTV na kampuni nyingine nyingi ,hii imepelekea ushindani kuongezeka miongoni mwa makampuni na kupelekea watu wengi kuhitaji huduma hii kutoka katika kampuni mbalimbali. Hivo kuna haja ya kuwa na kisimbuzi kimoja kitakacho kusanya channel za ndani na nje ya nchi.
IMG20240530171759.jpg


Kielelezo picha namba 3.mfano wa kisimbuzi.

Umuhimu wa kisimbuzi hiki

Kupunguza mzigo wa kuwa na visimbuzi vingi
; kisimbuzi hiki kitampunguzia mtumiaji mzigo mkubwa wa visimbuzi kwani kitajumuisha channel za ndani na nje ya nchi ambazo zingepatikana kwenye visimbuzi mbalimbali. Mfano wapenzi wa soka la ndani na nje ya nchi wataweza kutumia kisimbuzi kimoja kutazama soka ambapo awali iliwapasa kuwa na kisimbuzi zaidi ya kimoja .(DSTV na Azam TV)
IMG_20240509_000059.jpg


Kielelezo picha namba 4.mfano wa mtumiaji mwenye mzigo wa kisimbuzi zaidi ya kimoja.

Kupunguza gharama; kisimbuzi kitapunguza gharama kwani vipindi vingi mteja atavipata ndani ya kisimbuzi kimoja hivo ataokoa gharama za ununuzi wa visimbuzi vingi.Mfano kisimbuzi cha Azam Tv cha dishi kinagharimu fedha za kitanzania takribani shilingi 99000.Pia kisimbuzi cha star times kinagharimu fedha za kitanzania takribani shilingi 79000 ikiwa kutakuwa na kisimbuzi kimoja itasaidia kuokoa gharama hizi za kununua visimbuzi tofauti tofauti.

Kurahisisha ufanyaji wa malipo na utunzaji wa kumbukumbu; kusimamia au kuongoza kitu kimoja ni rahisi zaidi kuliko kuwa na kitu zaidi ya kimoja. Mfumo wa malipo wa visimbuzi hufanyika kwa njia ya kielektroniki. Hivo pakiwa na kisimbuzi kimoja itarahisisha zaidi ufanyaji wa malipo ambapo mtumiaji atakuwa na namba moja ya malipo ambayo anaweza kuhiifadhi kirahisi kwenye mfumo wa malipo Kama kumbukumbu ya malipo ili kurahisisha ufanyaji wa malipo.

Kupata channel nyingi kwa Pamoja na urahisi zaidi; ambapo mtumiaji wa kisimbuzi hiki atakuwa na uwezo wa kupata vipindi vingi bila ulazima wa kuwa na visimbuzi vingi ,ambapo awali ilimpasa kuwa na visimbuzi vingi ili kupata matangazo tofauti tofauti. Lakini kupitia kisimbuzi hiki ataweza kuona au kutizama vipindi vingi kwa wakati tofauti tofauti ndani ya kisimbuzi kimoja.

Huduma (urushaji) wa matangazo kuwa wa umma si wa mtu binafsi au kampuni; ambapo waandaji wa vipindi jukumu lao ni kuzalisha na kuuza matangazo kwa mmiliki wa kisimbuzi hiki ambaye ni serikali ya Tanzania.Tofauti na hali iliopo sasa haki miliki ya kisimbuzi" X" ipo chini ya mtu mmoja au kampuni ambapo ikitokea kampuni hiyo imeingia mgogoro na serikali nchi au na mshindani mwenzie kunaweza kupelekea kusitishwa urushaji wa matangazo hivo watu kukosa huduma.

Changamoto zinazoweza kukikumba kisimbuzi hiki.

Kukatika kwa matangazo eneo kubwa /maeneo mengi kwa wakati mmoja
;mabadiliko ya hali ya hewa au majira ya mwaka yanaweza kupelekea itilafu katika urushaji wa matangazo haya. Mfano kipindi cha masika visimbuzi vingi hushindwa kufanya kazi kwa ufanisi wake. Kwa kuwa matangazo ya kisimbuzi hiki yatakuwa chini ya mrushaji mmoja hivo kupelekea eneo kubwa kubwa kukosa matangazo hayo. Tofauti na ambapo urushaji wa matangazo aya ungekuwa chini ya kampuni tofauti tofauti. Mfano channel za TBC1, ITV na TBC2 hurushwa katika kila kisimbuzi nchini endapo kisimbuzi "X" matangazo yatakatika kutokana na changamoto Kama mvua lakini kisimbuzi" Y"kitaendelea na urushaji wa matangazo.

Kupungua kwa kasi ya ushindani na ubunifu miongoni mwa wazalishaji wa vipindi; ushindani na ubunifu ni chachu kubwa ya maendeleo katika sekta au nyanja yoyote ya kiuchumi.kwa kuziweka channel hizi katika kisimbuzi kimoja na kufanya kisimbuzi hiki kuwa kisimbuzi cha umma kutapelekea wazalishaji wengi wa vipindi kupoteza ubunifu kwa kuwa ushindani utakuwa umeshuka kwa kiwango kikubwa Sana kwani wao watauza vipindi kwa mmiliki wa kisimbuzi tofauti na ambapo kila kampuni ingemiliki kisimbuzi chake ambapo ushindani ungekuwa mkubwa wa kukusanya wateja.

