Kubenea wa MWANAHALISI amenunuliwa na mafisadi?


Hi ni habari kubwa sana. Mimi nashawishika mpaka sasa kwa namna nimemsoma Kubenea hakuna wa kumnunua hapa Dunia ni mtu mwenye kutawaliwa na maadali fulani na sema sijui tuone.
 
Kamaudoulton kasepa na umbea wake wa ki**, hata thamani ya pesa yetu haijui!
20mil can't buy a plot in modern Kinyerezi. Mp***avu huyu.
 

Mkuu kwa mtu yeyote anayeijua CCM vizuri inatambulika kwa ULAGHAI, wengi tumeshafahamu kuwa uamuzi wowote wa CCM japo unaweza kuonekana mzuri kwa juu juu lakini ndani yake kuna hila kubwa sana na udanganyifu.

Sasa hata Mwanahalisi unaweza kudhani kuwa wanazomea sana maamuzi ya NEC ya kujifanya wanajivua magamba na kuwaacha akina RACHEL, the logic here is very simple, si kweli kwamba CCM wana nia ya dhati ya kujisafisha, na kama ingekuwa hivyo basi mwenyekiti wao nae angekuwa pengine wa kwanza kujiuzulu during that process.

CCM haina msafi hata mmoja, policy yao ni moja tu kupora mali na rasilimali za nchi kwa faida yao tu na si watanzania. So, wanachokifanya Mwanahalisi ni kuendelea kuupinga huu utawala wa kidhalimu na maamuzi yake yote kwani hawana jema hao na ndio maana kwa wenye uelewa mdogo au wasiojishughulisha kufikiri wanaweza kudhani kuwa wapambanaji wamejiunga na RACHEL.

RACHEL na CCM wote ni mafisadi tu and they all need to go ili nchi yetu iwe salama. CCM wanachotaka kuwadanganya wananchi ni kuwa ndani ya CCM kuna kundi la watu watatu tu ndio mafisadi, no no no! CCM imetengeneza mfumo wa kifisadi na ni lazima kuuondoa mfumo huu. Na kufanya hivyo ni lazima CCM iondoke.
 

Mimi binafsi siafiki wala sipingi hoja yako..........Ila naachia muda ndiyo utakaoamua kama hoja yako ni ya kweli au ni uzushi.....
 
Habari hii imekaa kizushi manake Kubenea akizitaka milioni 20 atapata hata mia lakini kwa upande mwingine kama ni kweli basi Rostam si mwepesi wa kujifunza. Nasema hivyo kwa sababu alipoona gazeti la Rai limekuwa mwiba mchungu aliamua kulinunua likakosa mvuto yakaibuka magazeti mengine kama Mwanahalisi na Raia mwema, kwahiyo kama kweli amemnunua Kubenea wataibuka waandishi wengine na wataendelea kutuhabarisha mambo muhimu ambayo yako mafichoni.

Kwa hiyo asiandike habari nyingine zaidi ya Riwaya Za Rostam na Lowasa nini maaana ya Habari sasa Kisa 20Mil kaazi kweli kweli


Sidhani kama Kubenea yupo cheep kiasi hicho........
 
Haina mashiko hii, haya ni majungu tu kwani Kubenea ni mtu makini na anajua anachokifanya!!!
 
Kama ni kweli basi money can buy anything except peoples' power!!! Lakini nina wasiwasi mkubwa na mtoa mada hivi ni mtambo wa aina gani unaouzwa mil.20 labda tupe ufafanuzi kidogo!!

Even people's power... hakuna ulizia Bariadi mashariki au monduli au Igunga... Money buys everything from nothing to dignity...

Pamojaaaaa....
 
Let wait hiyo jumatano kama habari ya porokwa itakuwemo, lisemwalo lipo

Habari ya Porokwa ndio current news hivi sasa. Kama kawaida magazeti ya dailiies huandika habaraia kwa juu na weekly kama MwanaHalisi na RaiaMwema huandaki habari hizo hizo kwa undani zaidi.

