May Day
JF-Expert Member
- May 18, 2018
- 6,311
- 9,027
Badala ya kusubiri Wachezaji wakishaacha kucheza na kupoteza umaarufu ndio Waje kama Mbalozi wa bidhaa au kampeni fulani, tufike mahali kukawa na sajili za muda ambapo Wachezaji Maarufu na wenye Mashabiki wengi Ulimwenguni kote wataweza kwenda kucheza popote pale Duniani akijiridhisha kwamba ana Mashabiki wa kutosha kwenye nchi hiyo, walau mechi moja.
Sidhani kama kuna atakayepingana na mimi kuwa Duniani kuna Ushabiki wa Vilabu na Ushabiki wa Mchezaji mmoja mmoja hata kama Mchezaji huyo anachezea timu wasiyoishabikia.
Hii ni kumaanisha ya kuwa Mchezaji ataweza kusainiwa na timu ya nchi yoyote akacheze mechi moja kwa gharama watakazokubaliana zikijumuisha na bima ya usalama wake, yaani walau mara moja kwa Mwaka Mtu kama Lewandosky anakuja kuichezea Simba mechi moja wapo ya ushindani, bila kujali atacheza vizuri au vibaya muhimu ni uwepo wake tu, baada ya hapo mkataba umeisha anarudi timu yake.