hata bandiko lako hili pia ungeandika tu kwa kingereza kama mabandiko yako mengine ungeeleweka tuSababu ni kutaka ujumbe uwafikie watu wengi zaidi. Upo hapo?
Soma mada zangu zikizobandikwa kwa kiingereza ujifunze misamiati na uandishi bora kwa lugha hiyo
all those who pretend to know english are uneducatedKuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya kuelimika na kujua kiingereza hapa nchini kwetu. Kwasabb lugha yetu ya kufundishia ni kiingereza.
Hivyo ili mtu aweze kuipata elimu kwa kiwango kikubwa lazima aifahamu vema lugha ya kiingereza maana ndiyo iliyobeba taarifa zote zinazotakiwa na mwanafunzi. Kama mwanafunzi atakuwa hajui kiingereza ni dhahiri.kwamba kuna kitu atakikosa.
Wachina, wajapani na warusi wanatumia lugha zao kufundishia ndiyo maana wao kiingereza hakina umuhimu kwenye kuelimika.
Baba wa taifa JK alikifahamu vema kiingereza ndiyo maana aliweza kukitumia kupigania Uhuru wa nchi yetu bila bunduki. Alikuwa na ushawishi kwa wazungu.
Jiwe ndiye aliyekuwa na uelewa mdogo kuliko marais wote waliopita ktk taifa hili. Hakuna alichokuwa anakifahamu zaidi ya ubabe. Maana kwenye maisha yake alichojifunza na kukielewa vema ni ubabe wa kuswaga ng'ombe.
Ironical statementall those who pretend to know english are uneducated
Yaan anajifanya anajifanya anaponda kiswahili na pia anatumia kiswahili kuleta uzi.Tatizo kubwa la watanzania ni kujenga hoja.Hoja yake ilikuwa kwenye kuelewa kiingereza ndio elimu.Lakin hoja hiyo hiyo imekwenda kumponda JPM. Ndugu Sexless hata jina unatumia la kiingereza ,na inaonekana haujui maana yake.Sexless ,yaan hauna jinsia. Mkoloni ameleta upumbavu na ujinga mwingi Sana.Kama huyu Sexless yupo hiari hata ,kubadili rangi awe mwingereza . Nafikiri ambacho tunatakiwa kufanya watanzania,ni kubadilisha sylabus zetu kutoka kiingereza ziwe kiswshili.Na maneno mengi ya kiingereza na kitekinolojia yawe ya kiswshili.Vijana wengi Wanasoma kiingereza na Wana kalili tu.Hawaelewi vizuri.Kama huyu ,haelewi sexless hanajiita tu.Ungeandika kiingereza tukajua kama umeelimika.
Au na wewe unauelewa mdogo kama jiwe.
[emoji38][emoji38][emoji38]Kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya kuelimika na kujua kiingereza hapa nchini kwetu. Kwasabb lugha yetu ya kufundishia ni kiingereza.
Hivyo ili mtu aweze kuipata elimu kwa kiwango kikubwa lazima aifahamu vema lugha ya kiingereza maana ndiyo iliyobeba taarifa zote zinazotakiwa na mwanafunzi. Kama mwanafunzi atakuwa hajui kiingereza ni dhahiri.kwamba kuna kitu atakikosa.
Wachina, wajapani na warusi wanatumia lugha zao kufundishia ndiyo maana wao kiingereza hakina umuhimu kwenye kuelimika.
Baba wa taifa JK alikifahamu vema kiingereza ndiyo maana aliweza kukitumia kupigania Uhuru wa nchi yetu bila bunduki. Alikuwa na ushawishi kwa wazungu.
Jiwe ndiye aliyekuwa na uelewa mdogo kuliko marais wote waliopita ktk taifa hili. Hakuna alichokuwa anakifahamu zaidi ya ubabe. Maana kwenye maisha yake alichojifunza na kukielewa vema ni ubabe wa kuswaga ng'ombe.
