TUKUTUKU
JF-Expert Member
- Sep 14, 2010
- 11,763
- 4,041
Anafanya yeye pamoja na Ndimara Tengambwange!!kwani kazi ya kuchapisha magazeti kubenea anafanya mwenyewe?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Anafanya yeye pamoja na Ndimara Tengambwange!!kwani kazi ya kuchapisha magazeti kubenea anafanya mwenyewe?
Milioni 20? Si angelisema tu Chadema wakamchangia? Na tena Wabunge tu wachache wangelimpa.
Huu ni uwongo wa hali ya juu kuwa mitambo kama hiyo iuzwe kwa bei ya Euro 10,000/-
Kijembe ambacho mmoja wa mapacha watatu wa ufisadi, Rostam Aziz Abdulrasul, alikirusha kwa Saed Kubenea kuwa anaweza kumnunulia mtambo wa kuchapishia gazeti lake la MwanaHalisi mapema mwaka huu, kimegeuka kuwa "azma iliyotimia" baada ya mwandishi huyo machachari aliyejizolea sifa kemkem kwa ujasiri kutiwa mfukoni na sasa ni sehemu ya majeshi ya Rostam ya kumlinda na kuwasambaratisha wabaya wake!
Kubenea ambaye mwaka juzi alishambuliwa na watu "wasiojulikana" na kumwagiwa tindikali machoni karibu apofuke, kasahau yote hayo na sasa ni silaha ya kuaminika ya Rostam katika kujihami dhidi ya kampeni kali ya CCM inayoongozwa na Katibu Mwenezi Taifa Nape Nnauye ili mkuu wake mpya Rostam abakie na gamba lake.
Taarifa za ndani kwenye duru za mwanahabari huyo zinasema kijembe kile cha kumnunulia Kubenea mtambo wa kuchapishia magazeti kimefanyiwa kazi na Kubenea yuko mbioni kupata mtambo mpya wa kisasa lakini kwa sharti la kuachana na habari hasi za Rostam na Lowassa kwenye gazeti lake na kuendesha kampeni kali dhidi ya msururu wa watu aliopewa katika miaka mitatu ijayo. Baadhi ya watu hao ni JK na familia yake, "Mtoto wa Mkulima", Magufuli, Chilligati, Nape, Sitta, Anne Kilango, Ole Sendeka, Lembeli, Mwandosya, Membe, Kinana, Mwakyembe, Mkuchika, Chatanda na Kigoda. Kubenea kakubali dili hilo ambalo tayari limemwingizia zaidi ya sh. milioni 20.
Gazeti la MwanaHalisi ambalo limekuwa kwa muda mrefu msumari wa moto kwa mapacha watatu wa ufisadi kutokana na Kubenea kuamini kwamba wawili kati ya mapacha hao watatu walihusika na mpango wa kumtoa roho au kumpa kilema cha maisha, halitabeba taarifa tena za Lowassa wala Rostam ila za wabaya wao hao.
Mathalan, toleo la kesho kutwa la MwanaHalisi tayari lina taarifa ndefu ya Daniel Porokwa akiwamwagia sumu "maadui" wa RA na EL bila kujali kuwa gazeti lake lilimwandika Porokwa mwaka jana kuwa kibaraka wa Lowassa baada ya kujitoa kugombea Ubunge jimbo la Monduli. Porokwa "alizawadiwa" kazi ya Katibu Msaidizi wa CCM wa Wilaya, gari mpya aina ya NOAH, shilingi milioni 2, na ng'ombe kadhaa baada ya kujisalimisha na kukubali Lowassa amkanyage kichwani kwa mila eti ya Kimasai kama siyo ya kishirikina.
