Kubadili combination A Level

Kubadili combination A Level

Hiyo sheria imeanzishwa lini.
Maana ninachojua huo ni utaratibu waliojiwekea wakuu wa shule ili kupata standard nzuri kwenye kufaulisha ila kuna watu wanabisha wanahonga watoto wao wasome PCB na mara nyingi wanafeli kama ilivyotarajiwa na shule.
Akiwa na C flat wanamzuia, akiwa na labda B flat hata kama ana Div.2 wanamkubalia.
Muongozo wa mwaka huu unasema hivyo

TAMISEMI walitoa taarifa hio
 
kama shule aliyopangiwa kuna combi anayotaka akifika anabadili tu wakat wa usajil wa acsee atasajiliwa Kwa comb aliyohamia. Necta wana vigezo vyao tofauti na hivyo vya tamisemi. Labda walimu wagome kumsaidia ila inawezekana kabisa
 
Una credits za kusoma PCB?

Akili yako inajiweza? Maana PCB, Form six si mchezo hata kidogo. Kama O level uliambulia D au C katika masomo yako, basi iache tu.

Pambana na HKL ambayo bila shaka ulipasua vema.

Anyway, kama shule ina PCB wahi mapema ukaombe wakubadilishie combination.

Kama haina, itakupasa sasa uhame shule ama uende binafsi ama uombe uhamisho kwenye shule yenye PCB.

Kila la kheri Daktari mtarajiwa. Karibu tulisogeze.
Nilisema Jana ahsante kunisemea Tena mwanangu akipata C ktk masomo yake ya PCB hataenda tena,atasoma kombe za H Kunani hukoo ..mziki wa PCB Sio mchezo
 
Tuanzie kwanza ana ufaulu gani huyo mwanao, pili alichagua combinations zipi kwenye mtiririko. Yani PCB ilikuwa ya ngapi na HKL ilikuwa ya ngapi. Pia tujue ana ufaulu gani kwenye hayo masomo matatu ya PCB.

Baada ya hapo utalinganisha na shule aliyosoma ufaulu wao ukoje, kama alisoma shule nzuri na ana ufaulu wa kawaida asiende PCB atazunguka na kurudi diploma. Kama shule ufaulu wa kawaida alijipambania kwa uwezo binafsi, anaweza pambana kwa nguvu kubwa A level na comb. hiyo.

HKL sio ya kusoma kama hana nia nayo, akishindwa options zote bora aende diploma, nusu ya nguvu ya kusoma PCB anaiweka uko anatoka na GPA ya 3.5+ na kwenda Degree kwa kuchelewa mwaka mmoja ila kwa uhakika.
T14 Armata , nisaidie tena. Alichagua CBG akachaguliwa HGL. Shule anayokwenda haina CBG. Acha PCB, kama akitaka kubadili kusoma combination nyingine process ikoje?
 
Sijui huyo pia ni wa kike.

Shule nyingi za serikali huwa hazijai idadi ileile ya waliopangiwa. Kuna wanaopangiwa A level ila wakaenda Diploma na kuna wanaoenda private schools hivyo kunakuwa na nafasi chache ambazo mkuu wa shule hawezi iambia wizara kwamba hawajaja, huwa anazijaza mwisho wa kuripoti ukifika Hivyo 'wanauza' zile nafasi, shule ikiwa nzuri enzi zetu 2017-2019 walihamia kwa laki 6 hivi, 2021 kuna mmoja mzee wake alikataa kutoa laki 6. Utaangalia integrity yako inakuruhusu ama la. Kumuhamisha bilabila utaambiwa nafasi hamna.

Kwa sisi walikuwa wanaripoti shule kwanza, then ndio aende yenye CBG. Akiwa hata na C flat na Div.2 ya kama 18 hivi anapokelewa vizuri. Preferably Moshi, kule shule nyingi za A level alafu jamii yao sio maskini kivile (ingawa selection ya A level inachanganya jamii kiasi) so kuna gaps kadhaa za walioenda private, na ni jamii ya hela as you know hawawezi kataa.
T14 Armata , nisaidie tena. Alichagua CBG akachaguliwa HGL. Shule anayokwenda haina CBG. Acha PCB, kama akitaka kubadili kusoma combination nyingine process ikoje?
 
Back
Top Bottom