Kuboronga kwa Taifa Stars, TFF na kumng'ang'ani Mkwassa

mwembemdogo

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2016
Posts
2,282
Reaction score
1,252
Hakika TFF sidhani kama wana dhamira ya kuinua soka la Tanzania.TFF in kikundi cha watu wababaishaji waliojipanga kushusha soka la Tanzania kuanzia Timu ya Taifa mpaka Vilabu vyetu huku wakipiga Hela za FIFA.

TFF pamoja Na kujua kabisa kuwa Kocha mzawa Charles Boniface Mkwassa ameshindwa kuifundisha timu hiyo lakini TFF imemng'ang'ania Kocha huyo Na hakuna juhudi zozote za makusudi za kumtafuta Kocha mpya hali ambayo tunahisi kuna maslahi binafsi katika mkataba wake.

Tunaviomba vyombo husika ikiwa pamoja Na Waziri husika zichukuliwe hatua za kuliokoa Soka la Tanzania.
 
Kwahiyo akiondoka mkwasa timu itafanya vizuri? Ivi kwa mpira wetu unavyo endeshwa unategemea akaondokewa mkwasa kutakakua na mabadiliko!!!
 
Sijaona mchango wa Mkwasa kama Kocha kwa Taifa Stars.Mechi na Zimbabwe ilituacha uchi sana.Nahisi hata wenyewe walijilaumu kucheza na sisi maana hakuna chochote walichojifunza.
 
niambie ni kocha gani aliyeleta mafanikio tanzania? mfumo wetu wa soka ndio umetufikisha hapa, hata angekuja morinyo tutatakua tukifungwa tu
 
Nafasi ya 144 na hakuna juhudi zozote za kutoka tulipo,shikamoo Ti elfu elfu.
 
Tatizo letu siyo kocha wachawi ni sisi wenyewe we unataka afukuzwe mkwasa aletwe nan Ttzo lilopo hatupo seriously na tunacho kifanya
 
Hamna hela ya kumlipa kocha wa kigeni, mkwasa anadai mshahara wa miezi mingi mwenyewe hajalipwa
 
Tuanzisheni michezo mipya kama huu wa Kabadi... Jiulize kwa nini wazungu wachezaji wanaenda kwenye mechi wamevaa suti... Ukipata jibu lake na tatizo letu kwenye soka litapatikana
 
Huyu mkwasa huwa ni kocha msaidizi tuuu ..., na hii ndiyo nafasi yake siku zote
 
Kwa kwel hakuna tunaloweza sio mpira sio mengineyo. Nchi haina mipango yoyote ya kukwamua soka letu, Ni bora kuwaachia wanayoyaweza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…