Mkuu sio kuuzika tuu,hata bure bado watu wengi hawayasomi. Jamaa mmoja aliniambia alisahau gazeti lake la HabariLeo Posta na baada ya masaa matatu aliporudi alilikuta palepale ila limewekewa kajiwe ili lisipeperuke,nilicheka sanaHomeboy
Jamaa anauza story hakuna kitu kama hicho! Ni vita wanapigana Magamba hao wanajaribu kumtumia Kubenea kama AK47. Kubenea is not that much cheap. Wanajua Magazeti yao ya Uhuru, Mzalendo, Habari leo hayauziki.
Nimejaribu kufanya utafiti pori. Mbele yangu nina faili zima la magazeti ya MwanaHALISI. Toleo la mwisho ambalo gazeti hili liliandika habari ya kumbamiza Lowassa ni tarehe 6 Aprili kwa kichwa cha habari: "Lowassa hasafishiki."
Baada ya hapo, matoleo yote 6 yaliyofuata ya MwanaHALISI yamekuwa na habari za kuwatetea kiaina kina RACHEL (Rostam Aziz, CHEnge na Lowassa), kumwandama Kikwete na kujaribu kumgombanisha Kikwete na Sekretariati ya CCM.
Angalia kama ifuatavyo matoleo haya mfululizo ya MwanaHALISI:
1.Kikwete 'jino kwa jino' na Lowassa (13 Aprili)
Habari hii ilipotoshwa makusudi kujaribu kuonesha kuwa uamuzi wa NEC wa kuwafuta kazi mafisadi ndani ya CCM ni vita kali vya madaraka kati ya Kikwete na Lowassa na si uamuzi rasmi wa CCM kama chama.
2. Dk. Slaa amweka pabaya Kikwete (20 Aprili 2011)
Habari hii iliyokuja immediately baada ya kikao cha NEC ya CCM imesema kuwa Slaa amtaja tena Kikwete katika ufisadi. Ikaongeza kuwa avuruga mkakati wa "gamba." Habari nyingine kwenye ukurasa wa mbele wa gazeti hilo ikasema kuwa: Lowassa, Rostam, Chenge bado
3. Mukama amdanganya Kikwete(27 Aprili 2011)
Habari hii ikitaka kuonesha kuwa Sekretariati ya CCM mpya iliyochukua nafasi baada ya kufukuzwa kwa mafisadi haifai.
4. Kikwete mahakamani (4 Mei 2011)
Huku habari nyingine ikisema CCM yafyata kwa mafisadi
5. Nyumba ya Kikwete yazua utata (11 Mei 2011)
Gazeti hili likiwa linaendelea kumwandama Kikwete kwa tuhuma huku likikaa kimya kuhusu kina RACHEL.
6. Kikwete ndani ya CCJ (18 Mei 2011)
Huu ni muendelezo ule ule wa mkakati wa kina RACHEL wa kuibua tuhuma dhidi ya Kikwete kupitia MwanaHALISI ili wao waweze kusalimika.
Naomba kuwasilisha...
Kama ni kweli basi money can buy anything except peoples' power!!! Lakini nina wasiwasi mkubwa na mtoa mada hivi ni mtambo wa aina gani unaouzwa mil.20 labda tupe ufafanuzi kidogo!!
kiukweli mimi bado hujanipata.......................kijembe ambacho mmoja wa mapacha watatu wa ufisadi, rostam aziz abdulrasul, alikirusha kwa saed kubenea kuwa anaweza kumnunulia mtambo wa kuchapishia gazeti lake la mwanahalisi mapema mwaka huu, kimegeuka kuwa "azma iliyotimia" baada ya mwandishi huyo machachari aliyejizolea sifa kemkem kwa ujasiri kutiwa mfukoni na sasa ni sehemu ya majeshi ya rostam ya kumlinda na kuwasambaratisha wabaya wake!
Kubenea ambaye mwaka juzi alishambuliwa na watu "wasiojulikana" na kumwagiwa tindikali machoni karibu apofuke, kasahau yote hayo na sasa ni silaha ya kuaminika ya rostam katika kujihami dhidi ya kampeni kali ya ccm inayoongozwa na katibu mwenezi taifa nape nnauye ili mkuu wake mpya rostam abakie na gamba lake.