Na mimi hoja yangu ni kwamba mtu kushindwa kuongea na kuandika vizuri kiingereza haina maana ya kwamba hakuwa akielewa masomo yake kwa hiyo lugha ya kiingereza, maana anaweza kusoma na kusikia akaelewa.Wewe kidogo umejikita kwenye mada.
Japo mada yangu imeongelea "kujua" kiingereza. Kujua kunabeba (kusoma, kuandika, kusikiliza na kuongea). Hivi vyote kwa pamoja mtu akiviweza vema ndiye tunasema anajua lugha fulani
Putin hajui kingereza nani kakudanganya au Ndio maneno ya kujifariji?Kuna muda ukitulia vizuri na kutafakari jambo kabla haujaandika haya yote utaishia kughairi kabisa. Najua unaposti kwakuwa una " time" au hata umetaka watu wabishanie hii mada yako.
Kama kweli umeitoa kwa akili zako timamu ,I swear kuna tatizo mahali, chuki zako binafsi unazimalizia kwenye paragraph ya mwisho ya maandishi yako.
Putin hajui Kiingereza, na nina uhakika hana hata muunganiko mzuri wa Sentensi za English, unamuona na yeye ni popoma kama jinsi ambavyo watu wenye IQ zakuototeza wanafanya?.
Ungesema mapema ya kwamba unamchukia Jiwe, mimi ningekubali kwakuwa ni mtazamo wako. Na hata kama ungetoa hoja zako zenye mashiko kuhusu utawala mbovu wa Jiwe ningepitia na kujua kama kulikuwa na sehemu ya kukubaliana na wewe ningekubali tu. Stop being silly, simama kama mwanaume tetea hoja zako kwa maandiko yenye mashiko. Jf should never be a damping site to store litter
Kujua kiingereza sio kipimo cha akili. It is only illogical of you to think being wise has anything to do with knowing the English Language.
Silenzio Bruno
Kiingereza hakiepukiki kwa hapa Tanzania. Tukirogwa tukaendekeza hizi porojo za uzalendo halafu tukafundishana kwa kiswahili, tutalizamisha taifa.English ilitakiwa iwe lugha ya kufundishia kwa Tanzania kwasababu mikataba mingi tunapigwa na wazungu kwa kusoma juu juu baadae tukija kushtuka kumbe kuna makubaliano hayo kwenye vifungu vya mkataba ila ukisema utaambiwa sio mzalendo.
Hata nyumba usipoijenga kwenye msingi madhubuti, lazima utarudi nyuma tu kuijenga upya. Tafsiri ya elimu hetegemeana na jamii husika. Shida inakuja kwamba siku hizi jamii zimechangamana sana sana. Si ajabu tukaishi kiunga kimoja ilihali tuna tasfiri tofauti za maana ya ELIMU. Na msingi wa mjadala huu ni tafsiri ya elimu. Sasa sijaona mtu amedadavua tafsiri ya elimu, watu wakawa wanajadili wakiwa na maana moja. Mi naona masikhara mengi tu. Ila kama ulikuwa na nia ya masikhara katika uzi wako huu, basi ni sawa. Endeleeni mi nibaki kuwa mtazamaji.Mmh! Wewe utaturudisha nyuma. Bora ubaki kuwa mtazamaji tu kwenye mjadala huu. Kama hujui hata maana ya elimu??
Ngoja niitafakari hoja yako nitakujibuNa mimi hoja yangu ni kwamba mtu kushindwa kuongea na kuandika vizuri kiingereza haina maana ya kwamba hakuwa akielewa masomo yake kwa hiyo lugha ya kiingereza, maana anaweza kusoma na kusikia akaelewa.
Na watanzania wengi hawawezi kuongea na kuandika vizuri kiingereza na miongoni mwao kuna wasomi, ndio maana nikasema kama tutasema tupime kuelimika kwa mtu kwa kigezo cha kujua kuandika na kuongea vizuri kiingereza basi watanzania wengi watakuwa hawana elimu.