Kupungua kwa ajira ;kuweka kwa channel nyingi kwenye kisimbuzi kimoja kutapunguza wigo wa ajira kwa mawakala, mafundi na warusha matangazo ambao awali walifanya kazi hizo katika kampuni zao husika za visimbuzi. Mfano kampuni za DSTV,Star times, Zuku na Azam Tv zikiunganishwa kwa pamoja wafanyakazi wengi watakosa kazi kwa maaana wigo wa nafasi hizo utaminywa. Tofauti na awali ambapo kila mfanyakazi angefanya kazi hiyo katika katika kampuni yake.

Kuongezeka kwa gharama ya manunuzi ya kisimbuzi na vifurushi; kutokana na kisimbuzi hiki kuwa kimoja tu na kinamililikiwa na serikali, gharama za manunuzi ya kisimbuzi hiki na vifurushi yatapanda kwa kuwa kila kampuni itahitaji mgao kwa kwa ajili ya kujiendesha kwenye uzalishaji na urushaji wa vipindi. Mfano DSTV watahitaji wapate faida ambayo itaweza kuendesha shughuli zao hivohivo kwa star times na kampuni nyingine.

Msongamano kwenye mfumo wa malipo; kutokana na watu wote kutumia mfumo mmoja wa malipo inaweza pelekea msongamano mkubwa kwenye mfumo hivo watu kuchelewa kupata huduma kwa wakati .

Nini kifanyike kukabiliana na changamoto hizi?

Kuimarisha mifumo ya urushaji wa matangazo; ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi (mvua, upepo mkali) na matatizo ya kiufundi maboresho yanahitajika kama kuanzishwa na kuboreshwa kwa aplikesheni ambazo zitapatikana kwenye simu na kompyuta mfano azam Max, startimes ON ili kuwafikia watu kila Kona hata kama kuna mvua pia matangazo aya yasitegemee uendeshaji wa njia ya satelaiti pekee bali yatumie njia ya tovuti .

Kutoa ajira kwa watu wenye ujuzi na uwezo kulingana na kitengo husika ;hii itapelekea huduma kupatikana kwa wakati kila mwajiriwa atakuwa na wajibu kutokana na kitengo husika watu wa matangazo watahusika na matangazo na watu wa masoko watahusika na masoko pia, wasambazaji nao watasambaza visimbuzi kila kona ya Tanzania.

Kuboresha mifumo ya malipo ;ili kupunguza msongamano katika malipo na kusababisha kucheleweshwa kurushwa kwa matangazo mifumo ya malipo iimarishwe kwa njia ya mtandao na menu za simu,pia kwa njia ya aplikesheni.

Kutolewa kwa tuzo na zawadi mbali mbali kwa wazalishaji wa vipindi; hii itaongeza kasi ya ushindani ya uzalishaji wa maudhui bora miongoni mwa wazalishaji wa vipindi na maudhui hivo kuipa jamii maudhui bora.

Mwisho kisimbuzi chochote kinahitaji uangalizi mkubwa wa mimiliki ili kiweze kudumu, suala la mabadiliko ya tabia nchi pia ni muhimu kukabiliana nayo ili kuweza kutunza na kuhifadhi kisimbuzi.
NB. Picha zote zilizotumika kwenye makala hii chanzo ni kutoka kwa mwandishi wa makala hii amepiga picha sehemu mbali mbali kwa kamera yake. (0749442229)
 
Upvote 2
Kutolewa kwa tuzo na zawadi mbali mbali kwa wazalishaji wa vipindi; hii itaongeza kasi ya ushindani ya uzalishaji wa maudhui bora miongoni mwa wazalishaji wa vipindi na maudhui hivo kuipa jamii maudhui bora.
Naunga mkono maudhui bora kulipwa. Sema ku'monopolize' visimbuzi inaweza kuenda kinyume na haki za uhuru wa vyombo vya habari.

Kikatiba mwananchi anayo jaki ya kutafuta na kutumia taarifa kutoka popote duniani, hivyo atakayetaka canal sports apate, atakayetaka skylink aipate.... aaani kiufupi badala ya kuvipunguza tungeviongeza maradufu au we unaonaje?

Sema tena mtaka yote kwa pupa, hukosa kuyafaidi yote aseee. Hatari
 
Tanzania sijui nani alituaminisha kuwa sekta binafsi ni mbaya,
Kwa hio unataka uturudishe kipind ambacho serikali inacontrol media zote? Mana watakuwa na uwezo wa kuzuia channels ambazo hawazipend,
Pia utaua ubunifu kwenye media,


Sababu hizo mbili tu ni nzito kufanya hoja yako iwe nullified, hatuwez risk media industry yote kisa mzigo wa visimbuzi vitatu
 
Back
Top Bottom