Kubenea na siasa za Kyela

Status
Not open for further replies.
jamaa mwenyewe si anagombea MAFIA?

Mweh! anazo pesa za Kampeni lakini? lazima nae atachokonolewa aliko pata pesa za kampeni si unajua "Muoshwa huoshwa" we subili
 
Mtanzania/Mwakalinga

Asante mkuu kwa maelezo yako ijapokuwa Kubenea aligusa gusa ila kumbe kuna ka ukweli tatizo nilionalo Kubenea ametia chumvi.

Nina kaswali naomba nikuulize, KWA NINI HUKUMUONA/MUULIZA DR. MWAKEYEMBE KAMA ANAGOMBEA AU LA? Asante sana na heshima mbele
 

Field80,

Ni wapambe gani hao wa Mwakalinga waliokuwa wanapotosha habari?

Hapa kuna kundi lililokuwa limeandaliwa kwa makusudi kujifanya ni wapambe wa Mwakalinga wakati walikuwa wanampinga Mwakalinga.

Ndio watu hao hao waliposikia Mwakalinga anaondoka Dar J3 wakakimbilia JF kuandika Mwakalinga ameingia Kyela wakati safari ya Mwakalinga ilikuwa kuelekea Arusha. Ni hao hao pia ambao walipoambiwa Mwakalinga anaondoka kurudi London, wakakimbilia JF kusema wametoka kumsindikiza airport bahati kwao wakafanya makosa kwenye taarifa zao ambayo yalilingana na kile ambacho Mwakalinga aliwaambia. Kwa mfano mtu anayekufahamu anakuuliza unaondoka saa ngapi ili tuonane airport. Kwasababu umemshutukia na hutaki kuonana naye, unamdanganya na kumwambia saa saba na nusu wakati wewe unaondoka saa sita. Anakimbilia JF kuandika unaondoka saa saba na nusu na ndege A na kufika London saa fulani. Ratiba inakuwa sio sahihi lakini inalingana na ulivyomwambia, hapo unapata confirmation 100% kwamba ni nani alikuwa anavujisha hizo habari.

Watu hao walipogundua wameshutukiwa, wamepotea hata JF na labda wamekuja kwa majina tofauti.
 
nakumbuka vizuri sana INVISIBLE aliwahi kutoa taarifa ambazo mwisho wa siku zilipingana na kilichofanyika/uloichokifanya!wewe unajua......!unataka sema gani sasa kwa hili?????
 

Selous,

Unaenda kumwambia mpinzani wako juu ya mipango yako? Hizo sio siasa ndugu yangu. Hata kwenye change management wamesema ukienda kutaka suluhu na mtu ambaye unajua kabisa haweza kubadilika unakuwa naive. Tumia huo muda kuwabadili watu wa kati ambao wanaweza kubadilika na kukuunga mkono.

Hata Obama alivyotaka kugombea hakwenda kuomba ushauri kwa mama Clinton, alienda kwa watu wengine ambao kwa uchunguzi wake alijua hawagombea au hawana nafasi ya kugombea.

Kwa siasa za Tanzania za ubabe na hasira, ukipigwa ngumi huko, kweli utamlaumu mtu? Hata Mwakipesile ni mdau mkubwa wa siasa za Kyela lakini hatukumwona mpaka baada ya kuwa na uhakika wa kiasi kikubwa kwamba hagombei.
 
jamani hivi kyela kuna nini?
mbona kuna majimbo mengi sana ya uchaguzi hayaongelewi?
kila kukicha ni kyela, mwakipesile na mwakalinga
kyela kuna mwakyembe mwenyekiti wa tume iliyomwondoa EDWARD LOWASA.LOWASA NI TAJIRI MKUBWA. RAFIKI WA ROSTAM Na KIKWETE (RAIS).bado una swali?
 
nakumbuka vizuri sana INVISIBLE aliwahi kutoa taarifa ambazo mwisho wa siku zilipingana na kilichofanyika/uloichokifanya!wewe unajua......!unataka sema gani sasa kwa hili?????
Geoff,

Nakumbuka na nakubaliana na wewe. Invisible pamoja na FMES walitoa taarifa fulani kwa nia njema ili kunilinda na kupunguza mashambulizi hata kama kile walichoandika hakikutoka kwangu moja kwa moja. Nina uhakika waliandika kwa nia njema kabisa.

Ninachokisema ni ile kwamba wameongea na mimi na nimekanusha kwamba sina mpango kabisa wa kugombea. Siwalaumu kwasababu walitoa kwa nia njema na kulikuwa na sababu za kufanya hivyo hata kama mimi kama Mwakalinga sikumwambia mtu yeyote kwamba nakanusha sina mpango wa kugombea.

Najua wote wako hapa na mnaweza kuwauliza kama katika mazungumzo yangu na wao nilikanusha kwamba sina mpango kabisa wa kugombea Kyela. In fact naamini walikuwa wanafahamu safari yangu kabla hata ya kuondoka UK kwamba ilikuwa ni pamoja na kwenda kuonana na wapiga kura Kyela. Nilipoongea nao nilipokuwa Ngorongoro, tuliongelea zaidi juu ya ile taarifa ya kwamba niko Kyela na nimeanza kampeni kinyume na sheria.

