Abdul Said Naumanga
JF-Expert Member
- Jan 28, 2024
- 673
- 1,318
Mnamo tarehe 9/05/2024, Halmashauri ya Manispaa ya Moshi ilitangaza kuanzisha kodi mpya ya sherehe katika wilaya hiyo. Kodi hii imeelekezwa kulipwa na wenye sherehe (waandaaji wa shughuli), jambo ambalo limezua mjadala mkali miongoni mwa wakazi wa wilaya hiyo. Wakazi wanahoji mantiki ya mwenye sherehe kubebeshwa mzigo wa kulipa kodi, ikizingatiwa kwamba sherehe mara nyingi si chanzo cha mapato kwa waandaaji wake.
Swali la msingi hapa ni: Je, mwenye sherehe ndiye anayefaidi kiuchumi kupitia sherehe hiyo kiasi cha kuwajibika kulipa kodi? Kama lengo la kodi ni kukusanya mapato kutokana na shughuli za kibiashara, kwanini asiwe mwenye ukumbi wa sherehe ndiye anayelipa kodi hiyo, ikizingatiwa kwamba yeye ndiye anayepata kipato moja kwa moja kutokana na kukodisha ukumbi wake kwa sherehe hizo?
Nadhani ipo haja ya kutafuta majibu na ufafanuzi zaidi kutoka kwa mamlaka husika kuhusu uhalali na mantiki ya kodi hii mpya, ama kuwapa nafasi wananchi katika kupendekeza njia mbadala ambazo zinaweza kuwa na tija zaidi kwa pande zote.
Pia unaweza kusoma Thread 'Ili ufanye harusi au sherehe Moshi lazima ulipe Kodi za Manispaa Tsh. 230,000'