Basi naomba nitoe tafsiri ya Elimu ili nipate maoni na hoja zakomaana ya ELIMU
Hahahaaa!!!! Asante sana. Unaona sasa.......na ninaamini asilimia 90 ya waliochangia huu uzi, tafsiri yao ya elimu ni nofauti kabisa na ulicho tafsiri wewe. Hivyo lazima mgongano wa mawazo utatokea. Sababu mnaongelea vitu viwili tofauti na sikushangaa nilivyoona watu wanavurumishiana matusi.Basi naomba nitoe tafsiri ya Elimu ili nipate maoni na hoja zako
ELIMU ni mchakato wa kurithisha maarifa, tabia, mila na maadili ya jamii.
Kuna mifumo aina mbili ya kurithisha maarifa.
(a) mfumo usiyo rasmi
(b) mfumo rasmi.
Kwenye mada yangu nataka tuongelee mfumo rasmi tu..
Kwa tafsiri na ufafanuzi huo. Karibu ndugu Infopaedia
Hili tatizo, kwani kichwa cha habari au kichwa cha mada kwa Kiswahili sanifu tunasemaje ? Tunasema "ANUANI". Naona unathibitisha ya kuwa hujui hata maana ya tamko "Anuani". Hili tatizo lingine tena kubwa sana.Hujaelimika kama hujui kiingereza. Na ndiyo maana umeshindwa kujibu hoja hata moja kwenye uzi wangu. Umeanza kimajungu na umemaliza kimajungu.
Nilitegemea utoe hata ufafanuzi wa unachokielewa kuhusu elimu na kuelimika.
Mwisho, kwenye mada yangu hakuna anuani
Hii siyo maana ya elimu.ELIMU ni mchakato wa kurithisha maarifa, tabia, mila na maadili ya jamii.
Uwezo wa kukabiliana na changamoto siyo tafsiri ya elimu bali ni dhima/kazi ya elimu. Kwamba aliye elimika zaidi atakuwa na uwezo mzuri zaidi wa kupambana na changamoto.Kabla sijaondoka.....kwangu mimi tafsiri ya ELIMU ni ule uwezo wa mtu au jamii fulani kupambana na mazingira yake.
Infopaedia.
Na mimi hoja yangu ni kwamba mtu kushindwa kuongea na kuandika vizuri kiingereza haina maana ya kwamba hakuwa akielewa masomo yake kwa hiyo lugha ya kiingereza, maana anaweza kusoma na kusikia akaelewa.
Na watanzania wengi hawawezi kuongea na kuandika vizuri kiingereza na miongoni mwao kuna wasomi, ndio maana nikasema kama tutasema tupime kuelimika kwa mtu kwa kigezo cha kujua kuandika na kuongea vizuri kiingereza basi watanzania wengi watakuwa hawana elimu.
Jibu haraka! Wapo wengi wanajua kingereza na wana Phd ila kwenye hayo sita hawajaweza hata moja.Nioneshe mtanza aliesoma akaelimika na kujua kingereza vizuri ambaye:
1.Anakampuni kama Alibaba na facebook.
2.Anakampuni ya kuunda injini za pikipiki kama fecon, San lg
3.Anakampuni ya kutengeneza vyombo vya nyumbani.
4.Ana kampuni ya kubadili pamba kuwa vitambaa.
5.Anakampuni ya kuzslisha kemikali mbalimbali.
6.Anakampuni ya kuzalisha vitabu na kuuzwa duniani kama pearson comp, Cambridge printing nk.
Hapo nimekutajia vitu vyepesi vyepesi vinavyohitaji elimu ndogo bado vile vizito kama Space station nk.
Ukunitajia Mtanzania mmoja basi nitakuunga mkoni kuwa TZ kuna watu wameelimika kutokana na kiingereza vinginevyo unatupotezea muda bure.
Watanzania wamehudhiria shule ila hawajaelimika, uthibitisho ni hizo point sita hapo juu, atakae weza kuzijibu basi ntamuunga mkono kuwa TZ wameelimika na kingereza ni jawabu la elimu.