Mimi wakati huo sikuwa na uwezo wa kusoma JF kwahiyo sikujua kulikuwa kumewaka moto kiasi gani. Naamini Invisible na FMES walitumia busara yao kuamua watoe taarifa kwa namna gani. Ila leo kwa mara ya kwanza nakuthibitishia kwa asilimia 100, sikukanusha, si kwa invisible wala FMES nia yangu ya kugombea Kyela.

Nilipokuja JF na kugundua tuhuma hizo kwamba wiki mbili nilisema sigombei na ghafla nagombea, niliamua kukaa kimya ili kutokuwaingiza motoni zaidi Invisible na FMES ambao naamini walitumia nguvu zao kubwa sana kunitetea na kunilinda hata kwa yale ambayo hawakuwa na uhakika.

Sasa moto umezimika ni vizuri kuweka record wazi na ukweli ndio huo na mnaweza kuwauliza wahusika.

Na wewe Geoff, unakumbusha hata yaliyopita?
 
nilikuwa naitest R.A.M yangu!kumbe bado iko safi😀😱

basi bwana-mkubwa mimi kama GEOFF nimeridhika na maelezo yako!nakutakia kila la heri katika safari yako!.....JAH-GUIDE!

SHAME-ON-KUBENEA
 
Acheni kumsakama mtu kwa personal interest leteni habari kuwa wapi kavunja miiko ya utoaji habari ktk kuidurusu na kuiwakilisha kwa hadhira. Matusi na dharau kama Makamba haisaidii zaidi ya kuwajua kuwa nyie ni watu wa aina gani katika jamii. Jamii bora na yenye mwamko chanya wa maendeleo inabishana kwa ujenzi bora wa fikra za hoja na sio majibu ya mkato na ya kukata tamaa. Kwa hayo utawadanganya watu kwa muda likija kujulikana unaumbuka. Leteni hoja
 
Kuna kikundi kilikuwepo hapa kwa masrahi ya Mwakalinga naweza sema sasa hivi kimepotea kabisa
Fidel80,

Sasa jiulize mwenyewe kwanini wapotee ghafla? Huko nyuma niliwahi kuandika kwamba waliyoandika akina Sikonge, FMES na Invisible nakubaliana nayo kwamba yalikuwa na lengo la kunitetea hata pale walipoteleza na kuandika tofauti.

Hayo makundi mengine kulikuwa na mamluki wengi tu. Huenda kulikuwa na waliokuwa wananiunga mkono na wengine ambao walikuwa wananipinga huku wakijifanya wananiunga mkono.

Ilichukua muda mrefu kujua nani alitoa taarifa ya kwamba mimi nimefika Kyela wakati nilikuwa Arusha? Nilionywa juu ya usalama kutokana na siasa za Kyela za sasa, hivyo niliamua safari yangu kuwa siri. Kuna ndugu wachache sana wa karibu ndio walikuwa wanajua nilikuwa naenda wapi kwa siku husika. Sasa nilipopigiwa simu kwamba kuna mtu kaandika JF kwamba niko Kyela, ilibidi kuanza kufuatilia maongezi yote na watu mbalimbali.

Bahati mbaya kwake mtu huyo huyo akaja kufanya kosa la kwamba amenisindikiza airport siku naondoka na ndio nikapata uhakika habari hizo zilikuwa zinatoka wapi. Mzee mwenyewe nilikuwa namheshimu pamoja na kwamba nilijua ni mpambe wa upande mwingine. Ni katika hao walionifuata London kunishauri nisigombee. Nilikubali kuendelea kuwa na mawasiliano naye kama mwana Kyela na niliongea naye nikiwa TZ. Kumbe mwenzangu alikuwa na lengo tofauti.

Toka siku nilipogundua niliapa kutuwasiliana naye tena mpaka baada ya uchaguzi. Hata yeye anajua nimemshutukia, nafikiri hata JF kabadili jina.

Uzuri wa kujitokeza mapema, unagundua marafiki na maadui na kuachana nao mapema wale ambao wamepandikizwa. Ingelikuwa ni dkika za majeruhi, unajikutwa unafungwa goli na beki wako uliyekuwa unamtegemea. Siasa za Afrika ni ngumu sana maana zinaongozana na njaa na kama ninavyosema siku zote mwenye njaa hawezi kuwa na mawazo huru.
 
Unajua Mwakalinga mbona kile kikundi ambacho kilikuwa kina jinadi kuwa kimeahidiwa laptop mbona hukukanusha na wala hukuwakataa kama ndo wapiga debe wako sasa hawa ndo walio chafua hali ya hewa.
 
kazi kwelikweli. TZ hakuna asiye fisadi ni opportunity tu za kufisadi zinakuwa hazijakufikia.!!!!!!!!
kubenea mhhhh
 

Duh, we ndo umenichekesha
We hulijuhi lile liMwakyembe limejaa MA BP kibao,angemwambia nini?Mwakyembe angepiga simu hapohapo polisi kwamba Mwakalinga alikwenda kumchoma kisu,Jamaa ni mkorofi sana
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…