Sultan MackJoe Khalifa
JF-Expert Member
- Nov 24, 2022
- 6,782
- 14,148
Nishakutana na mzee alafu msela.Kavaa kata K anaongea maneno ya kisela tupu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Usijidanganye,chukua hatua mapemaKikao Cha mwisho tulikubaliana kuwa uzee mwisho Chalinze
Wapo ,ila kumbuka hawaweze kuaminika baadhi ya maeneoNishakutana na mzee alafu msela.Kavaa kata K anaongea maneno ya kisela tupu.
KawajibikeHuu uzi ngoja niupige lamination nikifa huo umri utakuwa guideline, mda huu wacha niende kwa mshangazi wangu...
Nawajibika kuwajibika ni amri mkuu haipingwiKawajibike
Nauliza tu kwanini watu wazima wale walio kwenye 50+ huwa wanavaa maguo mapana kupitiliza? Hivi kwani kuvaa nguo inayo ku fit isiyobana sana kuna shida gani aisee?Salaam jamiiforum
Hii ni ijumaa,ni weekend ndogo kwa baadhi ya wafanyakazi wavivu na hata wanafunzi,mtu anajikuta tu haendi kazini bila sababu za msingi.kwa leo hata Mimi ni mmoja wapo
Leo tuliangalie suala la umri na kukumbushana mambo kadhaa,ili kutambua wapi tumetoka ,tulipo na hata tunapoenda,inasaidia kulinda heshima na kukubalika kwenye jamii zinazotuzunguka.
Hakuna umri maalumu kuonesha unazeeka bali physical appearance (muonekano wako) unaweza kuonesha.umesoma kilomita nyingi.
Si ajabu kuona mwenye miaka 45 anaonekana Mzee kuliko mwenye miaka 50 _53 hii inatokana na muonekano.
Unene kupitiliza,mvi kuwahi kutoka ,kazi ngumu ,lakini mitindo mbalimbali ya maisha yenye kututofautisha mtu baina ya mtu.
Chukua hatua hizi ili usionekane kubwa jinga na usiyekua
1.Chagua kazi za kufanya
Kuna msemo unasema Kazi na umri,kuna kazi (haswa vibarua) huenda zamani ulikuwa unazimudu lakini kulingana umri kusogea zikaonesha kukushinda nguvu,angalia namna ya kufanya.
2.Punguza ugomvi na maamuzi ya kupigana.
Wakati ukuta inawezekana ulikuwa bondia mzuri mtaani kwenu na unaogopeka lakini tambua kadri miaka inavyosogea ,nguvu hupungua ,na vijana nao wamekua,usilete dharau eti mtu alizaliwa unamuona mara akiwa mchanga ulimbeba,utakuja kuaibika au kupata kilema cha ukubwani.
3.Punguza kutongoza ovyo.
Unapokuwa mtu wa totoz sana baada ya umri kukutupa mkono ni dhahiri unajitengenezea aibu tu,kushare mpenzi na vijana wadogo.
Labda nikwambia kitu msomaji, msichana ni mtu anayevutiwa Sana na mtu wanayelingana umri,waliozaliwa era moja.kwako atakupendea pesa tu,hata kama unamkuna na kumfikisha kileleni,bado nature ipo pale pale.hapa ndipo utakaposhare mpenzi na mwanao.
4.Badilisha mtindo wa mavazi
Penda kuvaa mashati yasiyokuwa na maandishi yeyote na yenye kola, pamoja na kupunguza vazi la jeans hata kama unazikubali,
kama ni mpenzi wa kapelo vaa ambayo haina logo au machata ikiwa haina maandishi itapendeza zaidi.lakini kama hakuna ulazima wa kuvaa cheni na viurembo mikononi acha.saa inatosha.
5.Jenga utaratibu wa kuhudhuria misiba na dharula zinazojitokeza,shirikiana na majirani,fanya unayoweza Kwa kiasi huwezi kufurahisha kila mtu.
6.Usitumie umri wako vibaya.
Acha kutuma tuma,mara umemuona mtoto wa mtu,ushakamata na kumuagiza sijui kutuma,punguza utakuja ujibiwe vibaya watoto wenyewe hawaeleweki.
7.Punguza ujuaji
Kuzaliwa miaka mingi siyo kufahamu kila kitu,vijana wa sasa hawadanganyiki kihivyo,kuna Google,kuna apps kibao vijana wanapata madini mengi tu, jamiiforum ndiyo hii kuna watu hawajajiunga lakini wasoma Sana tu
Hivyo usikae vijiweni na kuanza kuonesha unajua kila kitu utajiaibisha na kuaibisha familia yako
8.Punguza ushauri
Kuna watu huomba ushauri wakiwa na majibu tayari,hata hivyo tumia busara kutoa majibu , yasiwe yenye kuumiza mpe mtu moyo,usimkatishe tamaa ikiwezekana muongopee ili kumnusuru ,hebu fikiria mtu anakuomba ushauri ili akaanzishe ugomvi Kwa mtu anayemchukulia mume au mke.
Jitahidi kumjibu vizuri na kumuepusha na hatari,kifo na hata jela.
9.Mpende na kumtunza mkeo.
Aisee mwanamke hazai wala kuishi na mwanaume mpumbavu,hawa watu wanauelewa mpana na wakipenda wamependa,hivyo kuzeeka pamoja ni dalili njema mno,ni wakati wa kufurahia matunda mliyotengeneza pamoja ,watoto na mali zenu hata kama mna kibanda cha vyumba viwili na baiskeli ni vyenu hivyo vifuraieni pamoja,kumbuka hakuna Jambo linaumiza kama kuachana ukubwani.
10.Fanya ibada ,fanya mazoezi.punguza vilevi
Kadri umri unavyosogea ndivyo seli za mwili nazo hupungua,viungo vyote hupungua nguvu,kukojoa kila mara,kutoka jasho haraka hivyo waweza punguza sigara au pombe,
Lakini pia fanya mazoezi ya wastani ili kuweka viungo sawa,
Fanya ibada,mrudie muumba wako pia ni mfano mzuri Kwa watoto na wajukuu wako.
Acha kujichetua kutafuta engagement Kwa vitu vyenye kukudhalilisha kama huyo hapo pichani.
NB: haya maneno siyo Sheria,chukua yanayokufaa