Tatizo hapa sio kupinga Ufisadi bali ni vita ya watu kugombea uraisi ndani ya CCM 2015. Kama alivyotabiri Mwalimu Nyerere kuwa Tanzania na watanzani watapata ahueni pale CCM itakapogawanyika. Na fursa ya kufanya hivyo ilijitokeza katika CCJ lakini Sitta na wenzake wakakosa ujasiri kama aliokuwa nao Mrema, Mpendazoe n.k

Laiti kama wangekuwa majasiri na kutoka CCM 2010, CCM ingegawanyika na vita ya ufisadi ingekuwa katika gia kubwa zaidi. Hivyo ni muhimu watanzania waelezwe kila kitu kuwa ujasiri wa Sitaa kupambana na ufisadi uko ataached na yeye kupata urais kwa kuwadhoofisha wapinzania wake kwa kutumia ufisadi. Mbona Sitta alifilisi CDA?
 
Jamani naona inabidi tuanze kupimana IQ tusije tukawa tunapoteza muda kumbe tuna argue na mtu aliye chizika!!!! mh. mil 20??? basi kumbe Rostam hana pesa kama tunavyo fikiri au Kubenea ana nunuliwa kirahisi namna hii??? kama ni kweli najutia viela vyangu nilivyo kuwa najitaidi kumsupport huyu jamaa ni bora ningekuwa nagonga mkaburu tuuu!!!!
 
lets wait and see,mbona haikukaa vizuri hii, mwanahalisi wana uwezo ku generate zaidi ya hizo 20 mil,ni taasisi kubwa
 

Ushageuza majungu mtaji!??
 
Kwa wale wanaosoma Biblia wanajua jinsi Yuda Iskariot alivyomsaliti Bwana Yesu kwa kupewa chochote. Huu ni msimu wa kuvuna bwana! Ni wazi sasa kwamba si kundi la Lowasa wala Sitta litaiona Ikulu 2015. Wacha Kubenea naye ajiweke pazuri kimasilahi.
 
MAFISADI HAWANA JIPYA WAMEDODA NA WAMEFULIA KISIASA..........................., bado naendelea kuamini kwamba mafisadi hawana jipya na watazidi kuchemsha na kundi lao lote na vijana wao wote wao ndio wanaopanga njama na kumuingiza madarakani kijana wao kutoka visiwani JAMAL KASSIM kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Mh Masauni(Mb) naamini hawatafanikiwa hata kidogo....nasema hata kidogo.

-wacha wamnunulia Kubenea hata JUMBO MASHINE PRINTER nini hicho kikoroboi cha milioni 20-30, ila njama wanazozipanga hazitafua dafu hata kidogo wanaplan nyingi kuliko uwezo wao wa kufikiri, wanahela nyingi hawajui wazifanyie nini, wanakundi kubwa lisilo kuwa na tija, hakuna watakalofanikiwa hao. plan wanazotumia kumuingiza JAMAL KASSIM kuwa mwenyekiti UVCCM hazitafua dafu ni bora litibuke tusubiri mwakani 2012 kuliko hizo njama zao, kikao kilichokaliwa na hao vijana wao wa mwmvulia chini ya HUSSEN BASHE BASHE wasidhani havijulikani vinajulikana na wanayoyafanya yanajulikana.

-WANAPINGO KAMA IFUATAVYO: kama LOWASA hawi rais 2015 basi kijana wao EMENUEL NCHIMBI awe rais na LOWASA kuwa WAZIRI MKUU TENA hiyo ndio hesabu yao hata hili wataula wa chuya kwa uvivu wa kuchagua, leo wamemgeuka mwanamama wao MARY CHATANDA kwa kuwa hakuweza kumsaidia demu wao BATILDA BURIAN kuwa mbunge ARUSHA MJINI sasa imekula kwao waendelee kuvurugana tu na kijana wao JAMES MILLYA mwalimu sijui shule ipi ya sekondari aendelee kutumika utadhani sio mmasai halisi.

-wanamthumu kijana wa watu bure MRISHO GAMBO bila sababu yeyote japo naye mwanzo alikuwa wao lakini hawakumpenda na baadae amejua ukweli sasa wanamuona mbaya, nchii kila aliyekataliwa na BABA W TAIFA MWALIM JULIUS KAMBARAGE NYERERE HAKUNA ATAKACHOFANYA KIKAKUBALIKA MILELE hata kama utamfanyia mtu madhali ni ww unafanya itakula kwako na hao unaowafanyia.

