Kubenea na siasa za Kyela

Status
Not open for further replies.

Mhh timu Mwakalinga wanachukua play book toka kwa mfadhili wao mkuu - Lowassa.

Hawa watu wakipewa nafasi tena, jehanamu itakuja kabla ya wakati wake. MUNGU azidi kumlinda mpiganaji Mwakyembe toka kwa mafisadi na watu wenye visasi kama hawa.
 
Mkulima Version yako ya kwanza umesema

......hapendwi mtu hapa.......na hiyo sio tabia yangu......ukinisoma tangu mwanzo maoni yangu yalikuwa wazi......kumpongeza Mtanzania (but with exceptions).........kama kubenea akichemsha atapewa vipande vyake.....(of which Ndg Mtanzania alishaweka wazi kilichojiri)......kilichonishtua ni arrogance na immaturity shown.......na ninashtuka zaidi......ninavyoona hiyo hali inashabikiwa........

....anza hata sasa hivi kunichafua mimi "Ogah".....KAMWE sitakuja kukumwagia Tindikali.........au cha moto zaidi yake........


na version yako ya pili.......

.....ni kweli vijana wa dala dala barabarani ni wasumbufu sana/wajeuri/wanatukana matusi and things like that..........Marehemu Mh Ukiwaona Ditopile Mzuzuri........aliua hivi hivi......baada ya gari lake kugongwa......sasa hivi vitendo.......ni vya kuvishabikia jamani.......!!

..........Ni mara ngapi tumeona waandishi wakiomba radhi wazi wazi kwa makosa waliyofanya?..........ushabiki mwingine bana.........
 
mimi nilikutetea kiasi cha kufungiwa wiki moja hata pole hukunipa.

Wewe ulifungiwa kwa sababu ya kutoa lugha za matusi huku ukitishia watu kuwa utawapungia majini ya mafia whatever that means (kutumia muda mwingi madrassa kumeharibu kila kitu kichwani mwako).
 

- Mhhhhh! Mkuu wangu heshima mbele sana, Kubenea ni ndugu yangu sana sasa bado najaribu kumtafuta toka jana ili aje hapa aweke ukweli unapotakiwa, so far sijamuhukumu anybody, isipokuwa nimesema kwamba iwapo Kubenea atashindwa kujitokeza atakuwa amejiangusha sana, bado sijafikia hatua ya kuamini hivyo kwamba ameandika majungu asiyo na uhakika nayo!

- Mimi ni bin-adam huru na huwa sihitaji kusemewa na anybody kuhusu msimamo wangu on any ishus, huo uliousema hapo juu sio msimamo wangu on the conclusion ya hii article, ninashukuru sana kwamba jina langu linatajwa sana kwenye hii topic lakini please msimamo wangu nitausema mwenyewe!

- Kama ambavyo ninasubiri time itakapofika, niamue nani anafaa kutuwakilisha huko Kyela, kati ya wagombea watakaojitokeza bado tunasubiri wengine, otherwise tunaendelea kusubiri Mkulu Kubenea aje hapa, unajua mwisho wa mwaka huu na Kristmats, watu wako kwenye pilika pilika tuwape nafasi kwanza!

Respect.


FMEs!
 
FMES,

Labda umeshindwa kuelewa nilichoamaanisha. Maneno yako niliyoyatumia ni hayo ya big time! Sikuwa na maana kwamba unasema Kubenea amefulia big time.

Maneno ya Kubenea kafulia ni ya kwangu na ndio nikaongezea na msemo wako wa big time!

Kama ulielewa tofauti samahani sana, sikuwa na maana hiyo.

Nimesoma ujumbe wako wa leo na hujasema popote kwamba Kubenea kafulia, ningelikuwa nimesema hivyo ungelikuwa ni uzushi kwa upande wangu.

Nilitaka kulitumia hilo neno ambalo kwa kawaida hapa JF naona unapenda sana kulitumia la big time! kumbe nikaishia kulikoroga. Samahani kama kwa aina yoyote Kubenea ataona umemsema hovyo.
 

- Anyways, ninaomba kwenda ndani zaidi na this article, ningependa sana kuona Kubenea, anakuja hapa na kutoa maelezo zaidi katika hizi sehemu nilizoziwekea alama nyekundu,

- Kwa mfano sio siri kwamba Mwakyembe, in one way or another alikuwa anatekeleza kazi ya Muungwana katika kumtwanga Lowassa, sasa iweje tena amtumie Mwakipesile kuwasumbua Mwandosya na Mwakyembe?

- Sasa ni vyema Kubenea akaja kutolea maelezo hizi habari zenye wekundu, in the meantime bado tunaendelea na juhudi za kumtafuta, maana alisema mwenyewe kwamba Mwanahalisi ni upanga kwa upanga, je ni theory for the truth au majungu?

Respect.


FMEs!
 

- Ahsante mkuu, tuendelee kukata ishus na yamekwisha na huwa siangalii nyuma tena.

Respect.


FMEs!
 
