Kubali au kataa lakini page ya Mange Kimambi ya instagram ndio talk of the town kwa sasa

Kubali au kataa lakini page ya Mange Kimambi ya instagram ndio talk of the town kwa sasa

IMG-20171202-WA0012.jpg
 
Naamini sote Tumeanza Mwezi Wa December wenye shamrashamshara za kipekee, nikiwa bado niko Arusha nikimalizia kazi, nimeona nirudi tena kwenu kwa salamu za December.

Kwanza nataka CHADEMA na Afisa Habari wenu mnayemheshimu Mange Kimambi mtambue kuwa watoto 1,300 wa Kibiti mnaotangaza kuwa wamepotea na kutaka kuwaaminisha Watanzania kuwa wamekufa sio kweli, Kamanda Simon Sirro anasema alitajiwa idadi hiyo kuwa ni ya watoto watoro wa shule (Absentees).

Na kwa kuwa Afisa Habari wenu anayetumiwa na Wazungu kuivuruga Tanzania na nyie kwa Unyumbu wenu mnamtukuza hajui tatizo la utoro Tanzania basi mmedandia hoja na kuanza kushutumu kuwa wameuawa na Serikali imenyamazisha vyombo vya habari visiripoti .

CHADEMA mchukueni Mange Kimambi wenu mpelekeni wilaya zote za Tanzania akajionee tatizo la utoro.

Mwambie Afisa Habari wenu anayefanya kazi kutokea Marekani kuwa kuna wilaya za Tanzania utoro umefikia hadi wanafunzi 7,000 .

Mwambieni wanaoripotiwa kuwa watoro wengine wamehama shule bila kutoa taarifa shuleni ama mamlaka za Serikali.

Mwambie wengine wanaolewa na kutoroka shule, mwambieni wengine wanaacha kusoma na kwenda kwenye uzalishaji mali na familia .

Na hii sio mara ya kwanza, ilikuwa inaokotwa miili ufukwe wa bahari Dar es Salaam. Afisa Habari wa CHADEMA Mange Kimambi akaanza kutangaza wananchi wanaua, na Viongozi wakuu wa CHADEMA wakadandia lakini mpaka leo hawajaonesha ni ndugu wa nani waliuawa kwa idadi ile.

Nataka kuwatahadharisha Watanzania dhidi ya uchochezi unaofanywa na Mange Kimambi.

Wazungu ni wataalamu sana wa kutengeneza akina Mange Kimambi ili waivuruge nchi. Wanatumia mitandao ya kijamii hivi hivi na wanashabikiwa na wananchi.

Tunayoyaona leo Libya yalianza hivi, Wazungu waliwatumia akina Mange Kimambi wakagombanisha watu na Serikali, wakawatengeneza vijana ili wamuue Ghadafi na walifanikiwa wakamuua Ghadafi.

Leo Libya imevurugika, haikaliki na wananchi wa Libya wamekuwa watumwa wanauzwa kama bidhaa. Wanadhalilishwa, na wanauawa kama kuku, Libya neema haipo tena. Libya imekuwa jehanamu .

Ni hayahaya yalifanyika Syria leo Syria ni balaa. Ni hayahaya yalifanyika Iraq. Yanayotokea Iraq wote tunayaona.

Najua Watanzania wanaakili timamu na wanauwezo wa kutambua upuuzi wa CHADEMA na Mange Kimambi wao ambaye baada ya Watanzania kuwaadhibu kwenye kura za udiwani juzi amejaribu kuhamasisha watu waanze kupambana na Serikali eti wameibiwa kura lakini amekwama.

Mimi naomba Watanzania tukiangalie Chama cha CHADEMA . Tuwaangalie viongozi wake, tuwapime wanaitakia nini nchi hii. Hivi chama Serious kinaweza kufika mahali kinamtukuza mgonjwa wa akili kama Mange Kimambi? Yaani Mwenyekiti Freeman Mbowe anamtaja kabisa kwenye hotuba yake na kumshukuru Mange Kimambi? Anayoyaposti Mange Kimambi yanafaa kwenye nchi ya wastaarabu kama Tanzania? Halafu ndio hawa wanataka wapewe nchi.

Tuonane Machame this Xmass .

Ngariba Mkuu
Arusha, Tanzania
01/12/2017

wewe una akili SANA. yaani mtu anayeiba taarifa za siri za nchi na kuziweka wazi ndiye wanayemtukuza. hawajui hata wao ikitokea wako madarakani anaweza kuiba taarifa za siri za serikali yao na kuwapa watu hatari. watu kama hawa ni wa kuwaogopa kama ukoma.
sijui kwa vijana wa sikuhizi kama mliwahi bwana mmoja alikuwa anaitwa Okelo from Uganda. huyu bwana alikuwa mastermind mzuri sana kufanya mapinduzi. alikuwa na wasifu uliotukuka. hata kuipindua serikali ya sultan wa Zanzibar akifanya kazi nzuri SANA. lkn baada ya mapinduzi akataka aendelee kuishi kisiwani Zanzibar. rais wa kwanza wa Zanzibar akamkatalia akasema hapana wewe chukua ujira wako uondoke. alimkatalia maana alijua ya kuwa huyu mtu akijiwa na yeyote na kumshawishi kuipindua serikali yetu, yeye atakubali.
ndivyo itakavyokuwa kwa huyu mwizi wa taarifa. hatashindwa kuiba taarifa toka kwenu na kupeleka kwa michepuko.
 
Sijui hata huko Instagram unaingiaje!

Na sina haja ya kuingia ilhali kuna ma sugarboys kama Salary Slip wanaoingia huko na kutuletea kinachojiri huko.

I stay put in my JF.

hivi malaria sugu yuu wapi siku hizi??
 
NB: Mods, thread inayosema page ya Mange ni talk of the town haijaandikwa leo, page ya Mange imefungwa leo hivyo vitu viwili ambavyo sijaelewa kwanini mnalazimisha kuunganisha iwe thread moja au ndio mambo ya ngazi za juu?

Wakuu,

Mange Kimambi amefunga page yake kwasababu ambazo hajaziweka wazi.

Hivyo wapenda ubuyu wote kutoka kwa Mange hatuna haja tena ya kuingia Insta. Tunafuta app yao
 
Vyuma vimekaza aisee Mzee wa frustration ata wa frustrate watu wengi sana mwaka huu na miaka ijayo
 
Mmh,kufutwa kwa account ya mange insta imenisononesha mwee,.ntakuwa naingia kwa mwezi Mara 2 sasa looh,..ntakomaa tuu na jf yangu.
 
Vijana wa Makumbusho na Ununio wamei hack ili kuona kwenye private sms ni kina Nani ndio huwa wanampelekea taarifa nyeti na kumwambia hide my Id, Sasa wale Wote team hide my ID wamekwisha

sasa kama walikuwa na uwezo huo, mbona wamemchelewesha SANA? ona umaarufu alioupata SASA. haina shida maana umaarufu kaupata toka kwa mazuzu.
 
Alikuwa anachangisha pesa za matibabu ya Lissu, kesha pata CHAKE , kaona bora afunge akaunti yake ili wasimsumbue!!!
 
Back
Top Bottom