Kuanzishwa Samia Scholarship ni ishara kwamba serikali inayosimamiwa na Samia kufeli katika Elimu hususan kusimamia HESLB

Kuanzishwa Samia Scholarship ni ishara kwamba serikali inayosimamiwa na Samia kufeli katika Elimu hususan kusimamia HESLB

Abraham Lincolnn

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2018
Posts
2,754
Reaction score
4,975
Kisheria bodi ya mikopo ya elimu ya juu pekee ndiyo bodi rasmi ya serikali ya kutoa mikopo, kulingana na vigezo mbalimbali vilivyowekwa. Wako vijana wanaokosa mikopo wakati wanavyo vigezo vyote, kwanini fedha hizo zielekezwe kwa wengine ilihali ni fedha ya umma na inatolewa kwa mfumo na utaratibu maalum unaozingatia mahitaji? Hii inamaanisha bodi ya mikopo ya elimu ya juu ambayo iko chini ya serikali inayosimamiwa na samia imefeli! Yaani msimamizi mkuu aliyepaswa kuisimamia bodi ya mikopo ndiye kwanza kaenda kuanzisha mikopo yake! Hii ina maanisha kwamba imekuwa vigumu kuisimamia bodi ya mikopo ya elimu ya juu.

Natambua kuna taasisi binafsi zinazotoa scholarship kwa wanafunzi wanaofanya vizuri, lakini taasisi hizo zinatumia fedha zake binafsi na nyingi huwa ni taasisi na kampuni za biashara zinazotumia fedha binafsi, mfano benki, Mo Dewji foundation n.k au kama ni taasisi za serikali mfano benki kuu, huwa kuna utaratibu maalum na kuanzia ngazi ya Masters

Je, fedha hizi za Samia zinatoka mfuko gani? Zinatoka kwenye mfuko wake binafsi? Kama sio, fedha hiyo inatoka wapi? Utaratibu ni upi ambao labda ni bora kuliko utaratibu ulioidhinishwa kwa sheria ya bunge?nini maana ya bodi ya mikopo HESLB?

Tunaomba maelezo kutoka wizara husika
 
Tasisi inatumia pesa nyingi kusomesha watu wakimaliza serikali inashindwa kuwaajiri ili iweze kuedelea kukusanya madeni kiwepesi Cjui serikali uwa ina kwama wapi. Yani umewakopesha watu wasome ili wakimaliza wakapata kazi wakulipe ila kipaumbele unaajiri watu wa diploma ambao ukuwakopesha chochote.
 
Mambo ya hovyo sana
 
Back
Top Bottom