FMES,

Kwenye hiyo habari Kubenea ana mengi tu ya kujibu. Inaelekea hata huyo Matai wanayesema alisema anajua kuwa ni kweli kwamba Mwakalinga alikuwa anatoa pesa mpaka laki moja anakataa, anasema hajawahi kuongea na mwandishi yeyote wa Mwanahalisi. Kwasasa hili tuliacha na ukweli utajulikana tu muda sio mrefu.

Hata hilo suala la kwamba Mwakipesile anashinda Kyela. Kwa taarifa nilizo nazo mimi na labda watu wa Kyela wanaweza wakathibitisha, familia ya Mwakipesile iko Kyela, hajahama kwenda nayo Mbeya. Mwakipesile anaondoka Jumatatu asubuhi kwenda Mbeya na anarudi Ijumaa usiku kurudi Kyela kwenye familia yake. Huko ni kushinda Kyela? Labda, lakini kwa maoni yangu sidhani kama huko ni kushinda Kyela. Kutoka Kyela mjini mpaka Mbeya mjini ni kama km 110. Huyu mtu angeweza hata kila siku kulala Kyela na kufanya kazi Mbeya.

Hilo la Dr. Hunter, huko nyuma jina lake liliwahi kutolewa kwa madai hayo hayo lakini CCM mkoa likarudishwa baada ya kuridhika na maelezo yake kwamba huo ndio umri wake na wao kufuatilia documents zilizokuwepo. Nafikiri kwa mwandishi wa habari angeweza kuchunguza zaidi na kuja na ushahidi kuonyesha huyo kijana kadanganya umri au la.

Mtafuteni aje atoe msimamo wake na kama amekosea awe tayari kuomba msamaha kwenye gazeti lake la wiki kesho.
 

Mkuu Solomon David.
Ushauri wa bure
Nenda Darasan kaka.Unachekesha.
Ni Lucent na sio Lucient
 
.

FMEs,
Ninakuunga mkonono kwa 100%.Kubenea ajitokeze na atuambie nini alichoandika.Huo ndiyo Uungwana.Kama aliteleza au hiyo habari imeandikwa na MWAKYEMBE mwenyewe aseme.Nimepata PM nyingi sana zinasema Kubenea ni mtu makani sana na Hiyo Taarifa imeandikwa na Mwakyembe mwenyewe.
 
MKUU kwa hiyo hukunishukuru kwa vile hunijui kwenye Real Life? kufungiwa kwangu hakukusumbua kichwa kwa vile mimi hunijui? kazi yangu hukuiona hapa?

Anyway nilisema kuhusu Laptop kwani tulikuwa kwenye kampeni kama unaingia kwenye siasa lazima ujue mbinu za siasa huwezi kuwa smart kwa siasa za Tanzania au Africa.Obama kuna mambo aliyasema lakini kiutendaji ni magumu.

suala la Laptop niliamini unaliweza kutokana na fani yako.kutoa Laptop kwa kila shule ya sekondari Kyela sio issue,kwani mimi ndio niliyesema baada ya kujiingiza kwenye timu yako.sasa ilikuwa uniulize hivi vitu tutapata wapi? na kama unataka hizo Laptop mimi naweza kukutafutia hadi 40 moja kila shule.nitafute kwenye PM kama una nia na vitu hivyo sawa.
 
Kanda2,

kampeni za namna hiyo hapana, hata kama ni Afrika.

Hatuendi kudanganya watu, tunaenda kufanya yale tunayoyaamini. Hata kama una uwezo wa kutoa laptops 40, bado ungetakiwa kujadiliana na mimi kwanza kabla ya kusema mimi nimetangaza kwamba nitatoa hizo laptops.

Sijui ya mungu, hata mimi naweza kutafuta hizo laptops lakini kwasasa sio priority na kuna mambo mengine ambayo ni muhimu zaidi.

kwa kusema mimi nimeahidi kutoa laptops bila mimi mwenyewe kusema hivyo, tayari watu wengi walishaamini mimi ni mwongo ninaposema siahidi kitu.

Ni bora umethibitisha mwenyewe kwamba mimi sikuahidi mahali popote kutoa laptops na hata sasa siahidi hilo.

Siku hizi kuna idea mpya ambayo ni bora inaitwa no pc. Ni bora hiyo kuliko hata laptops.

Pole sana kwa kufungiwa japo sijui ulifungiwa kwasababu zipi. Kuna wengi walinitetea na mbona hawakufungiwa?
 
Mhh timu Mwakalinga wanachukua play book toka kwa mfadhili wao mkuu - Lowassa.

Hawa watu wakipewa nafasi tena, jehanamu itakuja kabla ya wakati wake. MUNGU azidi kumlinda mpiganaji Mwakyembe toka kwa mafisadi na watu wenye visasi kama hawa.

Ungelikuwa na dada Mzuri ningelifahamu unataka niwe SHEMEJI yako.

Na kwa sababu nimeshaowa miaka mingi na sitaki kuwa Muislaam, basi nipishie mbali mwana wa Itimba aka Sikonge.

