Kenya 2022 Kuchafua uchaguzi wa Kenya kwa kisingizio cha ukabila ni kujilisha upepo

Kenya 2022 Kuchafua uchaguzi wa Kenya kwa kisingizio cha ukabila ni kujilisha upepo

Kenya 2022 General Election

Mbogi

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2021
Posts
803
Reaction score
997
Nianze kwa kuwapongeza ndugu zetu wakenya kwa kumpata Rais aliyetokana na uchaguzi ulio huru, haki na uwazi ambao pengine siyo somo kwa waafrika tu bali pia hata katika baadhi ya mataifa ya mabara mengine.

Humu wamejitokeza wanaJF ambao wamejipa kazi ya kuchafua jitihada nzuri Sana zilizo fanywa na tume ya uchaguzi ya Kenya kwa kujificha katika kupotosha kuwa uchaguzi ulitawaliwa na ukabila.

Jitihada hizi za wapotoshaji zinavyo viashiria vya kutumia upotoshaji huu kutaka kuhalalisha udhaifu wa mwenendo wa chaguzi zetu. Tunadhani ingekuwa busara na heshima kujadili funzo kubwa juu ya uchaguzi huu kuliko kuanza kujificha katika shamba la karanga.

Dkt. Ruto aliyechaguliwa ni mkalenjin aliyeungwa mkono na kabila kubwa la wakikuyu.

Odinga ameshindwa pamoja na kuungwa mkono na Rais Uhuru ambaye ni mkikuyu.

"Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni"

Hakika lazima tukubali kuwa tunalo la kujifunza katika uchaguzi huu ili tupige hatua maana hata wao hapo awali wakifanya vibaya Sana ila wakakubali udhaifu wao na leo wamekuwa mfano watakaokuwa wa mfano.

Tuwapongeze na mliojipa kazi ya kuficha udhaifu wa chaguzi zetu kwa kutumia ukabila MUACHE KABISA.
 
Ahsante mkuu,,
Mataga hayana aibu ,,Wana Hoja za kijinga Sana,,,Ubora wa IEBC hauwezi kufananishwa na NEC ya Mahera ....NEC YA JECHA NA MAHERA NI UOZO MTUPU.
 
Back
Top Bottom