Taarifa za ndani kwenye duru za mwanahabari huyo zinasema kijembe kile cha kumnunulia kubenea mtambo wa kuchapishia magazeti kimefanyiwa kazi na kubenea yuko mbioni kupata mtambo mpya wa kisasa lakini kwa sharti la kuachana na habari hasi za rostam na lowassa kwenye gazeti lake na kuendesha kampeni kali dhidi ya msururu wa watu aliopewa katika miaka mitatu ijayo. Baadhi ya watu hao ni jk na familia yake, "mtoto wa mkulima", magufuli, chilligati, nape, sitta, anne kilango, ole sendeka, lembeli, mwandosya, membe, kinana, mwakyembe, mkuchika, chatanda na kigoda. Kubenea kakubali dili hilo ambalo tayari limemwingizia zaidi ya sh. Milioni 20.
Gazeti la mwanahalisi ambalo limekuwa kwa muda mrefu msumari wa moto kwa mapacha watatu wa ufisadi kutokana na kubenea kuamini kwamba wawili kati ya mapacha hao watatu walihusika na mpango wa kumtoa roho au kumpa kilema cha maisha, halitabeba taarifa tena za lowassa wala rostam ila za wabaya wao hao.
Mathalan, toleo la kesho kutwa la mwanahalisi tayari lina taarifa ndefu ya daniel porokwa akiwamwagia sumu "maadui" wa ra na el bila kujali kuwa gazeti lake lilimwandika porokwa mwaka jana kuwa kibaraka wa lowassa baada ya kujitoa kugombea ubunge jimbo la monduli. Porokwa "alizawadiwa" kazi ya katibu msaidizi wa ccm wa wilaya, gari mpya aina ya noah, shilingi milioni 2, na ng'ombe kadhaa baada ya kujisalimisha na kukubali lowassa amkanyage kichwani kwa mila eti ya kimasai kama siyo ya kishirikina.
Kuna mambo mawili makubwa kuhusiana na RACHEL ambayo nimekuwa nikiyafanyia kazi kwa wiki nzima sasa ila bado sijafikia conclusion. Mojawapo ni hili la KUBENEA kununuliwa na RACHEL ili awasadie kuwachapa wapinzani wao wakuu kisiasa, wakiwemo SAMWEL SITTA na HARRISON MWAKYEMBE. Inasemekana kuwa kazi hii inafanywa kwa ufasaha sana na MWANAHALISI, na hata gazeti lao litakalokuwa mitaani kesho linawapiga tena SITTA na MWAKYEMBE, baada ya hoja hii ya kipuuzi ya CCJ kuongezewa nguvu na DANIEL PAROKWA mwishoni mwa wiki. Kwa upande wa PAROKWA ni wazi kuwa ametumwa na RACHEL. Tutathibitisha baadaye alilipwa kiasi gani. Suala la pili ambalo nalifanyia kazi ni taarifa kuwa MPENDAZOE naye amekatiwa kitu kidogo na RACHEL ili zimsadie kwenye kesi yake ya Ubunge. Taarifa hizi zinadai kuwa baada ya MPENDAZOE kumtaja NAPE kama mmoja wa waanzilishi wa CCJ kule MBAMBA-BAY, RACHEL wakamvaa na kumtaka akamilishe kazi kwa kuwataja pia SITTA na MWAKYEMBE. Alifanya hivyo akiwa NJOMBE, baada ya kupokea kitita chake kutoka kwa jamaa mmoja mwenye asili ya Kisomali aliyetumwa huko na RACHEL. Kama nilivyodokeza hapo juu, haya bado nayafanyia uchunguzi wa kina, na nitayaanika rasmi hapa JF nikishakusanya data zote na kujiridhisha.