-LOWASA ALISHAKATALIWA NA BABA WA TAIFA watanzania wanajua hilo....................., Mzee kambarage alishawahi toa hundi ya DOLLA LAKI TANO AMBAYO LOWASA ALIHONGWA NA WAHINDI KUKIUZA KIPANDE CHA ARDHI LEO NDIO KUNA SHULE YA AGKHAN MZIZIMA PRIMARY SCHOOL, hii lilikuwa MKUTANO MKUU WA HALMASHAURI KUU 1995 watanzania hawajasahau na hawatasahau hilo. wakati huo alikuwa WAZIRI WA ARDHI NYUMBA NA MAENDELEO.

-KUBENEA ATAKULA NAO SAHANI MOJA PAMOJA NA KUNUNULIWA HUO MTAMBO na hao aliotajiwa kuwashughulikiwa haita tokea mbona wanamiliki MAGAZETI YAO YA TAZAMA linatoka kila JUMANNE NA LIMESHINDWA KUFUA DAFU, WANAMILIKI MKAKATI linatoka kila IJUMAA nalo limeshindwa kufua DAFU? NINI WANATAPA TAPA HAWA WATU? WAMEFULA.

-WAMEKULA YA MBUZI WATAOTA MAPEMBE.............................!!!!!

MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Hakuna jipya,ni majungu tu ya makundi ya wana CCM wanaotafuta huruma ili waungwe mkono kupambana na Rachel! Kubenea ni mwandishi makini. Majungu yako peleka huko CCM.
 
me bado labda ni sadikitu kwa kua kua ule usemi wa lisemwalo lipo kma halipo laja ila sio kwa kua utashi wangu umekubali.
time will tell.
kuandika habari za porokwa sio ishu, kwa sababu nia haikua kumdidimisha sita, nape mwakyembe kama maadui wa rostam bali
kuonesha nafki wao na mtazamo wao hasi kwa chama chao.
hilo la kumsapot rostam ni advantageous ya primary intention.
 
Huyu mtoa mada, inawezekana katumwa, swala la kujua kama jumaa 5 ijayo kutakuwa na habari gani inawezekana kwa sababu gazeti hilo ni la wiki na huanza kuandaliwa siku ya alhamisi ya kila mwezi. Inawezekana habari ya porokwa ipo lakini mtoa mada huyu ametumwa jaribu kufanya namna habari hiyo iondolewe kwenye gazeti. MIMI BINAFSI SIAMINI MPAMBANAJI ALIYEJITOLEA MAISHA YAKE KWA AJILI YA WALALA HOI ANAWEZA KUPOTEZA HESHIMA YAKE ALIYOJIWEKEA NCHINI KWA AJILI YA PESA. Namshauri mtoa mada huyu atambue kwamba wana JF ni watu wenye akili timamu na ni watu wenye uwezo mkubwa sana wa kuchambua pumba na mpunga.
 
Hii inanikumbusha habari za Mwanakijiji kumponda Dr. Slaa baada ya uchaguzi. Leo hii ni habari nyingine. Tusubiri kesho itakuwaje
 
Uwe unaangalia hili pia mkuu, utaumiza kichwa bureee.....(Feb - May...join dates,be careful)
Join Date : 13th April 2009
Posts : 11
Thanks 10 Thanked 5 Times in 2 Posts

Rep Power : 0

 
unajua alieandika hapa ana akili sana kimsingi alikuwa anataka mwanahalisi wasiandike habari ya Parokwa kwa kuwa anajua watu wanangoja sana toka huko kujua ukweli wa jambo hilo..............si kweli kuwa kjubenea kapewa mtambo mpya na wa kisasa na rostam na ukweli ni kuwa rostam mwenyewe magazeti yake hayana mtambo wake wenyewe....pia huu mtambo anaonunua kubenea ni mtambo amabao ni used na ameuziwa na makampuni ya IPP,na amekuwa akiulipia kwa muda sasa na kimsingi ni kuwa ni mtambo ambao ipp walikuwa wakiutumia kabla ya kufunga matambo mpya.
 
Let wait hiyo jumatano kama habari ya porokwa itakuwemo, lisemwalo lipo

Habari ya Porokwa kuwepo si kitu cha ajabu maana nayo ni habari kubwa wiki hii baada ya kumvua gamba Nape. Huyu mtoa habari ametumwa na Nape ili asiumbuke katika habari hiyo.

Kubenea tunakujua ni Mtu makini, maneno ya vikaragosi kama hawa yasikukatishe hadhma yako ya kutueleza kuhusu alichosema Porokwa kuhusiana na Nape, Sitta na Mwakyembe kuhusu CCJ.

Go ahead Kubenea. We respect you.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…