Nilikuwa nabet sana Football miaka 2 iliyopita. Nilikuwa nakula na kuliwa hivyo Ngoma ilikuwa almost draw. Mwezi wa 3 mwaka huu kuna mdau aliweka bandiko humu la kujifunza kubet basketball akisema ni rahisi kushinda kuliko Football. Nikajifunza ndani ya masaa mawili nikawa nimeshajua jinsi ya kubet basketball. Nikajisajili Sportpesa nikaacha kubet Football. Ushuhuda wangu ni kwamba NAJUTA kupoteza muda kubet Football. Hakuna siku ambayo sijala Basketball. Juzi tu Jumamosi kwenye ligi ya Basketball Australia nimekula 2,464,640. Jana Jumapili kwenye ligi ya Under 18 World Cup nimekula jumla 745,500. Mikeka yangu timu nyingi ni 4, zaidi ya hapo ni timu 3 au 2 au 1 then naweka kuanzia 50,000 na kuendelea. Mkeka mmoja juzi Jumamosi niliweka timu 4 nikaweka 100,000,nikala 1,974,000. Leo hakuna mechi yoyote ya Basketball. Kwa hiyo kwa anayetaka kula betting namsihi abet Basketball. Kumbuka kwenye Basketball hakunaga Draw,ni lazima mtu afungwe,hivyo Research yako makini ya Head to Head ndio ushindi kwako