Kubeti: Huu Ndio mrejesho yangu niingie kwenye mchezo huu miezi 4 ilopita!!

Kubeti: Huu Ndio mrejesho yangu niingie kwenye mchezo huu miezi 4 ilopita!!

me kubet siwezi kuacha kwa maana life is so sweet. umepewa utashi na maono sasa kwanini usimeditate na kutengeneza pesa kwa betting. life is so fun.

Mkuu embu eleza vizuri hapa kwenye maono, itashi n ku medidate
 
Nimeanza kubeti mwezi March wakat Rafik yangu alipokuja kunitembelea Ghetto na kunionesha sample ya mikeka anayokula. Nikatamani sana!!

Mwanzo nilikua muoga sana, nikawa naweka stake ya sh. 500 tu. Nikila saana nakula 900 labda. Na ikitokea nimeliwa kajero kangu hakaniumi sana. Si jero tu!!

Siku moja nipo kituo cha kubetia (Premier) nikashuhudia jamaa mmoja anaweka stake ya 450,000 kwenye Bet of the day.
Kwamba Juve, Atletico na Santos wote washinde. Odds zilikua 11.

Na kweli kesho kuchek matokeo timu zote zimeshinda.
Kwahiyo nikapiga Hesabu jamaa atakua alilamba zaidi ya Millions 4+.

Daaah... Nikashawishika.
Bet of the Day ilofatia namie nikajitutumua. Kwa Mara ya kwanza nikaweka ka 10,000 kangu nikatulia. Odds zilikua 10.
Khaaaa... Kweli nikashinda.
Kesho mapeema nikaenda pale Premier (Mwananyamala A kuelekea Komakoma) nikavuta 100,000 yangu safiii...

Basi nikazidi kupata confidence.
Kumbe kuna hela za burebure namna hii.
Basi ikawa stake zangu natupia kuanzia 10, 000 kwenda juu..
Siku nimepinda sana, naweka 5000. Mara nakula, Mara naliwa.

Nakumbuka Mara ya mwisho kula hela nyingi ni Final ya UEFA.
Bet of the day ilikua Madrid ashinde ndani ya dakika 90 na pia timu zote zifungane magoli.
Odds zilikua 7. Nikaweka stake ya 15,000.

Kweli bana, wakatoka 4-1.
Kesho nikavuta 90,000 yangu safiiii....

Nikaendelea kama kawaida.
Nakula, naliwa...

Sasa Leo :
Nikakaa chini na kufanya Auditing ya biashara hii.
Nimeliwa shingapi.
Nimekula shingapi.
Net profit shingapi.

Bahati nzuri huwa nabeti online.
Hivo records zote ninazo.
Nimepitia accounts zangu zote Mbet, Premier Bet, Sportpesa, Mkekabet na Princess Bet.

Total Profit made is 177,000.
Total Loss incurred is 397,500.
Net Profit is -220,500.

Hapo sijagusia mikeka ya bukubuku nayowekaga kila siku kwenye Jackpot ya Perfect 12 ya Mbet. Kila siku naliwa tu.

Yani kifupi ni kuwa mwisho Wa siku mimi ni Loser.

Kubeti ni mchezo Wa kuhamisha pesa toka kwa masikini kuwajazia Matajiri.
Nimeachana na habari za kubeti Rasmi Leo hii 30 July 2017.

Mdogo wenu CCNP

Pole sana mkuu
 
Ukiona unapata hasara kubwa jua hujui kubeti. Aliyekutanmanisha mkeka hakukufunza na namna ya kutengeneza mikeka yenye akili
 
Kubeti siwezi acha iaseee,,,one amongst of the good business.
Screenshot_20210112-194005.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
luhilaseko pole sana ndugu kwa kuchelewa kubet basketball..mpaka hivi sasa nimenunua gari discovery 3 mil 48 kwa kubet basketball tu..Nawaangalia tu wanaoponda betting,acheni kubet football karibuni basketball uku pesa nje nje
Mwamba bado uko kwenye harakati?mi niko vzur ktk football,nataka unipe A,B,C za basketball

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Unaweka over 80.5, timu inaishia point 80, ume loss. Bado dakika 6 unahitaji timu ifunge points 5 tu lakini inashindikana, ume loss. Round ya 1,2,3 timu imefunga points 24,27, 22 lakini unakuta round ya 4 imefunga point 11 tu na over yako ya 85.5 ume loss. Ukicheza under ndio hatari zaidi.

Basketball betting stress stress stress na hatari kwa afya yako.
 
Unaweka over 80.5, timu inaishia point 80, ume loss. Bado dakika 6 unahitaji timu ifunge points 5 tu lakini inashindikana, ume loss. Round ya 1,2,3 timu imefunga points 24,27, 22 lakini unakuta round ya 4 imefunga point 11 tu na over yako ya 85.5 ume loss. Ukicheza under ndio hatari zaidi.

Basketball betting stress stress stress na hatari kwa afya yako.
[emoji23][emoji23] uchawi upo aisee
 
Watu wanaoipatia betting siku zote hawazidi timu 5 kwa Bet moja! Na inakuwa na amount nene! Ukiweka buku tano unataka ule laki siku zote utaliwa! Weka timu 3,4 ama 5 weka laki ama laki 2. Shinda laki 3 hadi 4 nenda kanunue cement ya laki nyingine utajua mwenyewe..

🤔
 
Wakuu hii Michezo haina faida yoyote... Ukiona mtu anasifia kuwa amepata ujue huyo katumika Kama Mfano ili kuwavuta wengi... Ni mmoja katika elfu Moja. Kimsingi Mataifa Yetu ya Africa yamejiingiza katika hii Michezo mapema Mno kabla hata Uchumi haujasimama. Mtu anaishia kufilisika Kabisa na Hana Cha kufanya... Anabaki maskini wa kutupwa. Wenzetu angalau wana Huduma za kijamii na kiutu kwa Watu maskini na wasiojiweza
 
Kweli inawezekana uchawi upo kabisa nimeshaloose mechi kama mbili hivi kwa tofauti ya 0.5 tu yaana umeweka over 150.5 inatoa 150. Unaweka mechi hata mbili tu lakini moja lazima ikatae.
 
Back
Top Bottom