Montserrat
JF-Expert Member
- Sep 9, 2011
- 10,938
- 14,745
Kuna hili limetokea, gari dogo baada ya kusimamishwa na traffic likaoneka lina deni. Kuagalia vizuri fine(madeni) zote zimeandikiwa mkoa wa Dodoma ikiwa gari dogo halijawahi kufika Dodoma, lipo Morogoro.
Makosa hayo ni kuzidisha abiria, maana yake ilitumika kukusanya maokoto.
Wataalam naomba kujua hapa ni nini kimetokea maana nashindwa kuelewa.
Nilichowaza pengine yawezekana traffic officer alimistaken namba ya gari. Lakini kwanini fine imejirudia mara mbili na mkoa ule ule.
Au pengine kuna raia ambaye sio mwema anakopi ya plate namba na anatumia kwa maslahi yake binafsi.
Je, kuna utaratibu wa hizi fine kufutwa endapo nikithibitisha kuwa gari huko haijawahi kufika?..
Nchi isingekuwa na lundo la Polisi wapumbavu, badala ya kukupiga fine wangeshikilia Gari lako, na kuanza uchunguzi kubaini kama kuna plate number mbili zikitumia namba moja.
You should also investigate this, because the car in Dodoma could be used in criminal acts, halafu unakamatwa wewe.
Polisi Tz rubbish