Hiyo ni kweli kabisa. Hao jamaa ni wale watu wanaowekeana mikataba na Bank na makampuni ya kuuza magari. Watu huchukua mkopo wa gari na anatokomea. Anaacha kulipa deni hilo kwa makusudi au kwa kushindwa kuwa na pesa.
Bank huwaarifu hawa jamaa na wao kazi yao ni kulitafuta gari na kulichukua. Kwa sababu wenye magari huwa wakali sana sana kuona magari yao yanachukuliwa, mara nyingi wanakuwa kama wanayaiba na mwisho ndiyo wanamjulisha mwenye gari kuwa gari lake limechukuliwa na sanasana watampa documents zake au vitu vilivyokuwa ndani. Nafikiri ni sheria ambayo unaponunua gari kwa mkopo basi unaukubali. Ila si unajua watu wanasahau?
Sasa hao jamaa wanavyofanya kazi, nafikiri TV Station fulani au Discovery ndiyo waliweka mkataba nao kuwa watakuwa wanapiga Video jinsi wanavyofanya kazi. Kuna program kama hizi nyingi sana USA. Kuna zile za Wagoni za kufumania jamaa zake Mwigulu Nchemba, kuna za Wapelelezi, Reality TV kwenye family, Big Brothers, makundi ya watu nk
Hili jamaa lilikuwa jinga sana. Wee unaona kimama kina MKANDA MWEUSI, ni alama tosha kuwa huyo si wa kawaida.