tafsiri ya msichana chini ya miaka 18 mwenye mtoto maana yake ni mtoto ana mtoto, hivyo kuwa chini ya miaka 18 na ameshazaa hakumwondolei hali ya kuwa mtoto kisheria. msimamo wa sheria za tz ni kwamba ukifanya mapenzi na binti chini ya miaka 18 ambaye si mkeo, hata kama amekubali/amehiari haujamlazimisha hiyo ni statutory rape, yaani rape inayotafsiriwa na sheria na adhabu yake ni sawa tu na wabakaji wale wa vichakani wanaobaka mwanamke yeyote.
kinachoangaliwa kwenye kosa la rape ni je? msichana yuko chini ya miaka 18 au juu ya miaka hiyo? je?alihiari au amelazimishwa kama yuko juu ya 18? na je, penetration hata kama ni kidogo tu imetokea?....nikisema penetration ni kwamba, ili kuprove rape there must be penetration however slight, yaani hata kichwa cha uume kikiingia walau kasentimita kamoja tu maadamu ulishaanza kuingia/kupenye kwenye njia ile tayari kosa limetendeka hata kama mbakaji hajaendelea kubaka labda amekurupushwa amezidiwa nguvu n.k.
vilevile tunaposema "msichana chini ya 18 kama si mkeo" tunasema hivi kwasababu kisheria tz msichana mwenye miaka chini ya 18 lakini si chini zaidi ya 15 anaweza kuolewa ila kwa ridhaa ya wazazi/walezi wake. vilevile mazingira mengine msichana mwenye umri wa 14 anaweza kuolewa ila si kwa ridhaa yake wala ya wazazi bali kwa uamuzi wa mahakama pale suala hilo likipelekwa mahakamani na makama ikaona kuna umuhimu msichana huyo aolewe, inaweza ikawa hivyo.
kupata kitabu bora kilichoongelea haya yote kwa undani kabisa, pamoja na sheria yote ya ndoa tena kwa kiswahili fasaha, bofya hapa
SHERIA KWA KISWAHILI