Kama ulikuwa unanitafuta basi utanipata. Na hivi nataka nifungiwe kwa miezi mitatu baada ya mwaka mpya (David Beckham style), nisije nikakuangukia kwa lugha za wabeba Lami na Zege.

Hao Maruhani wako wa kusema mie ni wa Lowassa, itabidi ushukuru Mungu kama utaishia kumwagiwa ACID. Ntamtafuta mkeo au girlfriend wako....... Ukishapata donge, tuone kama utakuwa unachekacheka hivi na kutuita kuwa tumekumegea mkeo kwa kutumia hela za mfadhili wetu Lowassa. Wanaume wengine bana, utafikiri wanavaa SHIMIZI.
 

wapi nilisema wewe umesema utatoa LAPTOP? niliyesema ni mimi.kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM 2005 HAKUNA kipengele cha chuo kikuu cha Dodoma ni JK aliamua kulisema yeye kama binafsi kwa vile ni jambo jema CCM ikalichukua na kulifanyia kazi.

sasa kama huhitaji Laptop mbona unalalamika kukosa vitabu vya BOOKAID INTERNATIONAL?hawa waliona WAMA wamejikita kwenye utaifa na wewe umekijikita kwenye Ukyela,wakaona uzito uko Wama.

Unasema wewe hutoi ahadi ila unatekeleza.utachaguliwa vipi bila kueleza kuwa nia yako ya kuwa mbunge ni kuwafanyia hili na lile wana Kyela?huwezi kukopi siasa za Ulaya ukapeleka Kyela.kama unasema huwezi kufanya siasa za Africa mbona unamjibu KUBENEA ambaye yuko kazini kisiasa kukuchafua wewe.ungenyamaza na kusema watu wa KYELA wakupime na utekelezaji wako.
 

Mkuu Sikonge,

...heshima mbele, sijawahi na sitajaribu kutaka kujua wewe unatokea wapi...na wala sihitaji kujua....huo utambulisho wako.......kwani haipo katika sehemu ya utashi wangu.....kutafuta kujua/ku-speculate nani ni nani na anatokea wapi.............


...........fair enough!...............you are entitled to your own opinion.......
 

Kumbe unatishwa NYAU? Nilitaka kuwa na uhakika unavyojibu ujumbe wangu kiutaniutani, unafikiria pia mie ni wa Kyela? Ndiyo maana nikataka kuweka rekodi sawa. Kufahamu mtu anatoka wapi haina maana umemfahamu.

Tuke pamoja mkuu wangu. Wote lengo letu ni moja labda tu kila mtu ana maono ya njia tofauti za kutumia. Zangu kidogo ni Radical na wengine zenu ni soft. Ingawa kusema ukweli, ili mambo yaende inabidi zote zitumike yaani kama ni POLISI, basi kuwe na POLISI mbaya (mimi) na POLISI mzuri(wewe).

NB: Jumbe mbili za mwanzo kwako nazifuta. Ntafurahi ukifuta kuanzia ule wako wa kwanza kama kweli unaamini "i'm entitled to my own opinion".

*** Wee nyanda Samwel, nenda kalale 🙂 Utapewa talaka bure. Kesho nakulima waya kwenye mtandao(Skype).
 
mkuu unajichanganya umesema hapo juu kuwa huna uwezo wa kupata Laptop halafu leo umetuma ujumbe mwingine ukisema unao uwezo wa kupata hizo Laptop lakini sio priority kwako.

kingine unaposema wewe huwa hutoa ahadi jee hutakuwa na Manifesto kwenye kampeni zako?

Sijawahi kuona siasa ambazo hazina AHADI iwe America,ulaya au Africa. Kama ajira OBAMA aliahidi kuzalisha ajira,na JK naye aliahidi hivyo hivyo. Ameanza kwa kufungua chuo kikuu cha DODOMA na miradi mingine. Mtu hupimwa kwa ahadi zake. Huwezi kufanya siasa za kufikirika.

Gordon Brown na David Cameroun wanatoa ahadi kila siku ambazo zingine hazitekelezeki ingawa wako ulaya ndio siasa. Kwa mtindo wako huo sidhani kama ubunge ni mahala pako lazima ubadilike.

Niambie mbunge gani mkweli kuanzia vyama vya upinzani hadi tawala? Wewe utakuwa malaika? Mfano utaenda kwa waziri wa miundombinu atakwambia kuwa barabara ya kyela itajengwa kwenye bajeti ya 2010/2011 wewe kama mbunge ukitoka hapo utaenda kuwaeleza wananchi wako kuwa barabara hiyo itajengwa muda ujao. Halafu wizara ghafla inabadilisha ratiba hiyo, hayo yanatokea sana.
 
Pole sana, yaani kwa kusema mie ni Mwakalinga basi kwako amekuwa Mwakalinga kweli?...Wewe kutapeliwa ni sekunde tu...!
 
Mhh...wewe ni Mwakalinga? Si ungesema mimi badala ya Mwakalinga? anyways, i might be wrong though...ila i wonder...!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…